Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amezindua
rasmi kambi ya kitaaluma ya siku 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata
ufaulu hafifu (daraja sifuri) katika mtihani wa ‘Mock’, lengo likiwa ni kuwasaidia
waweze kuongeza ufaulu wao katika mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Novemba
2019.
Akizindua kambi hiyo Septemba 05, 2019 Mtaka amesema
wanafunzi hao watafundishwa masomo manne tu ambayo ni Kiswahili, Kiingereza
,Uraia(Civics) na Historia, hivyo akatoa wito kwa walimu mahiri waliochaguliwa
kuwafundisha wanafunzi hao kwa moyo na upendo ili wanafunzi hao waweze kupata
alama D na kuendelea katika mtihani wa Taifa.
“Hawa watoto wafundisheni masomo manne, Kiswahili,
Kiingereza, Historia na Civics; wafundisheni kwa moyo, wapeni mazoezi ya mara
kwa mara katika siku hizi 60 watakazokuwa kambini, muwasaidie watoke kwenye F
wapate angalau D nao wapate vyeti, kwa sababu hata ajira siku hizi kigezo ni
angalau mtu awe na cheti cha kidato cha nne” alisema Mtaka.
Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa jamii ya
Simiyu kuendelea kuwekeza kwenye elimu ili kuuwezesha mkoa kushindana kiuchumi
kwa kuwa maendeleo ya kiuchumi yanategemea maendeleo ya elimu katika eneo
husika.
Afisa Elimu mkoa wa Simiyu, Mwl.Ernest Hinju amesema
kati ya Wanafunzi 9956 waliofanya mtihani wa
Utimilifu (Mock), 1300 hawakupata alama D hata moja, hivyo waliopata
matokeo hafifu (daraja sifuri) wamewekwa pamoja wafundishwe masomo manne ili
waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa, huku waliopata daraja la kwanza
hadi la nne wakiendelea na kambi kufundishwa masomo yote.
Aidha, Hinju ameongeza kuwa kambi za kitaaluma zimechangia kuongeza ufaulu
kwenye Mtihani ya Taifa wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita,
ambapo katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ufaulu ulikuwa asilimia 74
mkoa ukiwa nafasi ya 14 kati ya mikoa 26, mwaka
2017 ufaulu asilimia 79.8 nafasi ya 11 na mwaka 2018 ufaulu asilimia
82.5 ukashika nafasi ya 9 kati ya mikoa
26.
Kwa upande wao wanafunzi wa kidato cha nne waliopo
kambini wameshukuru kuwekewa kambi hiyo
na wakaeleza imani yao juu ya uwepo wa kambi hiyo ambapo wameomba kambi za
kitaaluma Simiyu ziwe endelevu ili ziwasaidie kujifunza na kujiandaa vema na
mitihani ya Taifa hatimaye mkoa uweze kufanya vizuri.
“Tunawashukuru viongozi wetu na wazazi wetu kwa
kukubali kutuwekea kambi ya kitaaluma, ninashauri kambi hizi zisiishie kwetu
ziendelee na kwa wadogo zetu ili mkoa wetu uweze kuongeza ufaulu” alisema Esther
Nashoni mwanafunzi shule ya sekondari Bariadi(Bariadi)
Mkuu wa Shule ya Sekondari Simiyu, Mwl.Paul Susu amesema
walimu wamejiandaa vema katika kuwafundisha wanafunzi na kuwapa mitihani ya
mara kwa mara ili waweze kufanya vizuri, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali
wa elimu kujitolea katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuwe na miundombinu
ya kutosha itakayoongeza nafasi kwa kambi za kitaaluma kufanyika vizuri.
Kambi
ya kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha nne iliyozinduliwa Septemba 05, 2019
ilianza rasmi Septemba Mosi na inatarajiwa kufanyika ndani ya siku 60 kabla ya
kufanya Mtihani wa Taifa mwezi Novemba.
MWISHO
Baadhi ya wanafunzi wa
kidato cha nne, walimu na wadau wa elimu mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akizindua kambi ya
Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne, waliopata ufaulu hafifu katika
Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa
utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini
Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizindua kambi ya Kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha nne,
waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili waweze kuongeza ufaulu
katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika
Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa elimu wa Mkoa wa
Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya kambi maalum ya kitaaluma kwa
wanafunzi waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ wakati wa ufunguzi
wa kambi hiyo inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu
katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika
Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa elimu wa Mkoa wa
Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya kambi maalum ya kitaaluma kwa
wanafunzi waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ wakati wa ufunguzi
wa kambi hiyo inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu
katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika
Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wanafunzi wa
kidato cha nne, mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kambi ya Kitaaluma kwa
wanafunzi wa kidato cha nne, waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’
ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019 uzinduzi
huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Komredi Enock Yakobo akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne
waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ wakati wa ufunguzi wa kambi
hiyo inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika
mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba
05, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya walimu mahiri
na wadau wengine wa elimu mkoani Simiyu wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo
inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani
wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi huu umefanyika Septemba 05, 2019
Mjini Bariadi.
Mkuu wa Shule ya
Sekondari Simiyu ya Mjini Bariadi, Mwl. Paul Susu akieleza umuhimu wa kambi za kitaaluma wakati
wa uzinduzi wa kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata
ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi
hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi
huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa
Mkoa wa Simiyu na wadau wengine wa elimu
akiwepo mwandishi mashuhuru wa vitabu Richard Mabala(wa tatu kushoto)
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani)
wakati akifungua kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne Septemba
05, 2019 Mjini Bariadi , waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ ili
waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019.
Mwenyekiti wa Chama cha
Walimu Tanzania Mkoa wa Simiyu, akieleza umuhimu wa kambi za kitaaluma wakati
wa uzinduzi wa kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata
ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi
hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi
huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Mganga Mkuu wa
mkoa, Dkt. Mugune Maeka akieleza namna idara ya afya itakavyowahudUmia
wanafunzi wa kidato cha nne walio katika kambi ya kitaaluma, kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata
ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’ inayofanyika ili kuwasaidia wanafunzi
hao waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019, uzinduzi
huu umefanyika Septemba 05, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na
wadau wa elimu mkoani Simiyu, wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kambi ya Kitaaluma kwa
wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu katika Mtihani wa ‘Mock’
ili waweze kuongeza ufaulu katika mtihani wa Taifa utakaofanyika Novemba 2019 uzinduzi
huu umefanyika Septemba 05, 2019
0 comments:
Post a Comment