Katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa soko la pamba mkoa wa Simiyu umeandaa mkakati
maalum wa miaka mitano (2019-2024) wa mapinduzi ya kilimo cha zao hilo ili
kujibu changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa Wadau wa Pamba uliofanyika uliofanyika
Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi kwa lengo la kuboresha Mkakati maalum wa
Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka
mitano 2019-2014,
Akifungua
Mkutano huo Mtaka amesema upo umuhimu mkubwa kwa Mkoa wa Simiyu kuwa na
kiwanda/viwanda vya kuongeza thamani ya zao la pamba ikiwemo viwanda vya nguo
kama suluhisho la soko la pamba kwa wakulima.
“Kama hatutakuwa na viwanda vinavyoongeza thamani
kwenye pamba,hata kama tukiongeza uzalishaji, itafika mahali tutatukanana tu,
maana pamba itakuwa nyingi na hakuna mtu wa kukununua na wanaonunua wanajua
hatuna kwa kuipeleka, kwa hiyo ni lazima tukubaliane na ndiyo maana tukasema
tuje na mkakati huu unaoanza na mkulima kuanzia kwenye kulima” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amesema ili kuwasaidia wakulima katika
upatikanaji wa mikopo ni vema benki zikaweka utaratibu rafiki wa kutoa mikopo
kwa wakulima huku akitoa wito kwa Benki Kuu kupitia Kurugenzi ya Sera kuandika
maandiko ya miradi ya mazao ya mikakati likiwemo pamba ambayo yatasaidia katika
kuyaongezea thamani mazao hayo.
Akiwasilisha mkakati huo kwa wadau wa pamba mkoani Simiyu,
Katibu Tawala Msaidizi wa Mipango na Uratibu Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus
Weginah amesema uongezaji thamani kwenye pamba mkoani Simiyu bado liko chini;
ambapo kwa sasa kinachofanyika ni kutengenisha pamba nyuzi, mbegu na kuchuja
mafuta, huku akibainisha kuwa matarajio ya mkoa ni kwenda kwenye hatua nyingine
zaidi ya kuchambua pamba.
Pamoja na kuongeza thamani ya zao la pamba wadau wa
pamba wametoa maoni mbalimbali katika kuboresha kilimo cha Pamba ili kiwe
chenye tija na kubainisha kuwa “Ili tuweze kuboresha kilimo cha pamba ni lazima
teknolojia zitakazokabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, wadudu
na magonjwa” alisema Epifania Temu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) Ukiriguru
“Mbegu ndiyo msingi wa tija ya pamba inayopaswa
kuzalishwa kwenye soko, hivyo kwenye eneo lililokubaliwa kuzalisha mbegu kama Meatu
na Igunga ginners (wenye viwanda vya kuchambua pamba) watakaokununua pamba ya
eneo wapewe jukumu la kuzalisha mbegu ili kuwa na mwendelezo wa mbegu bora”
alisema Mkondo Cornelius Afisa Kilimo Mkuu, Wizara ya Kilimo.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka Gatsby Africa, Samweli
Kilua ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha kila mdau anatimiza wajibu wake
katika kuhakikisha mkakati huo unatekelezwa kwa ufanisi katika kuboresha kilimo
cha pamba.
Akifunga kikao Katibu Tawalawa Mkoa wa Simiyu, Bw.
Jumanne Sagini amesema mkakati wa mapinduzi ya kilimo cha pamba Mkoani Simiyu utatekelezwa
kwa vitendo na akazitaka Taasisi za fedha, viongozi na wataalam
wanaosimamia wakulima, vyama vya ushirika na wadau wengine waanze mazungumzo ili mkakati
huo utakapoanza kutekelezwa kuwe na uelewa wa pamoja kwa wadau wote.
Mkutano wa kuboresha mkakati maalum wa miaka mitano (2019-2024)
wa mapinduzi ya kilimo cha pamba ulijumuisha wadau mbalimbali wa kilimo cha
pamba ambao ni pamoja na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Simiyu, Watalaam
wa kilimo kutoka Taasisi za Utafiti wa Kilimo, Wizara ya Kilimo, Halmashauri na
Mkoa, Watendaji wa Taasisi za Fedha, viongozi
wa vyama vya msingi vya ushirika.
MWISHO
Mwenyekiti wa UVCCM
Taifa, Komredi Kheri James akitoa salamu zake kwa Wadau mbalimbali wa kilimo
cha pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha
Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014,
uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Komredi Enock Yakobo akizungumza na
Wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba katika Mkutano wa kuboresha Mkakati
maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi
cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wadau wa
kilimo cha pamba wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa
kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa
Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019
Mjini Bariadi.
Baadhi ya wadau wa
kilimo cha pamba Mkoani Simiyu wakifuatilia uwasilishaji wa Mkakati Maalum wa
Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka
mitano 2019-2014, katika Mkutano wa
kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Miradi wa
Gatsby Africa, Samweli Kilua akitoa taarifa ya namna shirika hilo
lilivyoshiriki katika uaandaaji wa Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha
Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, kwenye
mkutano wa kuboresha mkakati huo
uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Miradi
kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wwa Mataifa(UNDP), Amon Manyama akichangia
hoja Mkutano wa kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la
Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika
Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi
Seksheni ya Mipango na Uratibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw.
Donatus Weginah akiwasilisha mkakati wa maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao
la Pamba Mkoa wa Simiyu katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, katika Mkutano wa kuboresha Mkakati huo
uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mmoja wa Wawakilishi wa
Wakurugenzi na wamiliki wa Viwanda vya Kuchambua pamba kutoka kiwanda cha
Alliance Ginneries Ltd, akichangia hoja katika Mkutano wa kuboresha Mkakati
maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi
cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza, akichangia hoja Mkutano wa
kuboresha Mkakati maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa
Simiyu, katika kipindi cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019
Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa
wa Simiyu, Mariam Manyangu, akichangia hoja katika Mkutano wa kuboresha Mkakati
maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi
cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe akichangia hoja katika Mkutano wa kuboresha Mkakati
maalum wa Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi
cha miaka mitano 2019-2014, uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wadau wa
kilimo cha pamba Mkoani Simiyu wakifuatilia uwasilishaji wa Mkakati Maalum wa
Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka
mitano 2019-2014, katika Mkutano wa
kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wadau wa
kilimo cha pamba Mkoani Simiyu wakifuatilia uwasilishaji wa Mkakati Maalum wa
Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka
mitano 2019-2014, katika Mkutano wa
kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wadau wa
kilimo cha pamba Mkoani Simiyu wakifuatilia uwasilishaji wa Mkakati Maalum wa
Mapinduzi ya Kilimo cha Zao la Pamba Mkoa wa Simiyu, katika kipindi cha miaka
mitano 2019-2014, katika Mkutano wa
kuboresha Mkakati huo uliofanyika Agosti 28, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment