Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, MHE. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC), ambapo pia ametoa wito kwa wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda vya dawa
na vifaa tiba hapa nchini, ili kuiwezesha Bohari ya Dawa (MSD) ambayo ni
mzabuni wa dawa na vifaa tiba wa nchi za SADC kupunguza uagizaji wa dawa na
vifaa tiba nje ya nchi.
Mtaka
ametoa pongezi hizo Agosti 21, 2019 wakati akifunga mkutano wa siku tatu wa Menejimenti
ya Bohari ya Dawa (MSD) na mameneja wa Kanda za Bohari ya Dawa (MSD)
uliofanyika kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji.
Mtaka
amesema Bohari ya Dawa kama mzabuni wa dawa na vifaa tiba katika nchi za SADC
wanapaswa kutumia fursa ya Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kuhimiza
wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa
tiba.
“Nampongeza
Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na Pongezi nzuri kwa Mhe. Rais
ni pale ambapo nchi yetu ambao pia tuna faida ya kuwa mzabuni wa dawa na vifaa
tiba kwenye SADC; tutapata Watanzania wengi watakaochangamkia fursa ya kuwekeza
na kutumia nafasi ya Tanzania kuwa Mwenyekiti wa SADC tukiwa na Idadi ya watu
wengi kwenye soko la dawa na vifaa tiba” alisema Mtaka.
Aidha,
Mtaka ameongeza kuwa Kiwanda cha Vifaa tiba kinachotarajiwa kujengwa mkoani
Simiyu
Mkurugenzi Mkuu wa
Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurian Bwanakunu akizungumza na wajumbe wa
menejimenti ya MSD katika Mkutano wao maalum wa tathmini ya utendaji ambao
umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa
Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa akitoa taarifa ya yaliyofanyika katika
Mkutano wao maalum wa tathmini ya utendaji ambao umefanyika kwa muda wa siku
tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu mkutano amabo umehitimishwa na Mkuu wa mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Agosti 21, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na
Wakurugenzi na Mameneja wa Kanda wa Bohari ya Dawa (MSD) baada ya kufunga
Mkutano wao maalum wa tathmini ya utendaji ambao umefanyika kwa muda wa siku
tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa
Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa akimweleza
jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka Agosti 21, 2019 baada ya kufungwa kwa Mkutano maalum wa tathmini
ya utendaji wa Menejimenti ya MSD ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.

Mmoja wa Wakurugenzi
katika Bohari ya Dawa(MSD) akitoa taarifa wakati wa kufunga Mkutano maalum wa
tathmini ya utendaji wa Menejimenti ya MSD ambao umefanyika kwa muda wa siku
tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa mkoa wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Laurian Bwanakunu(wa pili kulia) na Wajumbe
wengine wa Menejimenti ya MSD baada ya kufungwa kwa Mkutano maalum wa tathmini
ya utendaji wa Menejimenti ya MSD ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa
Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa akimweleza
jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka Agosti 21, 2019 baada ya kufungwa kwa Mkutano maalum wa tathmini
ya utendaji wa Menejimenti ya MSD ambao umefanyika kwa muda wa siku tatu Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment