Na Stella Kalinga
Mhandisi wa Ujenzi wa Sekretarieti ya
Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Mshuga amesimamishwa kazi kwa kukabiliwa na mashtaka
matatu.
Akizungumza na watumishi wa Sekretarieti
ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amesema Mhandisi
huyo anashtakiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu aliyopewa kwa kiwango cha
kuridhisha.
Amesema akiwa mtumishi wa umma kinyume
na kipengele cha 8 cha sehemu"A" ya jedwali la kwanza la kanuni za
Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003; mtumishi huyo alishindwa kuandaa
makadirio ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa yenye uhalisia.
Aidha , Aliandaa makadirio ya Tsh46,106,456,000
yaliyosomwa mbele ya Mhe. Rais tarehe 11 Januari,2017 ambayo ni ya juu kuliko
uhalisia.
Shtaka la pili linalomkabili ni kufanya uzembe mkubwa wakati wa utekelezaji
wa majukumu ya kazi iliyopewa kinyume na kipengele cha 13 cha sehemu
"A" ya jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma,Tangazo la
Serikali na 168/2003;
Alitaja (1) kuandaa makadirio ya ujenzi
wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa Tshs.46,106,456,000 hali iliyosababisha Mhe Rais
kusomewa taarifa ya gharama zisizo na uhalisia na(2) Kuandaa michoro ya taswira
(3 D)isiyoendana na michoro halisi ya Hospitali ya Mkoa iliyooneshwa mbele ya
Mhe.Rais
Shtaka la tatu ni kufanya kazi kwa
kukiuka maadili ya taaluma yake wakati wa utekelezaji ya kazi aliyopewa kinyume
na kipengele cha 14 cha Sehemu "A" ya Jedwali la kwanza la Kanuni za
Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003:- kwa (1) Kuandaa makadirio
ya shilingi 46,106,456,000 ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
bila kuzingatia mita za mraba za eneo, michoro na kusababisha gharama kubwa
zisizo na uhalisia
(2) Kuandaa makadirio ya shilingi
3,009,640,000 yasiyo na uhalisia ili kugharamia ujenzi wa majengo ya msingi
kuwezesha Hospitali kuwa "functional" kwa kupiga simu Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Singida.
Katibu Tawala wa Mkoa, Ndg..Jumanne
Sagini ametoa wito kwa watumishi wa
Umma mkoani humo kutekeleza majukumu waliyopewa kwa bidii, weledi na
uadilifu ili kuepuka makosa ambayo husababisha watumishi kuchukuliwa hatua za
kinidhamu.
“Nikiwa kama mwajiri nimesikitishwa na
kufadhaishwa na wataalam walioajiriwa ngazi ya mkoa kuishauri Sekretarieti ya
Mkoa na kuzisimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuzishauri kitaalam, kutenda
matendo yanayodhihirisha upungufu wa weledi,
kushindwa kutekeleza majukumu na uzembe
mkubwa” alisema.
Naye Mkuu wa Mkoa huo,Mhe.
Anthony Mtaka amesema gharama zilizowasilishwa awali na wataalam hazikuwa na
mchanganuo toshelevu na makisio hayakuwa na uhalisia, hivyo amemwomba radhi Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, kwa taarifa za upotoshaji zilizotolewa na
wataalam wakati wa ziara yake Mkoani humo.
“....kuna vitu vingine
vilivyopachikwa kwenye ramani, wenye taaluma yao walipokutana ili kujustify
hiyo bilioni 46.1 walishindwa kujustify kwenye ramani, kwa hiyo hatukuwa na
uhalisia; baada ya mapitio ya kazi zote ilionekana
Hospitali ya Mkoa wa Simiyu inaweza kujengwa kwa gharama ya bilioni 11.4 mule mule alimosema Rais” alisema Mtaka.
Makadirio ya awali ya
Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa yalikuwa ni shilingi bilioni 46.1 na gharama hii
haikukubaliwa na Mhe.Rais na badala yake akaagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama
ya Mkoa kutembelea TBA Makao Makuu, ili kujifunza na kuona jinsi walivyoweza
kujenga majengo ya hosteli ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa gharama ndogo ya shilingi bilioni 10 na
akaahidi kutoa bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo.
![]() |
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa huo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya awali ya uchunguzi wa gharama za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa |
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa huo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya awali ya uchunguzi gharama za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa |
ReplyDeleteHello.
Mimi ni Mr Rahel binafsi wakopeshaji mkopo ambao hutoa maisha wakati nafasi ya mkopo kwa watu binafsi, makampuni ya biashara, bima, nk Je, katika shida yoyote ya kifedha au katika haja ya mkopo wa kuwekeza au unahitaji mkopo kulipa bili yako kutafuta hakuna zaidi kama sisi ni hapa kufanya matatizo yako yote ya kifedha kitu cha zamani. Sisi kutoa kila aina ya mkopo katika dhehebu lolote fedha kwa kiwango cha 2% bila fee.I upfront wanataka kutumia kati hii kubwa ya kukufahamisha kwamba tuko tayari kukusaidia kwa aina yoyote ya mkopo kutatua kwamba tatizo.Kama yako ya kifedha ndiyo basi kupata nyuma sasa kupitia barua pepe (rahelcohranloan@gmail.com) kwa maelezo zaidi, wewe ni sana makala.