Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Luhaga Mpina amesema mapambano dhidi ya uvuvi haramu yamechangia kuongezeka
kwa kiasi cha samaki wakubwa ambapo kwa sasa upatikanaji wake ni asilimia 5.2
kutoka asilimia 0.3 ya awali kabla ya operesheni kuanza.
Ameyasema hayo Agosti 07, 2019 wakati akitembelea mabanda ya
wizara ya mifugo na uvuvi kwenye maonesho ya nane nane Kitaifa yanayofanyika
kwenye viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
Aidha, amesema kuwa katika upambanaji dhidi ya uvuvi haramu
kiwango cha samaki wazazi katika Ziwa Vikitoria kimeongezeka na kuvuka kiwango
kinachotakiwa hadi kufikia asilimia 5.2 kutoka asilimia 0.3 hali iliyopelekea
kupungua kwa samaki katika Ziwa hilo ambapo uhitaji wa samaki wazazi ni angalau
asilimia 3.2 .
“ uvuvi haramu ulipelekea kuongeza kwa kiwango cha samaki
wachanga ndani ya ziwa … karibia ziwa lote lilikuwa na samaki wachanga kwa
kiwango cha asilimia 96.6% ambapo kwa sasa kimeshuka na kufikia 62.8% jambo
hili lilipekea kupungua samaki wakubwa” alisema waziri mpina .
Ameongeza kuwa hali hiyo ilipelekea serikali kutumia kiasi cha
shilingi bilioni 56 kwa ajili ya kuagiza samaki wa vitoweo nje ya nchi ambapo
kimeshuka na kufikia bilioni 11 ambapo kiasi cha bilioni 40 kimeokolewa na
samaki aina ya sangara waliopo katika Ziwa Victoria limefikia tani 555 kutoka
417.
Katika hatua nyingine Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina
amesema kuwa wizara hiyo imejipanga kutatua changamoto ya chakula cha
mifugo hususani cha samaki ambacho kimekuwa kikiagizwa kutoka nje ya nchi, huku
akiwahakikishia wadau wa mifugo na uvuvi kuwa serikali imejipanga
kutafuta soko la uhakika ili wavuvi waweze kufuga na kuuza kwa urahisi.
MWISHO
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akipewa maelezo juu
ya teknolojia ya ufgaji wa samaki kupitia matanki, wakati alipotembelea mabanda
ya mifugo na uvuvi kwenye maonesho ya nane nane Kitaifa yanayofanyika kwenye
viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina(wa nne kushoto)
akipewa maelezo juu ya mfano wa teknolojia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba
ambayo hufanyika ziwani, wakati alipotembelea mabanda ya mifugo na uvuvi kwenye
maonesho ya nane nane Kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi Bariadi
mkoani Simiyu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina(mwenye miwani)
akipewa maelezo juu ya zana bora za kilimo zinazouzwa na Kampuni ya AGRICOM,
wakati alipotembelea mabanda ya mifugo na uvuvi kwenye Maonesho ya nane nane Kitaifa
yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina(wa pili mbele) akielekea
kwenye eneo la malisho ya mifugo, wakati alipotembelea mabanda ya mifugo na
uvuvi kwenye Maonesho ya nane nane Kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi
Bariadi mkoani Simiyu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiangalia ng,ombe
wanaofugwa kisasa, wakati alipotembelea mabanda ya mifugo na uvuvi kwenye Maonesho
ya nane nane Kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani
Simiyu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina(mwenye miwani) akipewa
maelezo namna mashine ya kuandaa chakula cha mifugo inavyofanya kazi, wakati
alipotembelea mabanda ya mifugo na uvuvi kwenye Maonesho ya nane nane Kitaifa
yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina(wa nne kushoto)
akipewa maelezo juu ya mfano wa teknolojia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba
ambayo hufanyika ziwani, wakati alipotembelea mabanda ya mifugo na uvuvi kwenye
maonesho ya nane nane Kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi Bariadi
mkoani Simiyu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina(wa nne kushoto)
akipewa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na wataalam wa ofisi yake, wakati
alipotembelea mabanda ya mifugo na uvuvi kwenye maonesho ya nane nane Kitaifa
yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina(wa nne kushoto)
akipewa maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na wataalam wa ofisi yake, wakati
alipotembelea mabanda ya mifugo na uvuvi kwenye maonesho ya nane nane Kitaifa
yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment