Mwekezaji kutoka
nchini Uturuki, Bw. Mustafa Albayram ameahidi kujenga viwanda viwili;
kiwanda cha nguo na kiwanda cha kutengeneza glasi katika eneo la Isanga Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu mwaka 2020, mara baada ya kuridhishwa na mazingira ya
uwekezaji ambapo viwanda hivyo
vinatarajia kuajiri wananchi takribani
2000.
Albayram ameyasema hayo Novemba 13, 2019 mara baada ya
kutembelea maeneo mbalimbali kwa lengo la kuangalia mazingira wezeshi kwa uwekezaji
wa viwanda, ambaye alifuatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof.
Elizabeth Kiondo kwa ziara ya siku mbili mkoani Simiyu.
Amesema endapo miundombinu yote muhimu hususani
umeme itawekwa kwa wakati katika eneo hilo uwekezaji huo utaanza mara tu baada
ya kukamilisha taratibu zote muhimu zinazohitajika ikiwa ni pamoja na usajili
wa kampuni na kutafuta hati miliki ya ardhi.
“Tumeamua kuwekeza Simiyu, kila kitu kikienda sawa
kiwanda cha nguo kinaweza kujengwa na kufanya kazi ndani ya miezi tisa mpaka
mwaka mmoja, kiwanda cha glasi ni mwaka mmoja; baada ya usajili wa kampuni
nitarudi tena Simiyu kukamilisha masuala ya hati miliki ya ardhi, sitaki
kumuangusha Mhe. Balozi maana amefanya mengi kwa ajili yetu,” alisema Albayram.
Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo amesema mwekezaji
ameridhishwa na eneo hilo na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa kutoa
ardhi bure huku akibainisha kuwa ombi kubwa la mwekezaji ni kuwa na nishati ya
kutosha kwa kuwa viwanda hivyo hususani kiwanda cha nguo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemhakikishia mwekezaji
huyo upatikanaji wa mahitaji yote muhimu na kuahidi kushirikiana na taasisi
zote za Serikali zinazohusika kuhakikisha anapata huduma zote kwa wakati na
bila urasimu wowote.
Kuhusu
suala la Umeme Mtaka amesema katika Bajeti ya mwaka 2019/2020 Wizara ya Nishati
kupitia Shirika la umeme TANESCO imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo
cha kupozea umeme(substation) ambacho kitajengwa karibu na eneo la uwekezaji
huo.
Mtaka
ameongeza kuwa mtazamo wa mkoa wa Simiyu ni kuwa na viwanda vichache
vinavyoajiri watu wengi badala ya kuwa na viwanda vingi vinavyoajiri watu
wachache, huku akitoa wito kwa wakulima wa pamba kulima pamba kwa wingi kwa
kuwa kiwanda cha nguo kitakuwa mkombozi wa kuongeza thamani ya zao la pamba na
itauzwa kwa bei ya uhakika.
Naye Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa pamba nchini,
Bw. Boaz Ogola amesema kujengwa kwa kiwanda cha nguo mkoani Simiyu kutasaidia wakulima
wa pamba kupata soko la uhakika kuondoa changamoto ya bei ya pamba kwa kuwa
kitapanua wigo wa soko la pamba, ambapo pamba inayotumika hapa ni nchini ni
asilimia 20-25 ya pamba yote inayozalishwa.
MWISHO
Mwekezaji kutoka nchini Uturuki, Bw. Mustafa Albayram
akizungumza na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu wakati alipotembelea eneo
la Isanga lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa Viwanda katika Halmashauri ya
Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake ambayo amembatana na Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
(kushoto) akisalimiana na Mwekezaji kutoka nchini Uturuki Bw. Mustafa Albayram
mara tu baada ya kuwasili Mjini Bariadi Novemba 13, 2019 kwa ziara ya siku
mbili yenye lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika viwanda ambaye
amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo(katikati).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto)akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini
Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo(wa tatu kushoto) ambaye alifuatana na Mwekezaji kutoka nchini
Uturuki Bw. Mustafa Albayram( wa nne kushoto)
na wadau wengine mara tu baada ya kuwasili Mjini Bariadi Novemba 13,
2019 kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji
katika viwanda.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akionesha moja ya eneo linalofaa kwa uwekezaji
katika Kata ya Nyakabindi Mjini Bariadi, wakati wa ziara ya Balozi wa Tanzania
nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo ambaye alifuatana na Mwekezaji kutoka
nchini Uturuki Bw. Mustafa Albayram mara tu baada ya kuwasili Mjini Bariadi
Novemba 13, 2019 kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kuangalia mazingira ya
uwekezaji katika viwanda.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini(kushoto) akisalimiana na Mwekezaji kutoka nchini
Uturuki Bw. Mustafa Albayram mara tu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege
wa Mwanza Novemba 13, 2019 kwa ajili ya
ziara ya siku mbili mkoani Simiyu yenye lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji
katika viwanda ambaye amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof.
Elizabeth Kiondo(katikati).
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu(mwenye shati jeupe katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo(wa saba kushoto) na Mwekezaji
kutoka nchini Uturuki Bw. Mustafa Albayram(wa sita kulia), viongozi mbalimbali
wa mkoa wa Simiyu na wadau wengine katika siku ya kwanza ya ziara mwekezaji
huyo na Mhe. Balozi mkoani Simiyu yenye lengo la kuangalia mazingira ya
uwekezaji katika viwanda.
Mwekezaji kutoka nchini
Uturuki Bw. Mustafa Albayram(kulia) akiwaonesha jambo Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini na
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
kutoka katika simu yake mara baada ya kutembelea eneo la Isanga
lililotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa Viwanda katika Halmashauri ya Mji wa
Bariadi mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake ambayo ameambatana na Balozi wa
Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof.
Elizabeth Kiondo na Mwekezaji kutoka nchini Uturuki Bw. Mustafa Albayram wakati
wa ziara yao mkoani Simiyu Novemba 13, 2019 yenye lengo la kuangalia mazingira
ya uwekezaji katika viwanda.
Mwekezaji kutoka nchini
Uturuki Bw. Mustafa Albayram akiangalia pamba inayochambuliwa katika kiwanda
cha kuchambua pamba cha NGS kilichopo Mjini Bariadi wakati wa ziara yake mkoani
Simiyu Novemba 13, 2019 yenye lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika
viwanda.
Mwekezaji kutoka nchini
Uturuki Bw. Mustafa Albayram(kulia) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
mara baada ya
kuwasili mkoani Simiyu Novemba 13, 2019 , kwa ajili ya ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu ambayo ameambatana na Balozi wa
Tanzania nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo(katikati)
Balozi wa Tanzania
nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya
viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa
ziara yake mkoani hapa Novemba 13, 2019 ambayo aliambatana na Mwekezaji kutoka
nchini Uturuki Bw. Mustafa Albayram ziara yenye lengo la kuangalia mazingira ya
uwekezaji katika viwanda.
Balozi wa Tanzania
nchini Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yao mkoani
hapa Novemba 13, 2019 yenye lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika
viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akizungumza jambo na Mwekezaji kutoka nchini Uturuki Bw.
Mustafa Albayram wakati ziara ya mwekezaji huyo aliyeambatana na Balozi wa
Tanzania nchini, Prof. Elizabeth Kiondo (hayupo pichani) wakati wa ziara yao
mkoani hapa Novemba 13, 2019 yenye lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji
katika viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akizungumza jambo wakati wa ziara ya Mwekezaji kutoka nchini Uturuki Bw. Mustafa
Albayram aliyeambatana na Balozi wa Tanzania nchini, Prof. Elizabeth Kiondo,
mkoani hapa Novemba 13, 2019 yenye lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji
katika viwanda.
Baadhi ya viongozi wa
Mkoa wa Simiyu wakijadiliana jambo wakati wa ziara ya Mwekezaji kutoka nchini
Uturuki Bw. Mustafa Albayram (kulia) aliyefuatana na Balozi wa Tanzania nchini,
Prof. Elizabeth Kiondo, mkoani hapa Novemba 13, 2019 yenye lengo la kuangalia
mazingira ya uwekezaji katika viwanda.
Baadhi ya viongozi wa
Mkoa wa Simiyu wakijadiliana jambo wakati wa ziara ya Mwekezaji kutoka nchini
Uturuki Bw. Mustafa Albayram (kulia) aliyefuatana na Balozi wa Tanzania nchini,
Prof. Elizabeth Kiondo, mkoani hapa Novemba 13, 2019 yenye lengo la kuangalia
mazingira ya uwekezaji katika viwanda.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini
Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege
wa Mwanza, kwa ajili ya ziara ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo ameongozana na
Mwekezaji kutoka nchini Uturuki Bw. Mustafa Albayram (hayupo
pichani).
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akiwa ameongozana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Prof.
Elizabeth Kiondo (wa pili kulia) mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kwa ajili ya
ziara ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo ameongozana na Mwekezaji kutoka nchini Uturuki Bw. Mustafa Albayram (hayupo pichani).
Baadhi ya viongozi wa
Mkoa wa Simiyu wakijadiliana jambo wakati wa ziara ya Mwekezaji kutoka nchini
Uturuki Bw. Mustafa Albayram (kulia) aliyefuatana na Balozi wa Tanzania nchini,
Prof. Elizabeth Kiondo, mkoani hapa Novemba 13, 2019 yenye lengo la kuangalia
mazingira ya uwekezaji katika viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(mwenye
shati jeupe katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini
Uturuki, Prof. Elizabeth Kiondo(wa saba kushoto) na Mwekezaji kutoka nchini
Uturuki Bw. Mustafa Albayram(wa sita kulia), viongozi mbalimbali wa mkoa wa
Simiyu na wadau wengine katika siku ya kwanza ya ziara mwekezaji huyo na Mhe.
Balozi mkoani Simiyu yenye lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika
viwanda.
0 comments:
Post a Comment