Thursday, December 10, 2020

KILA MDAU AWE SEHEMU KUUFIKISHA MKOA NAMBA MOJA MITIHANI YOTE KITAIFA: RAS SIMIYU

Katibu Tawala wa Mkoawa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga ametoa wito kwa viongozi, walimu, wazazi na wadau wote wa elimu mkoani hapa kushiriki kikamilifu katika kutekeleza na kuwezesha azma ya mkoa ya kuwa nafasi ya kwanza katika mitihani yote ya  Taifa.

Mmbaga ameyasema hayo Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi wakati akifungua kikao cha viongozi, watendaji na wadau wa elimu mkoa cha kutangaza Mkakati wa Mkoa wa kuboresha taaluma kwa mwaka 2021 ambapo alibainisha kuwa endapo kila mdau atatimiza wajibu wake Simiyu itakuwa mkoa bora katika elimu.

“Mkoa wetu kushika nafasi ya kwanza inawezekana kabisa, kama tuliweza kutoka nafasi za mwishoni kabisha tukaingia, kumi bora, sasa hivi tuka katika tatu bora, naamini kwa uweza wa Mwenyezi Mungu tunaweza  kushika nafasi ya kwanza katika mitihani yote ya Taifa,” alisema Mmbaga.

Aidha, Mmbaga amewataka viongozi wa idara ya elimu kuepuka kutumia kauli chafu kwa walimu kwa kuwa zinawakatisha tamaa na kupunguza tija na ari katika utendaji kazi wao badal yake watumie mbinu sahihi za kiuongozi kutatua changamoto wanazoziona kwa walimu.

 Naye Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema ushirikiano, mawasiliano na mahusiano mazuri baina ya walimu, viongozi na wadau wote wa elimu yanasaidia muda mwingi kutumika kufundisha na kusimamiana badala ya kutumika kuzozana, kugoma na kusuluhishana.

Baadhi ya walimu na Maafisa Elimu wa Kata na Halmashauti wamesema wameupokea mkakati huo na kuahidi kutimiza wajjibu wao ili kuweza kufikia malengo ya mkoa na kuboresha taaluma na elimu mkoani Simiyu huku wakitoa maoni mbalimbali namna ya kuboresha zaidi utekeelzaji wa mkakati huo.

“Nashauri mkoa uanzishe mitihani ya pamoja ya madarasa tarajiwa yaani darasa la tatu, darasa la sita, kidato cha kwanza na kidato cha tatu, mitihani hii itusaidia kujua shule zipi zina changamoto gani na itasaidia kuweka mikakati ya kuziwezesha kufanya vizuri kwa kuwa walimu na viongozi wengine watakuwa na mwaka mzima wa kuyaandaa madarasa hayo kabla ya mtihani wa Taifa,” alisema Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Lagangabilili Itilima, Mwede Hongoa.

“Tunaomba Serikali iboreshe makazi ya walimu, walimu wengi hawana nyumba za kuishi maeneo ya shule wengi wanatoka mbali na Shule hivyo wakati tunapohitaji kuwasaidia wanafunzi hasa nyakati za usiku inakuwa vigumu kwao kushiriki kikamilifu,” alisema Mwalimu Flora Shimbi Mkuu wa Shule Itilima Sekondari.

“Serikali ya Mkoa imetoa motisha kwa walimu hasa wanaofanya vizuri na walimu wa mkoa wa Simiyu wamehamasika sana na wanajituma katika kazi yao, tunaomba serikali iendelee kuboresha miundombinu ikiwemo vyumba vya madarasa, madawati na viti ili mazingira yao ya kufundishia yawe bora zaidi,” alisema Mwalimu Oscar Nsolo Mkuu wa Shule Sapiwi Sekondari.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ameshauri mkoa wa Simiyu kuwa na mfuko wa elimu wa mkoa, ili mfuko huo uweze kusaidia katika ujenzi wa miundombinu ya elimu huku akitoa wito kwa wazazi na wadau wote wa elimu kuona umuhimu wa kuuchangia mfuko huo.

Mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021 umejumuisha mambo muhimu ikiwa ni pamoja na Uwezo wa kujituma kwa viongozi wa elimu, uungwaji mkono na viongozi wa juu,uwajibikaji wa maafisa elimukata na mfumo wa utawala, huduma bora na mawasiliano kwa walimu/wadau wa elimu, utoaji wa motisha na zawadi, ufatiliaji kabambe wa ufundishaji na ujifunzaji, mafunzo kazini,upimaji, miundombinu na samani, kambi za kitaaluma, matumizi ya mitandao ya TEHAMA.

MWISHO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi kikiwashirikisha walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani hapa.

Baadhi ya Walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani Simiyu, katika kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani Simiyu, katika kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi.

Mmoja wa walimu akichangia hoja katika kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi.

Mmoja wa walimu akichangia hoja katika kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania Mkoa wa Simiyu, akichangia hoja katika kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi.

Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka , Katibu Tawala wa Mkoa, Bibi. Miriam Mmbaga na Afisa Elimu wa Mkoa, Mwl. Ernest Hinju wakiteta jambo katika kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi

Baadhi ya Walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi

Baadhi ya Walimu, viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa elimu na wadau elimu mkoani mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akifungua kikao cha kutangaza mkakati wa kuboresha taaluma mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2021, kilichofanyika Desemba 09, 2020 Mjini Bariadi

Monday, December 7, 2020

HALMASHAURI ZATAKIWA KUKAMILISHA UTOAJI WA VITAMBULISHO KWA WAZEE KUFIKIA JUNI 2021

Rai imetolewa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha kuwa wanakamilisha zoezi la utoaji wa vitambulisho vya matibabu kwa wazee kufikia mwezi Juni 2021, ili wazee waweze kupata huduma za matibabu katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya kama Serikali ilivyodhamiria.

Rai hiyo imetolewa Novemba 4, 2020 Mjini Bariadi na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika uzinduzi wa Baraza la Ushauri la Wazee Mkoa wa Simiyu..

“Mkoa kupitia Halmashauri umefanya utambuzi wa jumla ya wazee 68,175 kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanapatiwa huduma muhimu, hadi sasa  jumla ya mabaraza 770  ya wazee yameundwa katika ngazi zote ; kuhusu upatikanaji wa vitambulisho vya matibabu bure, jumla ya wazee 18, 911 wamepatiwa vitambulisho hivyo ndani ya mkoa sawa na asilimia 28,’ alisema Kiswaga.

Mabaraza si ya kiitikadi hivyo kila mtu mwenye umri wa miaka sitini na kuendelea ana haki ya kujiunga na kuwa mjumbe wa Baraza la Wazee mahali alipo, huku akiahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Wazee na kukukutana na wazee mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa inawasilikiza na mahitaji yao muhimu yanapatikana.

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa, Bibi.Mwanahamisi Kawega amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itahakikisha inasimamia utekelezaji wa suala la ugawaji wa vitambulisho vya matibabu kwa wazee katika Halmashauri zote ili wazee wote waweze kuvipata kwa wakati.

Aidha Kawega ameongeza kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu itawaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri kuwaalika viongozi wa mabaraza ya wazee kualikwa katika mabaraza ya madiwani ili waweze kuwasilisha kero zao na kupatiwa ufumbuzi.

Naye Meneja Mradi kutoka Shirika la NABROHO SOCIETY FOR THE AGED linalojihusisha na utetezi wa haki za wazee  , Bw. Kubini Nkondo ameipongeza Serikali kwa namna inavyotoa kipaumbele kwa wazee na namna ilivyokomesha mauaji ya wazee.

"Wazee wamepitia changamoto nyingi ukizungumzia  hata suala la mauaji ya wazee, takwimu awali zilikuwa juu sana lakini katika utawala huu tunazungumzia mauaji hayo kupungua mpaka kufikia 'digit' (tarakimu) moja, Mkoa wa Simiyu ambao ulikuwa ukitajwa katika Mkoa 10 inayoongoza kwa mauaji ya wazee sasa hivi haitajwi hata tena katika mikoa inayoongoza kwa mauaji hayo," alisema Nkondo.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Mkoa wa Simiyu, Bw. Lameck Sendo amesema Baraza hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika kushughulikia haki mbalimbali za wazee huku akiomba Serikali kuitungia sheria  Sera ya wazee ya mwaka 2003 ili iweze kutumika katika kuwaongoza pamoja na miongozo iliyopo.

Afisa Ustawi wa Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bw. Daniel Mapunda amesema Mkoa wa Simiyu una takribani wazee 68,175, hivyo kwa mujibu wa Sera ya Wazee ya mwaka 2003 Baraza la Wazee la Mkoa litakuwa ni chombo maalum cha kuwasemea wazee na kushiriki katika maeneo  mbalimbali ya kimaamuzi.

MWISHO

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa pili kushoto) akimkabidhi nyaraka mbalimbali Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Mkoa wa Simiyu, Bw. Lameck Sendo mara baada ya kuzindua baraza hilo Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Baadhi ya viongozi wa Mabaraza ya Ushauri ya Wilaya za Mkoa wa Simiyu wakifurahia jambo katika kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa na kuzindua baraza hilo.

Baadhi ya viongozi wa Mabaraza ya Ushauri ya Wilaya za Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa na kuzindua baraza hilo.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Mkoa wa Simiyu, Bw. Lameck Sendo akieleza namna Baraza hilo litakavyofanya kazi mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kuzindua baraza hilo  Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Daniel Mapunda akitoa ufafanuzi juu ya taratibu zinazopaswa kufuatwa katika Uchaguzi wa Viongozi wa Baraza la Ushauri la Mkoa, katika kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza hilo na kuzindua.

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Mwanahamisi Kawega akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali katika kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa na kuzindua baraza hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongzi wa Mkoa wa Simiyu, viongozi wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa(waliosimama) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Bw. Lameck Sendo(wa pili kulia walioketi), baada ya kuzindua baraza hilo Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Meneja Mradi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na utetezi wa Haki za Wazee mkoani Simiyu, Bw. Kubini Nkondo Kubin akizungumza na viongozi wa mabaraza  ya Ushauri ya Wilaya  katika kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa na kuzindua baraza hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, viongozi wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa, Viongozi wa mabaraza ya wilaya (waliosimama) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mkoa, Bw. Lameck Sendo(wa pili kulia walioketi), baada ya kuzindua baraza hilo Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Mkoa wa Simiyu, Bw. Lameck Sendo akitoa maelezo ya agenda kumi zinazowahusu wazee katika kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza hilo na kuzindua kazi iliyofanywa na  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kuzindua baraza hilo, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Maafisa Ustawi wa Jamii na kiongozi wa dini (waliosimama) na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa, Bw. Lameck Sendo(wa pili kulia walioketi), baada ya kuzindua baraza hilo Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa  wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa Baadhi ya viongozi wa Mabaraza ya Ushauri ya Wilaya za Mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza la Ushauri la Mkoa na kuzinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Baadhi ya viongozi wa Mabaraza ya Ushauri ya Wilaya za Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza la Usahauri la Wazee la Mkoa na kuzindua baraza hilo.

Mwenyekiti wa Baraza la ushauri la Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, akipokea nyaraka za utendaji kazi wa baraza hilo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga baada ya kuzinduliwa kwa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa, Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Maafisa Usatawi wa Jamii na kiongozi wa dini (waliosimama) na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa, Bw. Lameck Sendo(wa pili kulia walioketi), baada ya kuzindua baraza hilo Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Baadhi ya Viongozi wa Baraza la Ushauri la Mkoa wa Simiyu

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Mwanahamisi Kawega, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Daniel Mapunda na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa  wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba wakiteta jambo kikao kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kufanya uchaguzi wa Baraza la Ushauri la Wazee la Mkoa na kuzindua baraza hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na baadhi ya viongozi wa mabaraza ya ushauri ya wilaya za mkoa wa Simiyu kabla ya kuzindua Baraza la ushauri la Mkoa kilichofanyika Desemba 04, 2020 Mjini Bariadi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

Saturday, December 5, 2020

ASKOFU LEKUNDAYO AONGOZA MAOMBI KUMSHUKURU MUNGU KULIVUSHA TAIFA KATIKA JANGA LA CORONA, UCHAGUZI MKUU

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo ameongoza viongozi na mamia ya waumini wa kanisa hilo katika ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi la Mtaa wa Ntuzu lililopo Bariadi mjini ambapo  Waumini wa kanisa hilo pamoja na wengine kutoka mkoa wa Mwanza na Mara wamewakilisha waumini wengine hapa nchini, ambapo ibada hiyo imehudhuriwa pia na viogozi wa Chama na Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.

“Nilikuwa naangalia takwimu za hali ya janga la Corona ilivyo duniani leo asubuhi (Desemba 05, 2020) hadi sasa zinaonesha watu 66,281,000 wamepatwa na Corona, waliokufa mpaka sasa 1,525,294 ikiwa ulikuwa umechukulia kiurahisi, hizi takwimu zikuamshe kwamba Mungu ametupendelea sana Tanzania tunamshukuru sana Mungu kwa niaba ya wenzetu,” alisema Dkt. Lekundayo.

Awali akitoa mahubiri kabla ya maombi hayo pamoja na kuwasihi waumini kumshukuru Mungu kuwapitisha katika janga la Corona, Askofu Lekundayo pia ametoa wito kwa waumini kuendelea kumshukuru Mungu pia kwa namna ambavyo amelipitisha Taifa katika Uchaguzi Mkuu, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya jambo ambalo litabaki kumbukumbu yao juu ya neema ya Mungu katika masuala hayo.

Akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema Tanzania kupitishwa katika Janga la Corona haikuwa bahati bali ni neema ya Mungu, hivyo akawashukuru viongozi wa Dini kwa kuliombea Taifa kwa juhudi na Mungu akajibu.

Aidha, Kiswaga amesema Serikali inaendelea kuheshimu mchango wa kanisa na itaendelea kushirikiana nalo katika majukumu yake ya kitume na kimaendeleo, huku akitoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa na viongozi wake ili waweze kufanya kazi kwa manufaa na ustawi wa Watanzania.

“Katika neno la Mungu kuna habari ya wale wakoma kumi ambao waliponywa na Bwana Yesu lakini aliyerudi kushukuru ni mmoja tu, ninaamini maombi haya ya shukrani yaendelea kuiponya nchi yetu na majanga ambayo yanaonekana kwa macho na ambayo hayaonekani,” alisema Kiswaga.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Mhe. Samweli Kiboye  amesema kuna baadhi ya watu waliobeza Mhe Rais alivyotangaza  kumtanguliza Mungu kwa kutangaza siku tatu za kuliombea Taifa ili aliponye Taifa  na Janga la Corona lakini baada ya kuona matokeo ya maombi naamini wameona kuwa maamuzi yake yalikuwa sahihi.

MWISHO

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo akihubiri  katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani  hapa nchini iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo, viongozi wa Serikali na viongozi wa Chama, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji.David Makoye akiongoza maombi katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(kushoto), iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Kwaya kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi ikiimba katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Kwaya kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato Sabasaba Musoma mkoani Mara ikiimba katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji.David Makoye, katika  ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Kutoka kushoto Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt. Mch. Godwin Lekundayo, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji.David Makoye wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Baadhi ya Waumini wa Kanisa la Waadventisa Wasabato wakichangia ujenzi wa Kibweta kama alama ya shukrani kwa Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt. Mch. Godwin Lekundayo,, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Mhe. Samweli Kiboye akitoa salamu katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Mhe. Juliana Mahongo katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika salama hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazin kwa amani i mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakishiriki maombi katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo akihubiri  katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani  hapa nchini iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za Serikali kwa niaba ya  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini iliyongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo akivishwa skafu na vijana watengeneza njia katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo, viongozi wa Serikali na viongozi wa Chama, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini, iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Dkt.Mch. Godwin Lekundayo(Kulia) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa waSimiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika Janga la Corona pamoja na kusaidia Uchaguzi Mkuu kumalizika kwa amani hapa nchini iliyongozwa na Askofu huyo, iliyofanyika Desemba 05, 2020 katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi kwa niaba ya Waumini wa kanisa hilo hapa nchini.

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!