Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa jamii kupiga viya mila na
desturi zinazochangia watu kutotumia vyoo na kusisitiza kila kaya ione umuhimu
wa kuwa na choo bora, ikiwa ni njia ya kuboresha afya na usafi wa mazingira na
kuondokana na hatari ya magonjwa ya
mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Mtaka
ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo ambao
umefanyika Agosti 20, 2019 Mjini Bariadi ambapo amesema ni vema mila hizo zikapigwa vita ili jamii iweze
kurudi kwenye msingi.
“Kwenye
culture(tamaduni) zetu zipo sababu kwa nini baadhi ya watu walikuwa hawatumii
vyoo ambazo ni sababu za kitamaduni, kwamba baba mkwe hawezi kuchangia choo na mke wa kijana wake,
kwa hiyo ilikuwa hata ukijenga choo kwa baadhi ya kaya huko nyuma bado kulikuwa
na upinzani wa watumiaji”
“Unakuta
kuna choo kwenye kaya Fulani lakini bado wanajamii wa hiyo kaya wanaenda
kujisiri porini, huu ni utamaduni ambao ni lazima tuufanyie kampeni kama
tulivyofanya kampeni za kukataa mambo mengine kama ukeketaji ili jamii zetu
zirudi kwenye msingi, katika mkoa wetu kufikia mwezi Novemba, 2019 kila kaya
itakuwa na choo bora na kinachotumika” alisema Mtaka.
Aidha,
Mtaka amesema anaiunga mkono kwa asilimia 100 Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba
Ni Choo kwa kuwa ni kampeni inayolisaidia Taifa katika usafi wa mazingira na
kubainisha kuwa itakapofika mwezi Novemba 2019 kila kaya katika Mkoa wa Simiyu
itakuwa na choo bora kinachotumika.
Kwa
upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema Mkoa wa Simiyu umetajwa kuwa
na kaya 215,316 ambapo kati ya hizo zenye vyoo ni 208,856 sawa na asilimia 97 na zenye vyoo bora zikiwa ni
97,536 sawa na asilimia 46.7.
Naye
Mratibu wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya Anyitike
Mwakitalima amesema kampeni hii inafanyika kwa lengo la kusaidia
uboreshaji wa afya nchini kwa sababu magonjwa mengi yanatokana na uchafu na
njia moja wapo ya kukabili uchafu ni matumizi wa vyoo bora na unawaji wa mikono
kwa maji safi, salama na sabuni.
Amesema Serikali imeendelea kutoa elimu katika
jamii kuhusiana na matumizi na ujenzi wa vyoo bora katika ngazi ya kaya na
taasisi na tayari mikoa tisa imefikiwa, mkoa wa Simiyu ukiwa mkoa wa kumi
ambapo amesema lengo ni kuifikia mikoa yote 26 kabla ya Juni 2020
Kampeni
ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo itafanyika kwa takribani siku 20 katika
Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu
MWISHO
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie
Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana
yenye Ujumbe wa kampeni hiyo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Ofisini
kwake Mjini Bariadi kuashiria Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20,
2019.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie
Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana
yenye maandishi ya kampeni hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne
Sagini Ofisini katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa
Simiyu na timu ya hamasa ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Ofisini
kwake Mjini Bariadi wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20,
2019.
Balozi wa Kampeni ya
Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpotoakizungumza katika Uzinduzi
wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akipandisha bendera ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani
Simiyu Agosti 20, 2019.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie
Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto na Timu ya hamasa ya kampeni
hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani)
akizungumza katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa taarifa ya hali ya vyoo
Mkoani Simiyu wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo uliofanyika
Agosti 20, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa Mkoa wa Simiyu na timu ya hamasa ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo
Ofisini Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu
Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akionesha fulana yenye maneno ya Kampeni ya
Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo Ofisini kwake Mjini Bariadi mara baada
ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa Mkoa wa Simiyu na timu ya hamasa ya Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo
Ofisini Mjini Bariadi mara baada ya Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu
Agosti 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Kampeni ya Usichukulie
Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto Mjini Bariadi mara baada ya
Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Kutoka kulia ni Katibu
Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, Msanii na Balozi wa Kampeni ya Usichukulie Poa Nyumba Ni Choo
Mrisho Mpoto na Mratibu wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa mazingira kutoka Wizara
ya Afya, Bw. Anyitike Mwakitalima wakiteta jambo mara baada ya Uzinduzi wa
Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie
Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana
yenye Ujumbe wa kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Meatu, Bw. Fabian Manoza kwa naba ya
Wakurugenzi wa Mkoa wa Simiyu kuashiria Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mjini Bariadi.
Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019 .
Balozi wa Kampeni ya Usichukulie
Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto(kushoto) akimkabidhi fulana
yenye Ujumbe wa kampeni hiyo Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani
kwa naba ya Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu wakati wa Uzinduzi wa
Kampeni hiyo Mjini Bariadi. Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019 .
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akiteta jambo na Balozi wa Kampeni ya Usichukulie
Poa Nyumba Ni Choo Msanii Mrisho Mpoto Mjini Bariadi mara baada ya
Uzinduzi wa Kampeni hiyo Mkoani Simiyu Agosti 20, 2019.
.
0 comments:
Post a Comment