Saturday, September 22, 2018

RC SIMIYU AZINDUA TTCL RUDI NYUMBANI KUMENOGA MKOANI SIMIYU


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amezindua kampeni ya Shirika la Simu Tanzania (TTCL) Rudi Nyumbani Kumenoga mkoani humo na kuipongeza TCCL kwa kuboresha huduma zake na kuwa miongoni mwa mashirika ya Serikali yanayotoa gawio kwa Serikali, fedha ambazo zinasaidia kuboresha huduma za jamii na miundombinu.

Akizindua kampeni hiyo jana jioni Septemba 21, 2018 Mjini Bariadi, amesema kwa mara ya kwanza TTCL imetoa gawio kwa serikali fedha ambazo sehemu zimewezesha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ulioanza na Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD), ujenzi wa Barabara, miundombinu mingine pamoja na huduma mbalimbali kwa jamii.

Aidha, Mtaka ametoa wito kwa wananchi kutumia huduma za TTCL na kumuomba Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba kufungua ofisi mkoani Simiyu, kumleta meneja na kuongeza watumishi ili kuongeza wigo wa utoaji wa huduma.

Ameongeza kuwa  Mtendaji Mkuu wa TTCL aimarishe mfumo wa intaneti zaidi ili kuwezesha mpango wa mkoa wa Simiyu wa kufundisha kupitia teknolojia ambapo mtandao wa intaneti utahitajika kwa kiasi kikubwa.

“Tungehitaji tuone wanafunzi wa Simiyu wasome saa 24, wanafunzi wasio na walimu wa kutosha wa sayansi tutajenga vyumba vya madarasa vitakavyowezesha wao kusoma kupitia mfumo wa teknolojia, Mtendaji Mkuu wa TTCL imarisha mtandao wa TTCL wanafunzi wapate intaneti ili tuweze kurahisisha ufundishaji kwenye miji mikuu ya wilaya zetu” alisema.

Wakitoa maoni yao huduma za TTCL baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu wamesema walikuwa hawazitumii lakini baada ya shirika hilo kuboresha huduma zake hasa za mtandao wa intaneti wameanza kuzitumia na wakaomba ziendelee kuboreshwa zaidi.

“ Mimi nilikuwa sijawahi kutumia mtandao wa TTCL nilikuwa natumia mitandao mingine tu lakini nilivyoona matangazo nikasema ngoja nijaribu, nikaenda kununua laini na kuanza kutumia, napenda kutumia zaidi intaneti yao  iko vizuri” alisema Emmanuel Elias mkazi wa Bariadi

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba ametoa wito kwa Watanzania wote kurudi nyumbani na kuendelea kutumia huduma za TTCL kwa kuwa kadri wanavyotumia huduma hizo wanazalisha faida ambayo itaendelea kutumika hapa nchini kwa maendeleo ya nwananchi na Taifa kwa ujumla.

Aidha, kutokana na Taarifa ya kuwa na siku nne za maombolezo kwa Taifa ililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia ajali ya Kivuko cha MV Nyerere huko Ukerewe Mkoani Mwanza, Mkurugenzi Kindamba amesema TTCL haitaendelea na kampeni hiyo RUDI NYUMBANI KUMENOGA mpaka siku hizo zipite ili kuungana na Watanzania wengine kuomboleza juu ya msiba huu wa Taifa.

“Mhe. Rais ametangaza siku nne za maombolezo kuanzia tarehe 21 Septemba  hadi Septemba 24, 2018  kufuatia ajali ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere, tulikuwa tumepanga kuanza na Simiyu, twende Kahama halafu Tabora lakini kwa sababu ya msiba huu uliotugusa Watanzania wote na kwa kuwa  Shirika hili ni la Watanzania na sisi tumeguswa hivyo itabidi shughuli hii tuisitishe kwa muda; Mungu awarehemu wenzetu waliotangulia na majeruhi wapone haraka” alisema.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa huo pamoja na baaadhi ya Viongozi wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.
Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mtendajii Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba na Mkuu wa Wilaya ya itilima, Mhe. Benson Kilangiwakifurahia jambo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia)akimweleza jambo Mtendajii Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga mkoani Simiyu uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.
Mtendajii Mkuu wa TTCL Bw. Waziri Kindamba(aliyenyosha mkono) akitambulisha rasmi Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu. katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.



Baadhi ya wananchi wa Mji wa Bariadi mkoani Simiyu walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mji wa Bariadi mkoani humo walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizindua Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga ya TTCL Mjini Bariadi, jioni ya Septemba 21, 2018.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Aslay akitoa burudani kwa wananchi wa Mji wa Bariadi mkoani Simiyu walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.




Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Shilole akitoa burudani kwa wananchi wa Mji wa Bariadi mkoani Simiyu walioshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Rudi Nyumbani Kumenoga uliofanyika Mjini Bariadi jioni ya Septemba 21, 2018.

Thursday, September 20, 2018

WAZIRI KALEMANI AMUONDOA MENEJA WA TANESCO MEATU KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA USAMBAZAJI WA UMEME VIJIJINI


Waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani amemuondoa Meneja wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos  Mtae katika nafasi ya umeneja baada ya kushindwa kusimamia usambazaji wa umeme kupitia Mradi wa Umeme vijijini (REA) wilayani humo na amemwagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kumpangia kazi nyingine.

Waziri KALEMANI amechukua hatua hiyo katika mkutano wa hadhara mjini Meatu  akiwa katika ziara yake ya kukagua  kazi zinazofanywa na wakandarasi wa mradi wa Umeme vijijini REA awamu ya tatu Septemba 20, 2018, ambapo anaanzia katika uzinduzi wa mradi wa umeme  katika ofisi ya kijiji cha Dakama wilaya ya Meatu.

Dkt. Kalemani ameoneshwa kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi anayesambaza umeme wilayani Meatu ambaye ni kampuni ya White City, kutokana na kutokuonekana katika vituo na kutokuwa na vifaa vya kutosha na vituo vya kutosha.

“Kasi ya mkandarasi hapa ni mbovu niliteegemea nione wakandarasai wanachakarika maana kote nilikotoka nimekuta wanachakarika, pili nilitegemea nione yadi ya vifaa vya wakandarasi wetu”

“Huyu meneja ndiye msimamizi wa wakandarasi, namuuliza anasema hajui leo wakandarasi wako wapi sasa anasimamia nini? Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO pokea maelekezo, kuanzia sasa huyu Meneja wa TANESCO Wilaya mtoe, weka Meneja mwingine kuanzia kesho hapa, wananchi wanataka umeme hapa” alisema Dkt. Kalemani.

Katika hatua nyingine Dkt. Kalemani amewahakikishia wananchi wa vijiji 36 vya wilaya ya  MEATU kupata umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya tatu na akawasisitiza kuwa umeme utakapowafikia wautumie kwa ajili ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa wa Simiyu una asilimia sabini ya Mradi wa Umeme wa  REA ambapo wilaya ya Meatu  ilikuwa nyuma katika mradi huo ikilinganishwa na wilaya nyingine.

Aidha, amesema wananchi wa Meatu wakipata umeme utekelezaji wa Sera ya Viwanda utafanikiwa kwa kuwa wilaya hiyo ndiyo wilaya inayoongoza kwa kilimo cha pamba Tanzania na ndiyo wilaya inayoongoza kwa kilimo cha alizeti katika mkoa wa Simiyu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Salum  Khamis akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo hilo ameishukuru Serikali kwa kufanikisha utekelezaji wa usambazaji wa umeme katika vijiji vya wilaya hiyo na akaomba Wakandarasi waongeze kasi ili umeme awafikie wananchi kwa wakati

Naye mwakilishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Barnabas  Lupande ameahidi kuyafanyia kazi  maagizo ya  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani aliyoyatoa katika kuakikisha kazi kusambaza umeme kwa wananchi inafanyika inavyotakiwa.
MWISHO
Aliyekuwa Meneja wa Meneja wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos  Mtae (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kulia), wakati wa ziara yake wilayani humo Septemba 20, 2018.
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Umeme wa REA Awamu ya Tatu katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Baadhi ya iongozi wa Wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu wakishangilia mara baada ya Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Umeme wa REA Awamu ya Tatu katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ziara yake wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto)  akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Khamis wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu wakishangilia baada ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani kuwatangazia kuwa vijiji vyote katika wilaya yao vitapata umeme kupitia mradi waWakala wa Nishati  Vijijini (REA) Awamu ya tatu, baada ya uzinduzi wa zoezi hilo katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu, Septemba 20,2018


Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Salum Khamis(kushoto)  akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati , Mhe. Dkt. Merdad Kalemani wilayani Meatu yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA  awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwaonesha wananchi wa Kata ya Mwamishali kifaa cha Umeme kiitwacho UMETA , alipozungumza nao wakati wa ziarayake wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu, wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani wilayani Meatu yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA  awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu, wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani wilayani Meatu yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA  awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Mwamishali wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani(hayupo pichani) alipozungumza nao wakati wa ziara yake wilayani Meatu yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA  awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Mwamishali wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani(hayupo pichani) alipozungumza nao wakati wa ziara yake wilayani Meatu yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA  awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Simiyu kupitia CCM, Mhe. Leah Komanya  akizungumza kwa niaba ya wananchi katika Kata ya Mwamishali wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani wilayani Meatu yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA  awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu mkoani Simiyu, wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA  awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Salum Khamis   akizungumza kwa niaba ya wananchi katika Kata ya Mwamishali, wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani wilayani Meatu yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA  awamu ya tatu, Septemba 20,2018.


 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Meatu, Mhe. Juma Mwiburi akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu mkoani Simiyu, wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA  awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani(katikati mbele) na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu wakifurahia jambo wakati wa ziara ya Waziri huyo Septemba 20, 2018 wilayani Meatu.


SIMIYU YAZINDUA UPIMAJI WA MAENEO YA WAKULIMA, WAFUGAJI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA NDEGE NYUKI (DRONES)


Mkoa wa Simiyu umezindua Mpango wa kupima maeneo ya wafugaji na wakulima kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya ndege nyuki (drones) lengo likiwa ni kuwawezesha kuyatambua maeneo yao na kupewa hati miliki na baadaye kuyawekea miundombinu muhimu ya ufugaji na kilimo na kuondokana na migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Zoezi hilo limezinduliwa na  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka katika kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu na linatekelezwa Chini ya Serikali kwa Kushirikiana na Taasisi Ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

Amesema Mkoa huo ndiyo unaoongoza kwa kilimocha pamba nchini na ni miongoni mwa mikoa yenye ng’ombe wengi nchini, kwa kuwa wakulima na wafugaji wanamiliki ardhi ni vema maeneo yao yakapimwa wakapewa hati miliki na baadaye watalaam wa ardhi wawasaidie kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Ameongeza kuwa wafugaji wa mkoa wa Simiyu wamekuwa wakitozwa faini katika maeneo mbalimbali hivyo ili kuondokana na kadhia hiyo maeneo yao yakipimwa na wakaweka miundombinu muhimu kama vile mabwawa, visima, majosho na maeneo ya malisho wataondokana na uchungaji wa mifugo na kwenda kwenye ufugaji wenye tija

“Tungehitaji mpime mashamba yenu yakishapimwa mtapewa hati, watalaam wa halmashauri watawatengenezea mpango wa matumizi bora ya ardhi na kuwashauri namna sahihi ya uwekeaji wa miundombinu kama majosho, mabwawa, visima ili muwe wafugaji wenye tija ambao hamtapigwa faini wala kuibiwa ng’ombe” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mfumo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Bw. John Kajiba amesema upimaji kwa kutumia teknolojia ya ndege nyuki utafanyika  kwa urahisi  na haraka zaidi na ikilinganishwa na upimaji wa watu moja kwa kwa moja.

“Uzuri wa kutumia ndege nyuki ni kwamba tutatumia muda mfupi sana kupima eneo kubwa kwa wakati mmoja mfano,  eneo ambalo lngeweza kupimwa na watu wane kwa muda wa siku nne drone(ndege nyuki) inafanya kwa muda wa siku moja” alisema.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe. Pius Machungwa amesema upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji utawasaidia kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji na kupata hati ziatazowasaidia kuchukua mikopo kwenye taasisi za kifedha na kufanya shughuli za maendeleo kupitia maeneo yao
Nao wananchi wa Meatu wanasema wameupokea mpango huo kwa mikono miwili  kwa sababu watakuwa na uhakika wa umiliki wa maeneo yao baaada ya kupewa hati ambazo pia wamesema zitawasaidia kukopa mitaji ya kufuga na kulima kisasa na kwa tija.
“ Tumeupokea mradi huu kwa mikono miwili maana tutakapopimiwa maeneo yetu tutakuwa tunakopesheka kwenye taasisi za fedha, vile vile tutakuwa tumeondokana na migogoro kati ya wakulima na wafugaji kwa sababu maeneo yetu yatakuwa na mipaka iliyo wazi na kila mmoja atakuwa na hati ya kumili eneo lake” alisema John Mchagula mfugaji kutoka Kijiji cha Ng’hoboko
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akijiandaa kurusha angani ndege nyuki (drone) inayotumika kupima ardhi, katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani(katikati mbele) na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu wakifurahia jambo wakati wa ziara ya Waziri huyo Septemba 20, 2018 wilayani Meatu.
Mtaalam wa kutumia Ndege nyuki(drone) akiwaonesha viongozi na wananchi namna kifaa hcho cha kisasa kinavyorushwa angani na kwenda kukusanya taarifa zinazotakiwa, katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka/(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt. Joseph Chilongani, katika hafla ya  uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Meatu wakiiitazama ndege nyuki(drone) kifaa cha kisasa ambacho kitatumiwa kupima maeneo makubwa, katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu wakifauatilia burudani kutoka katika Kikundi cha BASEKI (hawapopichani), katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza  akiwasilisha taarifa ya zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji wilayani humo, katika uzinduzi wa zoezi hilo mkoani Simiyu, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya  Ng’hoboko, wakati wa   uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Baadhi ya wakulima na wafugaji wa Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, wakimsikiliza mkuu wa Mkoa huo wakati wa   uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani  akizungumza na wananchi wa Kata ya  Ng’hoboko wakati wa   uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo akielezea utendaji kazi wa Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa   uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018. 
 
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Simiyu, Lumen Mathias  akielezea utendaji kazi wa Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa   uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe   akiwasalimia wananchi wa Kata ya  Ng’hoboko, wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza,  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani  na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meatu, Mhe. Pius Machungwa,(anaonekana nyuma) wakifurahia jambo,  wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Mtaalam wa Ndege nyuki akiwaeleza wakulima na wafugaji na wananchi wengine juu ya namna kifaa hicho cha kisasa kinachotumika katika  zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji, ambalo limezinduliwa katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Viongozi wa  Wilaya ya Meatu wakiiitazama ndege nyuki(drone) kifaa cha kisasa ambacho kitatumiwa kupima maeneo makubwa, katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.

Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Viongozi wa  Wilaya ya Meatu wakiitazama ndege nyuki(drone) kifaa cha kisasa ambacho kitatumiwa kupima maeneo makubwa, katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza,  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani  na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meatu, Mhe. Pius Machungwa,(anaonekana nyuma) wakifurahia jambo,  wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018
Baadhi ya viongozi wa Vijiji na kata za Wilaya ya Meatu, wakitambulishwa wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani humo  Septemba 19, 2018.
Mtaalamu wa Ndege nyuki akitoa maelezo ya namna kifaa hicho kinavyofanya kazi kwa  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.
Mtaalam wa kutumia Ndege nyuki(drone) akiwaonesha viongozi na wananchi namna kifaa hcho cha kisasa kinavyorushwa angani na kwenda kukusanya taarifa, katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.

Kikundi cha Burudani kiitwacho BASEKI  kutoka Bariadi Mjini kikitoa burudani ya ngomba katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maeneo ya wakulima na wafugaji mkoani humo, ambalo limefanyika katika Kata ya Ng’hoboko wilayani Meatu,  Septemba 19, 2018.

WAZAZI WAASWA KUWALEA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA, KUWAEPUSHA NA DAWA ZAKULEVYA, MAAMBUKIZI YA VVU

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu  Mhe. Anthony Mavunde ametoa wito kwa  Wazazi nchini  kuwalea watoto wao  katika maadili mema ili kuwaepusha na  matumizi ya dawa za kulevya na Maambukizi ya   Virusi Vya Ukimwi.


Ushauri huo ameutoa  wakati akifungua makambi ya siku saba ya Kanisa la Waadventisa Wasabato mkoani SIMIYU, katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Mavunde amesema malezi ya watoto ni jambo muhimu sana hasa katika kizazi cha hivyo watoto wakikosa malezi bora katika umri walio nao ni rahisi kutumbukia katika makundi yasiyofaa yakiwemo ya matumizi ya dawa za kulevya na hivyo kukosa nguvu kazi ya Taifa.

“Kwa mujibu wa takwimu Tanzani kila siku watu 200 wanapat maambukizi mapya ya VVU katika watu 200 watu 80 ni vijana katika hao vijana 80 asilimia 80 ni watoto wa kike, hivyo tuendelee kuelemisha  na kuliandaa hili kundi kubwa la Vijana katika malezi bora ili wawe nguvu kazi ya kuleta tija katika Taifa letu” alisema.

Ameongeza kuwa ili watu waweze kuondokana na umaskini ni lazima wafanye kazi hivyo akatoa wito kwa Viongozi, waumini wa Kanisa la Waadventisa Wasabato na wananchi wote kufanya kazi kwa staha, uadilifu na malengo ili waweze kufanikiwa kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema makambi hayo ni sehemu ya Maandalizi ya Mkutano mkubwa wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadventista Wasabato (ATAPE) unatarajiwa kufanyika mwaka 2019 mkoani humo.

Aidha, Mtaka alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa mwaka 2019 kutakuwa na matukio makubwa matatu ambayo yataitambulisha Simiyu ambayo ni mkutano huo wa ATAPE, Mkutano wa Madaktari wa Nchi nzima na Maonesho ya Nanenane ya Kimataifa.

Katika hatua nyingine amewahimiza wananchi kujifunza masuala ya Ujasiriamali na kuwakaribisha katika Maonesho ya Viwanda Vidogo SIDO yatakayofanyika Kitaifa mwaka huu 2018 kuanzia tarehe 24 hadi 28 Oktoba, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi.

Awali akitoa somo kuhusu masuala ya Ujasiriamali, Mchungaji Joshua Njuguna aliwasisitiza waumini wote kuwa siyo mpango wa Mungu mtu yeyote awe maskini , akawaasa kufanya kazi ili kuutafuta utajiri  hivyo akawataka wazitafute fursa za kupata utajiri  na kufanya kazi kwa bidii.

Pia Naibu Waziri MAVUNDE  ameahidi kuchangia jumla ya mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya kuwaunga mkono WAUMINI HAO katika  ujenzi wa Hospitali ya Kanisa  katika eneo la Pasiasi jijini Mwanza.

Ufunguzi wa makambi umehudhuriwa na waumini mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, lengo likiwa ni kujifunza neno la Mungu, kutoa elimu ya ujasiriamali, mafunzo ya ndoa na malezi ya watoto na  kuliombea Taifa. 
MWISHO

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu  Mhe. Anthony Mavunde(mwenye miwani), Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakikagua gwaride la Vijana Kanisa la Waadventista Wasabato katika ufunguzi wa makambi Mjini Bariadi, Septemba 18, 2018.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu  Mhe. Anthony Mavunde akivisha skafu na  Vijana Kanisa la Waadventista Wasabato kabla ya ufunguzi wa makambi Mjini Bariadi, Septemba 18, 2018 ambao alikuwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye skafu kulia)  akiimba pamoja na  Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA) Kurasini, katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo yanayofanyika Mjini Bariadi, Septemba 18, 2018 .
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA) wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu  Mhe. Anthony Mavunde katika ufunguzi wa makambi yanayofanyika  Mjini Bariadi, Septemba 18, 2018
Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA) wakiimba katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo yanayofanyika  Mjini Bariadi, Septemba 18, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu  Mhe. Anthony Mavunde(wa tatu kilia) na viongozi wengine wa Serikali na Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA), wakifuatilia mafundisho katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika  Mjini Bariadi
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu  Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Viongozi na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA), wakati akifungua makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika  Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA), katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika  Mjini Bariadi.
Mchungaji wa Kanisa la Waadiventista Wasabato kutoka Nchini Kenya Joshua Njuguna Kenya akitoa mafundisho, katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika  Mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu  Mhe. Anthony Mavunde (mwenye miwani) akipokea zawadi kutoka kwa wawakilishi wa wakina mama wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA), katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika  Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akipokea zawadi kutoka kwa wawakilishi wa wakina mama wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA), katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika  Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akipokea zawadi kutoka kwa wawakilishi wa wakina mama wa Kanisa la Waadventista Wasabato(SDA), katika ufunguzi wa makambi ya Kanisa hilo Septemba 18, 2018 ambayo yanafanyika  Mjini Bariadi

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge Kazi,Vijana ,Ajira na Walemavu  Mhe. Anthony Mavunde( wa pili kushoto ) akisalimiana na mmoja wa Viongozi wa ATAPE mkoa wa Simiyu, Eng. Paul Jidayi mara tu alipowasili Uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi kufungua makambi ya Kanisa la Waadiventista Wasabato(SDA) , Septemba 18, 2018.


Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!