Na Stella Kalinga
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini ametoa wito kwa viongozi na
Wakuu wa Taasisi za Umma mkoani humo, kusimamia utekelezaji wa agizo la Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan la kufanya
mazoezi ya viungo Jumamosi ya pili ya kila mwezi.
Sagini ametoa wito huo leo katika hotuba yake kwa watumishi wa
umma,wanafunzi na wananchi walioshiriki mazoezi ya viungo na michezo mbalimbali
katika uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la
Mhe.Makamu wa Rais.
"...Niombe wote wanaowasimamia Watumishi wa Umma kuhimiza utaratibu
huu wa mazoezi ambao ni agizo la Makamu wa Rais ambalo limeongozana na nyaraka za
Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara yenye dhamana na Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
lakini mara kadhaa hata Wizara ya Afya imekuwa ikisema, Sisi kama
Watumishi wa Umma hatuwezi kuchagua kutekeleza au tusitekeleze" alisema.
Amesema kila mkuu wa Taasisi,Idara,Sehemu anapaswa kuhakikisha watumishi
walio chini yake wanashiriki mazoezi ya viungo mwezi ujao(Machi) kwa kuwa
kushindwa kutekeleza Maelekezo ya viongozi pasipo sababu za msingi ni
utovu wa nidhamu, ambalo ni kosa kwa mujibu wa Sheria,kanuni na taratibu za
Utumishi wa Umma.
Sagini ameongeza kuwa watumishi ambao hawatashiriki mazoezi ya viungo
pasipo sababu za msingi wahojiwe na ikibidi wachukuliwe hatua stahiki kutokana
na utoro huo.
Aidha, ametoa rai kuwa watumishi wa umma kujenga utamaduni wa kufanya
mazoezi mara kwa mara ili kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza kama
shinikizo la damu, kisukari na magonjwa ya moyo kwa kuwa muda mwingi wanakuwa
maofisini.
Wakati huo huo Afisa Michezo wa Mkoa wa Simiyu,Ndg.Addo Komba amesema
pamoja na kutekeleza agizo la Mhe.Makamu wa Rais, Mkoa una mpango wa
kuwakutanisha watumishi wote wa Umma na Wanafunzi mara mbili kwa mwezi kufanya
mazoezi ya viungo na michezo mbalimbali.
Sambamba na hilo Komba amesema katika kutambua na kuinua vipaji kwenye
michezo, mkoa umepanga kuandaa ligi mwishoni mwa mwezi Februari, 2017 kwa ajili
ya wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kwa michezo mitatu ambayo ni mpira
wa miguu, mpira wa pete na Riadha.
Utekelezaji wa Agizo la Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan mkoani
Simiyu, unafanyika chini ya kauli mbiu"SIMIYU MPYA, MICHEZO KWA AFYA,
AMANI NA MAENDELEO."
Hello.
ReplyDeleteMimi ni Mr Rahel binafsi wakopeshaji mkopo ambao hutoa maisha wakati nafasi ya mkopo kwa watu binafsi, makampuni ya biashara, bima, nk Je, katika shida yoyote ya kifedha au katika haja ya mkopo wa kuwekeza au unahitaji mkopo kulipa bili yako kutafuta hakuna zaidi kama sisi ni hapa kufanya matatizo yako yote ya kifedha kitu cha zamani. Sisi kutoa kila aina ya mkopo katika dhehebu lolote fedha kwa kiwango cha 2% bila fee.I upfront wanataka kutumia kati hii kubwa ya kukufahamisha kwamba tuko tayari kukusaidia kwa aina yoyote ya mkopo kutatua kwamba tatizo.Kama yako ya kifedha ndiyo basi kupata nyuma sasa kupitia barua pepe (rahelcohranloan@gmail.com) kwa maelezo zaidi, wewe ni sana makala.