Friday, August 9, 2019

WAZIRI MKUU AZINDUA MFUMO WA KANZI DATA YA KUSAJILI WAKULIMA, AWAHAKIKISHIA WAKULIMA PAMBA YAO KUNUNULIWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezindua mifumo mitatu  ya kielekroniki inayolenga kuboresha na kurahisisha ufanyaji wa biashara za mazao ya Kilimo  ambayo ni mfumo wa kusajili  wakulima nchini, mfumo wa soko la bidhaa na mfumo wa uingizaji na ununuzi wa mazao nje ya nchi.

Mhe. Waziri Mkuu amefanya uzinduzi huo Agosti 08, 2019 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu kwenye Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, ambapo pia amewahakikishia wakulima wote wa pamba kuwa pamba yote itanunuliwa na kuondoka mikononi mwao.

Aidha, amezitaka benki zote zinatoa fedha kwa wanunuzi wa pamba kutoa taarifa kwa serikali juu ya fedha walizotoa kwa wanunuzi wa pamba, ili Serikali ijue na kuweka mikakati ya usimamizi katika kuhakikisha fedha zote zinapelekwa kwa wakulima wa pamba kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo.

“Tunataka pamba yote itoke haraka mikononi mwa wakulima kwa sababu hali ya hewa inabadilika, tunataka wakulima wapate fedha zao waanze mpango mpya wa kilimo cha mwaka ujao, wapeleke watoto wote shule wafanye na mambo mengine,”

“Haya ndiyo matakwa na maagizo yaliyotolewa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa hiyo wakulima katika hili muwe na amani kabisa kwamba pamba inakuja kununuliwa na wanunuzi wako karibu katika wilaya zote” alisisitiza Mhe. Waziri Mkuu.

Katika hatua nyingine Mhe. Majaliwa amewaagiza maafisa mifugo kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu kuacha tabia ya kupiga chapa na kuweka alama kwenye mifugo kwa kuchoma ngozi jambo ambalo amesema linaharibu na kupunguza ubora na thamani ya ngozi hiyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema katika kutafuta suluhisho la changamoto ya bei ya pamba Mkoa wa Simiyu unaomba kijengwe kiwanda cha nguo huku akibainisha kuwa tayari barua imewasilishwa Benki Kuu kuomba idara ya sera na utafiti kuandaa andiko/ kufanya upembuzi yakinifu kuhusu uwepo wa kiwanda cha nguo

Ameongeza kuwa Mkoa wa Simiyu pia ni kwamba unaomba andiko la mradi wa ujenzi wa kiwanda cha nguo litakapokamilishwa Serikali ione uwezekano wa kutoa fedha za miradi ya kimkakati kwa Halmashauri za mkoa wa Simiyu ili kiwanda hicho kiweze kujengwa kupitia fedha hizo.

“Mhe. Waziri Mkuu tumemuona Mhe. Naibu Waziri wa Fedha akirudisha fedha kutoka kwenye Halmashauri zilizoshindwa kufanya miradi ya kimkakati, mapendekezo yangu Mhe. Waziri Mkuu sisi Simiyu tuna Halmashauri sita tunaomba tukipata andiko la mradi wa kiwanda cha nguo, zile fedha za miradi ya kimkakati ambazo Halmashauri nyingi zimeshindwa kufanya tuweze kwenda kwenye kiwanda cha nguo” alisema Mtaka.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mhe. Waziri Mkuu Waziri wa kilimo, Mhe. Japhet Hasunga amesema Wizara imejipanga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuimarisha kilimo cha umwagiliaji, kutumia mbegu bora zinazovumilia ukame na magonjwa na zinazotoa mavuno mengi

Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yameongozwa na Kauli Mbiu “Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa Nchi” na yameadhimishwa kwa mara ya pili sasa katika Kanda ya Ziwa Mshariki ambapo na mwaka 2020 yatafanyika tena Kitaifa Mkoani Simiyu.
MWISHO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akionesha vitabu vyenye mifumo mitatu inayoboresha na kurahisisha ufanyaji wa biashara za mazao ya Kilimo ambayo ameizindua katika Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akionesha vitabu vyenye mifumo mitatu inayoboresha na kurahisisha ufanyaji wa biashara za mazao ya Kilimo ambayo ameizindua katika Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akionesha Kifaa maalum kwa ajili ya  mifumo mitatu inayoboresha na kurahisisha ufanyaji wa biashara za mazao ya Kilimo ambayo ameizindua katika Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akitembelea mabanda ya Maonesho ya Taasisi mbalimbali  mara baada ya kuwasili Bariadi kwa ajili ya Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akitembelea mabanda ya Maonesho ya Taasisi mbalimbali  mara baada ya kuwasili Bariadi kwa ajili ya Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na viongozi wetu wa Mkoa wakiimba wimbo wa Taifa ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi Halfa ya ya Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiondoka katika Viwanja vya Nyakabindi mara baada ya kuhitimisha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, Bariadi Simiyu

Baadhi ya wakuu wa Wilaya za mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga  wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa katika Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.


Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akitoa salamu za chama katika Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wengine wakicheza wimbo wa asili ya wauskuma pamoja na Msanii Elizabeth Maliganya katika Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungamza jambo na mwananchi ambaye yupo  Viwanja vya Nyakabindi wakati wa Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, Bariadi Simiyu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia namna mazao ya kilimo yanavyopandwa katika ujuzi tofauti mara baada ya kuwasili  Viwanja vya Nyakabindi wakati wa Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, Bariadi Simiyu.


Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa  kwenye Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Vikundi vya Burudani vikitumbuiza kwenye Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu
Vipando vya Mbogamboga katika Viwanja vya Nanenane Nyakabindi eneo la JKT.

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kikombe na cheti Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, kwa kuwa mshindi wa kwanza katika kundi la Vyombo vya Ulinzi na Usalama, kwenye Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kikombe na cheti Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania kwa kuwa mshindi wa kwanza katika kundi la Taasisi za Fedha, kwenye Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kikombe na cheti Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, kwa kuwa mshindi wa kwanza katika kundi la Vyombo vya Ulinzi na Usalama, kwenye Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.

Mkurugenzi wa AGRICOM akipokea cheti  cha mshindi wa kwanza wa wanaouza bidhaa/zana bora za kilimo kwenye Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimpongeza mwakilishi wa CLOUDS MEDIA  Bw. Hassan Ngoma kutokana na CLOUDS MEDIA kuwa  MSHINDI WA KWANZA Katika  kundi la vyombo vya habari vya utangazaji kwenye Kilele cha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 Agosti 08, 2019, katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!