Thursday, August 8, 2019

HASUNGA AZITAKA TAASISI ZA FEDHA KUWAWEZESHA WAKULIMA ILI KUONGEZA MCHANGO WA KILIMO KIUCHUMI


Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga ametoa wito kwa Taasisi za Fedha kuhakikisha kuwa zinawafikia wakulima katika kuwezesha shughuli za kilimo ili kuongeza mchango wa kilimo katika pato la Taifa, upatikanaji wa chakula na ajira kwa Watanzania wengi, ambapo mpaka sasa takribani asilimia 65 hadi 75 wameajiriwa au kujiajiri kupitia kilimo.

Waziri Hasunga ameyasema hayo wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya Taasisi za fedha katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea, Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Amesema nchi inaweza kutoka hapa ilipo na ikasogea kwa haraka ikiwa kilimo kitawezeshwa ipasavyo kwa kuwa kilimo kikiwezeshwa kinaweza kuongeza mchango wake katika pato la Taifa.

“ Imani yangu ni kwamba nchi hii inaweza kutoka hapa ilipo kama tutakiwezesha kilimo kina uwezo wa kuongeza mchango wake kwenye pato la Taifa, upatikanaji wa fedha za kigeni, usalama wa chakula, kutoa ajira kwa watu wengi ambapo mpaka sasa hivi tuna karibu asilimia 65 hadi 75 wameajiriwa kwenye kilimo” alisema Mhe. Hasunga.

Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kufanya mabadiliko makubwa ya kuihamisha Sekta ya Kilimo kutoka kwenye kuwa sekta kujikumu na kuwa mhimili wa kweli wa ujenzi wa uchumi wa nchi na uchumi wa viwanda.

Aidha, amesema pamoja na kuwawezesha wakulima ni vema Taasisi za fedha zikatambua nafasi yake katika kuwawezesha mitaji wamiliki wa viwanda vinavyoongeza thamani mazao ya kilimo ili viweze kujengwa viwanda vya kuongeza thamani mazao mbalimbali.

Kwa upande wake  Meneja wa NMB Kanda Magharibi, Bw. Sospeter Magesse amesema Benki hiyo tayari inafanya kazi na wakulima na akamhakikishia Mhe. Waziri kuwa itajipanga kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha inawafikia na kuwawezesha wakulima wengi zaidi.
MWISHO
Mtaalam wa kilimo akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ( wa pili kushoto) na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede ( wa tatu kushoto) wakati walipotembelea  vipando vya mazao  ya kilimo, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mtaalamu wa TANESCO akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (kulia) na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede ( wa pili kulia) wakati walipotembelea banda la maonesho la TANESCO, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akifafanua jambo kwa Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (kulia) wakati alipotembelea Mabanda ya Mifugo ya Mkoa huo, Agosti 05, 2019 kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mtaalam wa kilimo akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga , Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede  na viongozi wengine wakati walipotembelea  vipando vya mazao  ya kilimo, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (kulia) akimweleza jambo Mtaalamu wa TANESCO wakati yeye , Waziri wa kioimo na viongozi wengine walipotembelea banda la maonesho la TANESCO, Agosti 05, 2019 kwenye  Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baadhi ya viongozi wakiangali baadhi ya bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi wakiangalia baadhi ya mabanda ya wajasiriamali wakati walipotembelea mabanda ya maonesho, Agosti 05, 2019 kwenye  Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ( wa tano kulia) na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (wa sita kulia) wakiangalia ufugaji bora wa kuku wakati walipotembelea  mabanda ya mifugo, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ( katikati)  akioneshwa mbegu bora za mahindi zinazozalishwa   na PANNAR wakati walipotembelea  mabanda ya mifugo, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ( katikati)  akioneshwa mbegu bora za mahindi zinazozalishwa   na PANNAR wakati walipotembelea  mabanda ya mifugo, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.



Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ( mwenye kofia kulia)  akipewa maelezo juu ya ufugaji wa samaki kwa kutumia mabwawa  alipotembelea   mabanda ya mifugo, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mtaalam wa kilimo akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga , Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede  na viongozi wengine wakati walipotembelea  vipando vya mazao  ya kilimo, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga , akizungumza na baadhi ya viongozi na wataalam wa Halmashauri ya Mji wa Bunda wakati alipotembelea   vipando vya mazao  ya kilimo, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baaadhi ya wananchi wakipata huduma katika Banda la Chuo Kikuu cha Kilimo, SOKOINE katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na viongozi wengine wakiangalia baadhi ya vifaa vya TANESCO vilivyowekwa katika banda lao kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi, katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baadhi ya viongozi na waannchi wakipata huduma katika Banda la maonesho la ASDP katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akimuonesha jambo  Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (kulia) wakati alipotembelea  Mabanda ya Taasisi zilizo chini ya wizara, Agosti 05, 2019 kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga(Mwenye Ushungi) akiwaongoza Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Prof. Dkt. Ratlan Pardede kuelekea kwenye ukaguzi wa mabanda ya Mifugo ya Mkoa wa Shinyanga, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mtaalam kutoka TEMESA akitoa maelezo  kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga  juu ya huduma zinazotelewa na TEMESA, wakati walipotembelea banda la Taasisi hiyo Agosti 05, 2019 kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Mtaalam kutoka TEMESA akitoa maelezo  kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga  juu ya huduma zinazotelewa na TEMESA, wakati walipotembelea banda la Taasisi hiyo Agosti 05, 2019 kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baadhi ya wananchi wakipatiwa  huduma katika banda la Jeshi la polisi kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa benki ya NMB wakati alipotembelea  banda la benki hiyo Agosti 05, 2019 kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Afisa kutoka TAHA akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga kuhusu namna TAHA inavyofanya kazi, wakati alipotembelea   Banda la TAHA, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu

Mfano wa Bustani za nyumbani za mbogamboga zilizopo katika Vipando vya HALMASHAURI YA Mji wa Bunda,  katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga , akitoa maelekezo kwa  baadhi ya viongozi na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu alipotembelea   vipando vya mazao  ya kilimo, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akiwa na viongozi wengine wakikagua   vipando vya mazao  ya kilimo, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baadhi ya wananchi wakipata huduma katika Banda la Maonesho la Shirika la Bima la Taifa(NIC) katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baadhi ya wananchi wakipata huduma katika Banda la Maonesho la Shirika la Bima la Taifa(NIC) katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kushoto), akipewa maelezo ya mfano wa namna ufugaji kwa kutumia vizimba  unavyokuwa, wakati alipotembelea   Banda la PASS, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga ( kushoto), akizungumza na wataalam kutoka AGRICOM ambayo inajishughulisha na uuzaji wa zana bora za kisasa, wakati alipotembelea   Banda la PASS, Agosti 05, 2019 katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baadhi ya zana za kisasa inayopatikana katika banda la AGRICOM katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baadhi ya zana za kisasa inayopatikana katika banda la AGRICOM katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yanayoendelea katika Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!