Friday, August 9, 2019

PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA KILIMO BIASHARA NANENANE SIMIYU


Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda, amefungua Kongamano la Kilimo Biashara katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayoendelea katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo amesema kilimo biashara kinaweza kutoa mwongozo wa changamoto ya tija ndogo katika kilimo; ikiwa ni pamoja na matumizi ya kilimo cha umwagiliaji, matumizi ya teknolojia sahihi katika uzalishaji na hifadhi ya mazao.

Mhe. Pinda ameyasema hayo Agosti 06, 2019  mjini Bariadi katika kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika wakati wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yanayofanyika Kitaifa Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Mizengo alisema kuwa ni vyema wakatumia teknolojia za kisasa zilizopo  ili waweze kupata tija kwenye kilimo ambacho kina mchango katika pato la Taifa na kubainisha kuwa mchango wake bado ni mdogo kutokana na sababu nyingi ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa hatua inayopelekea kilimo kutokuwa na tija ya kutosha.


Ameongeza kuwa hakuna haja kwa wakulima kulima kwa kutegemea mvua ilihali maeneo  mengi ya Mikoa ya Kanda ya Ziwa yanazungukwa na ZiwaVictoria  lenye maji mengi ambayo yakitumika vizuri wataweza kuzalisha mavuno mengi kwenye eneo dogo kupitia umwagiliaji na teknolojia za kisasa zilizopo.

“niishauri tu Mikoa hii ambayo inazungukwa na Ziwa lenye maji mengi ambayo nchi jirani zinatumia maji hayo kuzalisha mazao kutokana na umwagiliaji badala ya kutegemea mvua; unapotokea ukame unaathiri mazao hayo ipo haja ya kuona umuhimu wa kwenda  kwenye kilimo cha umwagiliaji”alisema waziri mkuu mstaafu Pinda

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema sekta ya kilimo ina uwezo wa kuongeza pato la Taifa kwani inachangia kwa asilimia 28.7 huku akibainisha kuwa tija ya uzalishaji kwa wakulima bado ipo chini huku akikisitiza matumizi sahihi ya ardhi na maji hususani kwenye shughuli za umwagiliaji.

Ameongeza kuwa licha ya asilimia 65.5 ya Watanzania kujiajiri kwenye sekta ya kilimo moja kwa moja asilimia 66% zinahitajika kwenye viwanda na kwamba zinatakiwa kuboreshwa ili ziweze kufikia angalau 80%.

Katika hatua nyingine Mhe. Hasunga ametoa wito kwa wawekezaji  kuwekeza kwenye viwanda vya mafuta kwani Serikali inatumia fedha nyingi kuagiza mafuta nje ya nchi licha ya kuwa mazao mengi yana malighafi ambazo zina uwezo wa kutengeneza mafuta ya kula zipo nchini.

“tuna mazao mengi ambayo malighafi zake zina uwezo wa kutengeza mafuta lakini serikali inatumia fedha nyingi kuagiza nje ambapo kwa mwaka ni tani 570,000 huku uwezo wa kuzalisha ukiwa ni tani 250,000 na katika hili tutatumia maamuzi magumu ili tuwekeze kwenye viwanda vya mafuta” alisema waziri Hasunga

Awali Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ameyataka  makundi ya wanawake, vijana  na waoneshaji kwa ujumla wake kutumia fursa ya uwepo wa Kongamano la Kilimo Biashra kujifunza ili waweze kuongeza ujuzi ambao utaenda sambamba na kutambua mnyororo wa thamani kwenye mazao na shughuli zao za kilimo.

Hata hivyo  Mkurugezi wa Mtendaji Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Tausi Kida amesema kuwa wakati umefika kwa wakulima kutumia maeneo madogo kuzalisha uzalishaji wenye tija unaoenda sambamba na mazao bora ambayo yatakuwa na uhakika kwenye masoko ya nje.
MWISHO.


Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda akifungua Kongamano la Kilimo Biashara katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Baadhi ya wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wajasiriamali wakimsikiliza Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda akifungua Kongamano la Kilimo Biashara katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baadhi ya wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara na wajasiriamali wakimsikiliza Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda akifungua Kongamano la Kilimo Biashara katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.


Mkurugenzi Mkuu wa ESRF Dkt. Tausi Kida akizungumza katika Kongamano la Kilimo Biashara katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda  ( wa tatu kulia) akikagua baadhi ya bidhaa za wajasiriamali waliowezeshwa na Benki ya NBC mara baada ya kufungua  Kongamano la Kilimo Biashara katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda  ( wa tatu kulia) akikagua baadhi ya bidhaa za wajasiriamali waliowezeshwa na Benki ya NBC mara baada ya kufungua  Kongamano la Kilimo Biashara katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda  mara baada ya kuwasili Viwanja vya Nyakabindi  kwa ajili ya kufungua  Kongamano la Kilimo Biashara katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga  wakifurahia  jambo Kongamano la Kilimo Biashara katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga  akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, muda mfupi kabla ya kufungua Kongamano la Kilimo Biashara katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima (mwenye kofia mbele) akimuongoza Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda kutembelea mabanda ya maonesho katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa pili kushoto) na Maafisa wa Benki ya NMB wakifurahia jambo wakati alipowatembelea katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.


Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa tatu kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa wakulima ilipowatembelea katika Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa NMB katika Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya lZiwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  wawezeshaji wa Kongamano la Kilimo Biashara kwenye Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine wa kitaifa,   ilipowatembelea Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu,  Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda (kushoto) akisaini Kitabu cha wageni,   katika  Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu nne, Mhe. Mizengo Pinda akipokelewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, mara baada ya kuwasili kwa Viwanja vya  Nyakabindi  kwa lengo la kufungua kongamano la Kilimo biashara , katika  Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  Kamati ya Ulinzi na Usalama  ya mkoa  mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la Kilimo Biashara kwenye Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa pili kushoto)akiangalia ng’ombe wanaofugwa kisasa na JKT wakati wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa, Viwanja vya  Nyakabindi Bariadi Simiyu, (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa tatu kushoto)akiangalia nguo zinazoshonwa na kuuzwa na  JKT.Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa pili kushoto)akiangalia namna teknolojia ya ufugaji wa samaki
Viongozi wa Kitaifa na Mkoa wa wakimuongoza Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa pili kushoto) akiangalia namna teknolojia ya ufugaji wa samaki
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara kwenye Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa pili kulia)akisaini Kitabu cha wageni katika Banda la Benki ya CRDB , kwenye Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akiteta jambo na Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Bw. Sospeter Magesse   wakati alipotembelea banda la Benki ya NMB kwenye Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) akiangalia mafuta ya nazi yanayotengenezwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(JKT),   wakati alipotembelea banda la JKT kwenye Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda (wa nne kulia) akiangalia teknolojia ya ufugaji samaki kwa kutumia matanki  wakati alipotembelea eneo la JKT kwenye Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na maafisa wa JKT mara baada ya kufungua Kongamano la Kilimo Biashara kwenye  Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara(hawapo pichani)  ambalo lilifunguliwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda, Agosti 06, 2019 kwenye  Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Mizengo Pinda ( wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa idara mbalimbali katika Wizara ya kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi baada ya kufungua Kongamano la Kilimo Biashara Agosti 06, 2019 kwenye Maonesho ya Nanenane  yanayofanyika Kitaifa mwaka 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!