Thursday, December 8, 2016

WANANCHI WAHIMIZWA KUTUMIA DAWATI LA JINSIA KUKABILIANA NA UKATILI WA KIJINSIA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na wananchi wa Bariadi (hawapo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP. Onesmo Lyanga na Afisa Usalama wa Taifa Mkoa wakipokea maandamano wa wananchi (hawapo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Watoto wa Kituo cha Watoto Yatima cha Home Of Peace cha Kanisa la K.K.K.T Bariadi wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi
Baadhi ya wananchi wa Bariadi wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Simiyu, ASP. Kajeng Muro akizungumza na wananchi wa Bariadi (hawapo pichani)  wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP. Onesmo Lyanga akizungumza na wananchi wa Bariadi (hawapo pichani)  wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi
Watoto wa Kituo cha Watoto Yatima cha Home Of Peace cha Kanisa la K.K.K.T Bariadi wakiwasilisha ujumbe wao  kwa njia ya ngonjera wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

Baadhi ya waimbaji wa kwaya ya Kanisa la AICT Bariadi wakitoa burudani ya wimbo kwenye Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.


Watoto wa Kituo cha Watoto Yatima cha Home Of Peace cha Kanisa la K.K.K.T Bariadi wakiwasilisha ujumbe wao  kwa njia ya ngonjera wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wadau wa mapambano dhidi ya Ukatiliwa Kijinsia wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi

Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wadau wa mapambano dhidi ya Ukatiliwa Kijinsia wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa na baadhi ya Maafisa wa Dawati la Jinsia na Watoto, mara baada ya kufunga maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi la Mkoa huo mara baada ya kufunga maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo mara baada ya kufunga maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa na Watendaji wa Wilaya ya Bariadi mara baada ya kufunga maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi
Baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi( Kikosi cha kuzuia Ghasia) wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.

Baadhi ya wananchi wa Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Na Stella Kalinga
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewahimiza wananchi wa Mkoa huo kulitumia vema Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Mtaka ameyasema hayo leo wakati alipozungumza na wananchi wa Bariadi katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Mkoani humo ambayo yamefanyika katika kituo cha mabasi cha zamani Mjini Bariadi.

Mtaka amesema Wananchi wanapaswa kutoa taarifa na malalamiko yao juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na mashambulio ya kudhuru mwili, ubakaji, ulawiti, mashambulio ya aibu, ndoa za utotoni na vitendo vingine vinavyofanywa katika jamii ili wahalifu wanaojihusisha na vitendo hivyo waweze kuchukuliwa hatua.

Aidha, Mtaka amesema pamoja na kulitumia Dawati la Jinsia lililopo katika vituo vya Polisi, wananchi wazitumie Ofisi za Serikali zikiwepo Ofisi za Vijiji/Mitaa, Kata, Wilaya na Mkoa katika kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia badala ya kwenda katika Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo baadhi huwatoza fedha katika kuwapa huduma hizo.

“Litumieni dawati la jinsia kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto wa kike na wanawake. Watumieni Maafisa Maendeleo ya jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii na maafisa wetu wengine wa Serikali mpewe huduma hizo bure, badala ya kupeleka malalamiko yenu kwenye mashirika au asasi ambazo si za Serikali zinazowatoza fedha” alisema Mtaka.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto  Mkoa wa Simiyu ASP. Kaneng Muro amesema Serikali kupitia Vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Polisi haitavumilia mtu yeyote atakayebainika kutenda vitendo vya kikatili na imejipanga kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa kabisa katika jamii.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu,ACP Onesmo Lyanga amesema wananchi waache kujichukulia sheria mkononi ikiwa ni pamoja na mauaji ya vikongwe kwa imani za kishirikina badala yake watoe taarifa za uhalifu katika vyombo vya dola ili vichukue hatua dhidi ya wahalifu hao kwa mujibu wa sheria.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa kazi linayofanya ya kupambana na uhalifu na hivyo kufanya mkoa kuwa salama.
Sanjari na hilo Mkuu huyo wa Mkoa amesema Mkoa wa Simiyu  unakabiliwa na tatizo la kuwaozesha watoto katika umri mdogo hali ambayo imesababisha vifo wakati wa kujifungua kwa baadhi ya watoto wa kike, msongo wa mawazo na kukosa maamuzi kwa kuwa wengi wao wanaolewa na watu wazima.

Katika kukabiliana na hilo Mtaka amesema wazazi wote wahakikishe watoto wao wanapelekwa shule ifikapo Januari mwaka 2017 na wasiwakatize masomo na kuwalazimisha kuolewa, ambapo alisema wale watakaokaidi watakuwa vibarua wa kufanya usafi katika Ofisi za Taasisi za Umma.

“Kama mtu anataka kuwa kibarua wa Serikali mwakani aache kumpeleka mtoto shule, atafanya usafi polisi, shuleni, hospitali,vituo vya afya, zahanati, masoko na maeneo mengine ya Umma. Hatuwezi kuwapa kazi askari wetu badala ya kulinda raia na mali zao waje wakulazimishe wewe umpeleke mwanao shule; nasema hivi ili tutakapoanza vitendo tusilaumiane” alisema Mtaka.

Mtaka ameongeza kuwa Serikali itawachukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kifungo baadhi ya watu wasio waadilifu ambao wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi wa kike na kukatiza masomo yao kwa kuwapa mimba, hali inayopelekea kuwa na ndoa za utotoni.


Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia hufanyika kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 10 kila mwaka ambapo Kauli Mbiu yaMaadhimisho haya mwaka 2016 ni “FUNGUKA, PINGA UKATILI WA KIJINSIA, ELIMU SALAMA KWA WOTE”

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!