Waziri wa Katiba
na Sheria Mhe.Prof. Palamagamba Kabudi amewataka wasajili wa vyeti vya kuzaliwa
kupitia mpango wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa
chini ya miaka mitano kwenye mikoa ya
Simiyu na Mara, kufanya kazi hiyo kwa umakini na uzalendo mkubwa katika kuhakikisha
wanawasajili watoto wenye sifa.
Waziri Kabudi
ametoa rai hiyo Machi 20 wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto
wenye umri wa chini ya miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa, katika mikoa
ya Simiyu na Mara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya
Musoma mkoani Mara.
“Mikoa ya Mara na Simiyu ina muingiliano
mkubwa sana na wananchi wa nchi jirani hivyo wasajili wawe makini na
watangulize uzalendo wakati wa kutekeleza mpango huu, tusisajili mtoto ambaye hahusiki
na pale ambapo tuna mashaka kuwa mtoto huyo anaweza kuwa wa nchi za jirani,
tutoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika ili hatua za kiusalama zichukuliwe” alisema
Profesa Kabudi.
Amesema
kuwa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya
miaka mitano unafanyika bila malipo hivyo wasajili wasitumie kwa namna yoyote
mpango huo kama fursa ya kujipatia fedha kwa udanganyifu.
Aidha,
Waziri Kabudi ameahidi kutoa tuzo maalum kwa mkoa (kati ya Simiyu na Mara) utakaofikia
asilimia 80 ya lengo la usajili kwa
kipindi cha miezi miwili tangu usajili ulipoanza na wakati huo huo akawataka Viongozi wa
Taasisi zote Umma kuvitambua vyeti vitakavyotolewa chini ya mpango huo kwa kuwa
ni vyeti halali.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini hapa nchini (RITA) Profe. Hamis Dihenga amesema kupitia mpango wa
usajili na kutoa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, RITA inakusudia kusajili jumla ya watoto 735, 545
katika mikoa ya Simiyu na Mara kwenye vituo 463 (Mara) na Vituo 324 (Simiyu).
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mhe.Annarose Nyamubi akiwasilisha
taarifa ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe.Adam Malima amesema hadi
sasa Mkoa huo umesajili jumla ya watoto 78, 625 na watahakikisha watoto wote
wanaopaswa kusajiliwa wanasajiliwa ndani ya miezi miwili na baadaye kuendelea
na usajili kwa watoto watakaozaliwa.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga, akitoa salamu za Mkoa wa Simiyu
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka amesisitiza wananchi kutambua
umuhimu wa kuwasajili watoto wao ili waweze kutambulika, kupewa vyeti vya
kuzaliwa na Serikali iweze kupata takwimu sahihi.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia Watoto (UNICEF) hapa nchini ambao
ni miongoni mwa wafadhili wa mpango huu, Bi. Maud Droogleever , amesema Shirika hilo
litaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wote wenye umri wa
chini ya miaka mitano wanasajiliwa na
kupata vyeti vya kuzaliwa.
Baadhi
ya wananchi wa Mikoa ya Simiyu na Mara walioshirikia katika Uzinduzi wa Mpango
huo wameishukuru Serikali kwa kuleta mpango huo kwa kuwa umewarahisishia huduma
ya kupata vyeti vya kuzaliwa kwa kuwasogezea huduma hiyo katika Ofisi za kata
tofauti na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wanalazimika kufuata huduma hiyo
katika Ofisi za Wakuu wa Wilaya.
Waziri wa Katiba na
Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi(wa tatu kushoto) akizindua Mpango wa
Usajili wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa, kwa mikoa ya Simiyu na Mara katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya
Musoma mkoani Mara.
Waziri wa Katiba na
Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati) akionesha nakala ya cheti cha
kuzaliwa kinachotolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa
watoto wenye umri chini ya miaka mitano, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili na kutoa vyeti kuzaliwa kwa watoto wenye umri huo kwa mikoa ya Simiyu na Mara uliofanyika Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Waziri wa Katiba na
Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akipewa maelezo juu ya mfumo unaotumika kukusanyia taarifa za usajili kwa watoto wenye umri
chini ya miaka mitano chini ya mpango wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa
watoto hao, katika mikoa ya Simiyu na Mara ambao aliouzindua Machi 20, katika Manispaa
ya Musoma mkoani Mara
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akioneshwa cheti cha
kuzaliwa kilichotolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini hapa nchini
(RITA), mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa miaka
mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, uliofanyika Uwanja
wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimkabidhi mkazi wa
Manispaa ya Musoma cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake mwenye umri wa chini ya
miaka mitano, mara baada ya uzinduzi wa
Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri wa miaka mitano na kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya
Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini hapa nchini (RITA), Bi.
Emmy Hudson akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa
watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, uliofanyika Uwanja wa Shule ya msingi Mkendo Manispaa
ya Musoma mkoani Mara.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akitoa salama za Mkoa wa Simiyu kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa
watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa
mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja
wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya
Musoma mkoani Mara.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini hapa nchini (RITA) Prof.
Hamis Dihenga akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili
wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa
mikoa ya Simiyu na Mara katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya
Musoma mkoani Mara.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi(wa tatu kulia) akifurahia
burudani kutoka kwa kikundi cha ngoma ya asili kutoka Mkoani Mara, wakati wa
uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na
kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule ya
Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Wasanii
wa Kikundi cha Ngoma ya Asili cha Wagoyangi kutoka Maswa mkoani Simiyu wakitoa
burudani wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa
miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika
Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi(kushoto) akisalimiana na Mkuu
wa Wilaya ya Musoma, Mhe. Dkt.Vicent Naano mara baada ya kuwasili Mkoani Mara
kwa ajili ya kuzindua Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka
mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara,katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi(kushoto) akisalimiana na Mkuu
wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera mara baada ya kuwasili Mkoani Mara kwa ajili ya
kuzindua Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na
kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara katika Uwanja wa Shule ya
Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi(kushoto) akisalimiana na Mkuu
wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt.Joseph Chilongani mara baada ya kuwasili Mkoani
Mara kwa ajili ya kuzindua Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka
mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi(kushoto) akisalimiana na Mkuu
wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi mara baada ya kuwasili Mkoani Mara
kwa ajili ya kuzindua Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka
mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja
wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi(kushoto) akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Hatari Kapufi, mara baada ya kuwasili Mkoani Mara kwa ajili ya kuzindua Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo Manispaa ya Musoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati kwa walioketi)
akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mara,
Wilaya ya Musoma na baadhi ya viongozi wa RITA mara baada ya uzinduzi wa Mpango
wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano na kutoa vyeti vya
kuzaliwa kwa mikoa ya Simiyu na Mara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo
Manispaa ya Musoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (katikati kwa walioketi)
akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mikoa ya Simiyu na Mara, mashirika ya Kimataifa na Viongozi wa kitaifa mara baada
ya uzinduzi wa Mpango wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya wa miaka mitano
na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo
Manispaa ya Musoma.
0 comments:
Post a Comment