Serikali
kupitia waziri wa kilimo Japhet Hasunga imezindua Bima ya Kilimo
inayokinga mazao ya mkulima yanapokuwa shambani dhidi ya ukame, magonjwa
,wadudu waharibifu , mvua zilizozidi, moto, uharibifu unaoweza kusababishwa na
wanyapori, pamoja na mvua ya mawe.
Akizundua
bima hiyo Hasunga amesema kuwa wameamua kuanza na kipaumbele katika zao la
pamba ambalo huzalishwa kwa wingi Mkoani hapa lengo likiwa ni kuwainua wakulima
wenye vipato vya chini sambamba na kuwasaidia kupata msaada pindi wanapopatwa
na majanga ambapo bima hiyo inatarajiwa kuzinduliwa kwenye mazao mengine ya
kimkakati.
Aidha
waziri Hasunga amewataka wakulima walio katika vyama vya msingi vya ushirika
(AMCOS) kuhakikisha wanajiunga na bima ya mazao itakayowasaidia kukuza uchumi
wao na kuongeza kuwa idadi ya vyama vya ushirika katika mazao yote imeongezeka
na kufikia 11,331 ambapo kiwango cha ukaguzi wa vyama hivyo ni 70% na
kuisisitiza Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuongeza kasi ya ukaguzi ili
ifikie 100%.
“Bima hiyo
ya mazao itamsadia mkulima kuepukana na majanga mbalimbali na kwamba tumeamua
kulipa kipaumbele zao la pamba na baada ya hapa tutaenda Kagera kuzindua bima
kwenye zao la kahawa na serikali imelenga kuongeza kuwainua wakulima ili
waweze kuchangia katika kukuza pato la Taifa”alisema waziri Hasunga
Ameongeza
kuwa wakati umefika wa kuwachukulia hatua za kisheria waliohujumu vyama vya
ushirika awali huku akiwataka waliopewa majukumu kwenye AMCOS kuwa wachapakazi,
waadilifu na waaminifu katika utendaji kazi wao.
“nitoe
tamko kuwa viongozi wote wa vyama vya ushirika ambao wanawafanya ubadhilifu na
kuihujumu serikali ni lazima wachukuliwe hatua za kisheria na pia ni vyema sasa
sheria na miongozo iliyopo ibadilishwe ili iweze kuendana na kasi ya ushirika
uliopo” alisema
Awali
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC) dokta Elirehema Doriye
amesema kuwa shirika hilo linatarajia kutoa bima ya mazao kwa wakulima wote
nchini huku akiwashauri wakulima kukata bima ili kuepukana na changamoto.
Aidha
ameongeza kuwa bima hiyo itamsaidia mkulima kuweza kukopesheka kwenye mabenki
kwani tayari mkulima atakuwa na kinga hivyo kutoa mazao yatakayochangia
pato lake na Taifa kwa ujumla huku akiongeza kuwa shirika hilo linalomilikiwa
na serikali kwa asilimia mia moja 100% likiwafikia wakulima wote na kwa kuanzia
wataanza na wakulima wadogo.
Pamoja na
hayo ameongeza kuwa bima hiyo ina manufaa makubwa kwa mkulima na
itamkomboa kutoka katika kilimo kidogo na kwenda kikubwa kitakachomuwezesha
kuwekeza katika kilimo cha kisasa bila kuwa na hofu ya kupoteza mtaji
aliowekeza shambani ikiwa sekta kilimo imeajiri zaidi ya 75% ya Watanzania.
Kwa upande
wake Kamishina wa Bima hapa nchini Dkt. Mussa Juma ameeleza kuwa lengo la bima
hiyo ni kusaidia kuinua kipato cha watu wenye kipato cha chini ili waweze
kuchangia katika ukuzaji wa uchumi wa nchi .
Mbali na
hayo amesema kuwa uchumi wa nchi unategemea sekta mbalimbali ambazo ni kama
kilimo, uvuvi, mifugo, madini na ili kuwa na viwanda ambavyo vinaweza kusaidia
kukuza uchumi wa nchi lazma kuwe na namna ya kudhibiti majanga.
Hata hivyo
ameongeza kuwa bima ambazo zinahusu watu wengi hasa wenye kipato cha chini
mamlaka imeona iweze kuwafikia kwa namna moja nyingine.
Awali
akimkaribisha waziri Hasunga mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema kuwa
mkoa umejiandaa kikamilifu kusaidiana na NIC katika kuhakikisha zaidi ya
wakulima 100,000 wa pamba waliosajiliwa wanapata bima ya mazao.
MWISHO
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga akionesha nakala ya Mpango wa Bima ya Mazao kwa viongozi na wananchi mara baada ya
kuzindua bima hiyo Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka
2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri
wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la
Bima ya Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye nakala ya Mpango wa Bima ya Mazao
mara baada ya kuzindua bima hiyo Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki
Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka nakala ya Mpango wa Bima ya Mazao mara baada ya kuzindua bima hiyo Agosti 03,
2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda
ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga akipandisha bendera ya Bima ya Mazao katika Banda la Shirika la
Bima ya Mazao kama ishara ya kuzindua
rasmi bima hiyo Agosti 03, 2019 katika
Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa
Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi
wakishuhudia zoezi la uzinduzi wa Bima ya Mazao lililofanywa na Waziri wa
Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019
yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wwa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza
kabla ya kumkaribisha Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga kuzungumza na
wananchi na kuzindua rasmi bima ya mazao, Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki
Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akitoa neon
la shukrani mara baaada ya uzinduzi wa Bima ya mazao Agosti 03, 2019 katika Maonesho
ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki
Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga akimkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika , Dkt.
Titus Kamani nakala ya Mpango wa Bima ya
Mazao mara baada ya kuzindua bima hiyo
Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea
katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani
Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Bima ya Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye
nakala ya Mpango wa Bima ya Mazao
mara baada ya kuzindua bima hiyo Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki
Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika , Dkt. Titus Kamani
akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(kulia) wakati
alipotembelea banda la Maendeleo ya Ushirika Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki
Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Kutoka kushoto Waziri
wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa
(NIC), Dkt. Elirehema Doriye na
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika , Dkt. Titus Kamani wakiteta jambo, mara baada ya kuzindua bima
ya mazao Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019
yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa
wa Simiyu na wawakilishi wa taasisi zilipokea vyeti vya kutambua mchango wake
katika kilimo, mifugo na uvuvi, Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya
Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Waziri
wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(wan ne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa mkoa wa Simiyu na watumishi wa Shirika la Bima la Taifa Agosti 03, 2019 mara baada ya kuzindua bima
ya mazao, katika Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya
Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Dkt. Elirehema Doriye(kulia) akimkabidhi Mfuko
Mbadala Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, mara baada ya kuzindua bima
ya mazao, katika Maonesho ya Nanenane
Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya
Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika , Dkt. Titus Kamani
akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga wakati wa zoezi
la uzinduzi wa bima ya mazao Agosti 03,
2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki
Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya kilimo, Mhandisi. Mathew Mtigumwe akizungumza kwenye zoezi maalum la
uzinduzi wa bima ya mazao, Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa
mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda
ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Mazao
kutoka Wizara ya kilimo, akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet
Hasunga wakati alipotembelea mabanda ya
wizara hiyo, Agosti 03, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka
2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa
Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Banda la ASDP kwenye
Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019,
yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya viongozi na
wananchi wakipita kwenye mabanda ya maonesho kwa ajili ya kujionea huduma na bidhaa mbalimbali, kwenye
Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019,
yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja Vya Nyakabindi
Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Banda
la Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU)
0 comments:
Post a Comment