Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange
ametoa wito kwa wananchi mkoani Simiyu kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi na
kuacha ulaji usiofaa kwa kuacha kutumia vyakula vyenye sukari, mafuta na chumvi
nyingi na nafaka zilizokobolewa kwa lengo la kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo
kisukari, shinikizo la juu la damu na saratani.
Dkt Dugange ameyasema hayo Novemba 22, 2019 wakati
wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza, ambayo
ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji
wa Bariadi.
“ Asilimia 43 ya wagonjwa wanaotibiwa katika vituo
vya kutolea huduma za afya wana matatizo yanayotokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kutofanya
mazoezi kunachangia kwa asilimia 60 magonjwa yasiyoambukiza, hivyo ni vema
wananchi wakafanya mazoezi na kuepuka ulaji usiofaa ili kudhibiti magonjwa
haya,” alisema Dkt. Dugange.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
amewataka watumishi wa idara ya afya mkoani hapa, kuwafikishia wananchi elimu
ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza na kutoa ushauri kwa mtu mmoja mmoja
kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi, lishe bora na madhara ya kutumia vilevi
kupita kiasi.
Aidha, Sagini amesisitiza wataalam wa afya
kuelimisha jamii namna ya kutambua magonjwa yasiyoambukiza kupitia upimaji na kufuatilia
watu wenye magonjwa sugu yasiyoambukiza.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
amesema atashirikiana na viongozi wengine kusimamia ufanyaji wa mazoezi ya
viungo ikiwemo utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi Jumamosi ya pili ya kila
mwezi ili kuwahamasisha wananchi kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza.
“Tutakachokifanya sasa hivi ni kugawa vituo vya
mazoezi ya mara kwa mara kulingana na kanda kwa kuwa mji unakuwa, lakini pia tutaweka
viongozi kwa kila kanda, ili kila inapofika Jumamosi ya pili mwezi viongozi
wanakuja na watu wao tunajumuika pamoja katika mazoezi,”alisema Kiswaga.
Kwa upande wao watumishi walioshiriki katika mazoezi
hayo wamewashukuru viongozi wa Mkoa kwa kuhamasisha watumishi na wananchi
kushiriki mazoezi haya, kwa sababu wanatumia muda mwingi kazini wakiwa wamekaa
hali inayoweza kuchangia wao kupata magonjwa yasiyoambukiza, hivyo wakaomba
utaratibu huo uwe endelevu na waahihidi kushiriki kila wakati ili kujikinga na
magonjwa yasiyoambukiza.
“Watumishi wengi tumekuwa tukijihusisha zaidi na shughuli zetu za kikazi tunasahau na
wakati mwingine tunashindwa kufanya
mazoezi ambayo ni muhimu kwa afya zetu na ufanisi wa kazi zetu, ninashukuru
viongozi wetu kuandaa na kufanikisha zoezi hili na sisi kama watumishi
tunaahidi kuwa suala hili litakuwa endelevu,” alisema Marko Igenge mtumishi
idara ya afya.
Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa ilizinduliwa
rasmi kimkoa Novemba 22, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi na
utaratibu wa kufanya mazoezi ya viungo utaendelea kufanyika kila Jumamosi ya
pili katika kila mwezi.
MWISHO
Baadhi ya viongozi, watumishi wa umma na taasisi binafsi na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Baadhi
ya viongozi, watumishi wa umma na taasisi binafsi na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika
uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22,
2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

ya viongozi, watumishi wa umma na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika
uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22,
2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Baadhi
ya viongozi, watumishi wa umma na taasisi binafsi na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika
uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22,
2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Baadhi
ya viongozi, watumishi wa umma na taasisi binafsi na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika
uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22,
2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
.
Wachezaji
wa timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu(wenye jezi za zambarau) na timu ya
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa(wenye jezi nyeupe) wakicheza mechi ya kirafiki
wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa
yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi
kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi wa umma
na wananchi, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22,
2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na watumishi wa umma na
wananchi, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa
yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi
kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(mwenye fulana ya mistari) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa
timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu kabla ya mechi ya kirafiki iliyochezwa
kati ya timu hiyo na timu ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, wakati wa uzinduzi wa
Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22,
2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(mwenye fulana ya mistari) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu
ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kabla ya mechi ya kirafiki iliyochezwa kati ya
timu hiyo na timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakati wa uzinduzi wa
Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22,
2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Wachezaji
wa timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu(wenye jezi za zambarau) na timu ya
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa(wenye jezi nyeupe) wakicheza mechi ya kirafiki
wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa
yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi
kimkoa Novemba 22, 2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Baadhi
ya viongozi, watumishi wa umma na taasisi binafsi na wananchi wakifanya mazoezi ya viungo katika
uzinduzi wa Kampeni ya kudhibiti na kuzuia magonjwa yasiyoambukiza ambayo ilizinduliwa rasmi kimkoa Novemba 22,
2019.katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
0 comments:
Post a Comment