Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amezindua
rasmi utafiti unaohusu matumizi ya simu za
mikononi katika kuongeza ulipaji kodi za majengo nchini Tanzania, PIERI 20355
ambao utafanyika kuanzia Novemba 28, 2019 hadi 30 Juni 2020 katika Halmashauri
ya Mji wa Bariadi na Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
Akizindua utafiti huo Novemba 28, 2019 mjini Bariadi Sagini amewataka
Wakurugenzi wa Halmashauri hizo kutoa ushirikiano unaotakiwa kwa watafiti ili kuwawezesha
kufanya kazi yao kwa ufanisi na kupata matokeo sahihi.
“ Wakurugenzi
katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Busega, hakikisheni mnatoa ushirikiano
katika utafiti kwani majengo yanayolipiwa kodi ya majengo yapo kwenye maeneo
yenu na wamiliki wa majengo hayo pia wapo katika maeneo yenu,” alisema Sagini.
Sagini
amewaahidi watafiti ushirikiano mkubwa ili utafiti ufanyike kama ilivyokusudiwa kwa lengo la kuongeza mapato yatokanayo na
kodi ya majengo huku akiwaomba watafiti hao kuendeleza kushirikiano na mkoa wa Simiyu katika tafiti
mbalimbali kwa maendeleo ya Mkoa, wananchi na Taifa kwa ujumla.
Akiwasilisha taarifa ya utambulisho wa utafiti huo Mhadhiri
Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe na Mtafiti Mwandamizi wa Utafiti huu, Dkt.Francis
Mwaijande, amesema Matokeo ya utafiti huu yatawezesha mamlaka za maamuzi
ziweze kutoa maamuzi kwa kuzingatia taarifa zilizifanyiwa utafiti na hivyo kuwa
na maamuzi ya kuongeza ufanisi kwenye ukusanyaji kodi.
Ameongeza kuwa matokeo ya utafiti huu
yanatarajiwa kuongeza mapato yatokanayo na kodi za majengo kwa Serikali kwa
kuhamasisha ulipaji kodi kwa kutumia simu zao za mkononi kwa njia ya meseji.
Utafiti unaohusu matumizi ya simu za
mikononi katika kuongeza ulipaji kodi za majengo nchini Tanzania, PIERI 20355
unafanyika kwa lengo la kutafuta
Ushahidi wa kitaaluma ili kuainisha kipi kinaweza kuongeza ulipaji kodi kwa
kufuata sheria.
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na watafiti
wanaofanya utafiti kuhusu unaohusu matumizi ya simu za mikononi katika kuongeza
ulipaji kodi za majengo nchini Tanzania, PIERI 20355 katika mikoa ya Simiyu na
Shinyanga wakati wa utambulisho wa utafiti mjini Bariadi Novemba 28, 2019Watafiti wanaofanya utafiti kuhusu unaohusu matumizi ya simu za mikononi katika kuongeza ulipaji kodi za majengo nchini Tanzania, PIERI 20355 katika Mikoa ya Simiyu na Shinyanga, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini wakati akizungumza nao katika utambulisho wa utafiti mjini Bariadi Novemba 28, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na
watafiti wanaofanya utafiti kuhusu unaohusu matumizi ya simu za mikononi katika kuongeza ulipaji
kodi za majengo nchini Tanzania, PIERI 20355 wakati wa utambulisho wa utafiti mjini
Bariadi Novemba 28, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini(katikati mbele) akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wanaofanya utafiti kuhusu matumizi ya simu za mikononi katika kuongeza ulipaji kodi za majengo nchini Tanzania, PIERI 20355 wakati wa utambulisho wa utafiti mjini Bariadi Novemba 28, 2019.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe na Mtafiti Mwandamizi wa Utafiti huu, Dkt.Francis Mwaijande akiwasilisha taarifa kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini wakati wa utambulisho wa utafiti huo mjini Bariadi Novemba 28, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na
watafiti wanaofanya utafiti kuhusu unaohusu matumizi ya simu za mikononi katika kuongeza ulipaji
kodi za majengo nchini Tanzania, PIERI 20355 katika mikoa ya Simiyu na
Shinyanga wakati wa utambulisho wa utafiti mjini Bariadi Novemba 28, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini akiagana na mmoja wa
watafiti wanaofanya utafiti kuhusu matumizi ya simu za mikononi katika kuongeza
ulipaji kodi za majengo nchini Tanzania, PIERI 20355 katika mikoa ya Simiyu na
Shinyanga, mara baada ya utambulisho wa utafiti huo mjini Bariadi Novemba 28, 2019.
0 comments:
Post a Comment