Zikiwa zimebaki siku mbili kufanya mtihani wa Taifa
wa Darasa la Saba, wanafunzi wa darasa la saba mkoani Simiyu wamesema
wamedhamiria kushika nafasi ya kwanza Kitaifa katika mtihani huo kutokana na mikakati ya
taaluma iliyopo na maandalizi yaliyofanyika, huku wakiahidi kutoa wanafunzi
kumi bora Kitaifa.
Hayo
yamebainishwa na baadhi ya wanafunzi wa Shule za msingi Somanda A, Somanda B,
Sima A na Sima B za mjini Bariadi wakati wa ziara ya Viongozi wa Mkoa
wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika shule hizo
iliyokuwa na lengo la kujiridhisha na maandalizi na kuwatakia heri wanafunzi
watakaofanya mtihani huo.
“Tumejiandaa
vizuri na mtihani wa Taifa utakaofanyika tarehe 07 na 08 mwezi huu, walimu wetu
wametuandaa vizuri tunawashukuru sana walimu kwa kutufundisha vizuri, tulifanya
vizuri mtihani wa Mkock na tumejipanga kufanya vizuri zaidi mtihani wa Taifa,
tunaahidi kutoa wanafunzi watano katika
kumi bora Kitaifa,”Kija Masunga mwanafunzi wa darasa la Saba Somanda B.
“Nawashukuru
walimu kwa kutufundisha kutoka chekechea mpaka darasa la saba pia tunashukuru
uwepo wa kambi za kitaaluma zimetusaidia sana, baadhi ya wanafunzi katika shule
za serikali wanadanganywa na wazazi wao wakaandike majibu yasiyo sahihi ili
wakaozeshwe lakini kupitia kambi wanafunzi tunalindwa na tunajiamini,”Edina
Meshaki kutoka Sima A.
Aidha,
wanafunzi hao wameomba Serikali iendelee kuboresha miundombinu ya kujifunzia
ikiwa ni pamoja na uwekaji wa nishati ya umeme katika vyumba vyote vya madarasa
ili waweze kujisomea nyakati zote hususani wakati wa kambi za kitaaluma.
Mwalimu
Monica Silayo kutoka Shule ya Msingi Somanda B amesema wamewaandaa wanafunzi
vizuri ambapo amebainisha kuwa hata wakiletewa mtihani sasa hivi wako tayari
kufanya mtihani huo wa Taifa.
Naye
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sima A, Hamza Hamis amesema “sisi si watu wa
maneno ni watu wa vitendo hatuzungumzi mambo mengi lakini tunaahidi kuwa
tumejipanga, hili suala la kuwa namba
moja tumeliwekea mikakati toka mwaka jana tunafanya mwendelezo wa mikakati yetu
mwaka huu Simiyu hatukamatiki”.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewashukuru walimu wote wa mkoa wa Simiyu kwa kazi nzuri wanayoifanya na
kuwataka viongozi na watumishi wengine kutoa kipaumbele kwa walimu katika
maeneo ya huduma ili wapata nafasi ya kuwafundisha wanafunzi wao .
Kuhusu
zawadi kwa wanafunzi na walimu watakaofanya vizuri katika mtihani waTaifa wa
Darasa la Saba mwaka 2020 Mtaka amesema, “wanafunzi watakaoingia 10 Bora kitaifa
kila mmoja atapewa shilingi 500,000/= mwalimu atakayeongoza kwa ufaulu wa A
nyingi kimkoa kwa kila somo , atapewa shilingi 500,000/=, shule itakayoingia 10
bora Kitaifa itapewas hilingi milioni tatu, wilaya itakayoingia 10 bora walimu
wake wataenda kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.”
Katika
matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la saba mwaka 2019 wanafunzi mkoa wa
Simiyu ulitoa wanafunzi wanne walioingia katika 10 bora Kitaifa kwa shule za
Serikali na kila mwanafunzi aliepwa zawadi ya shilingi 300,000/=
Kwa mujibu wa Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.
Ernest Hinju jumla ya wanafunzi 30,779 wanatarajia kufanya mtihani wa Taifa wa
Darasa la Saba, huku akibainisha kuwa maandalizi yako vizuri ambayo yamechangiwa
na walimu, wazazi, viongozi na wadau wote wa elimu katika kufikia azma ya mkoa
ya kushika nambari moja Kitaifa.
MWISHO
Wanafunzi wa Darasa la
Saba katika Shule ya Msingi Somanda A na Somanda B Mjini Bariadi wakipokea
mkono wa heri kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati
alipowatembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujiridhisha na maandalizi na
kuwatakia heri wakati wakielekea katika Mtihani wa Taifa wanaotarajia kuufanya Oktoba
7-8, 2020.
Mmoja wa Wanafunzi wa
Darasa la Saba katika Shule ya Sima A Mjini akiwaongoza wanafunzi wenzake kwa dua maalum
kwa ajili ya kuombe Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba unaotarajiwa kufanyika
tarehe 7-8 Oktoba, 2020; (kulia) waliosimama juu ya meza ni Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka akiungana nao katika dua wakati alipowatembelea
shuleni hapo Oktoba 05, 2020 kujionea maandalizi na kuwatakia heri katika
mtihani huo.
M
wanafunzi wa darasa la
saba katika Shule ya Msingi Sima B Mjini Bariadi, akizungumza namna
walivyojiandaa na mtihani wa Taifa unatarajiwa kufanyika Oktoba 07-08, 2020
wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka iliyolenga kujionea maandalizi yaliyofanyika na kutakia kila la
heri katika mtihani huo. Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Shule ya Msingi Sima A Mjini Bariadi Mwl. Hamza Hamis akieleza
hali ya maandalizi ya mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba katika shule yak, wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa
wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Oktoba 05, 2020 iliyolenga kujionea maandalizi yaliyofanyika
na kuwatakia kila la heri wanafunzi wa darasa la saba katika mtihani huo.Wanafunzi wa Darasa la
Saba katika Shule ya Msingi Sima A na Sima
B Mjini Bariadi wakipokea mkono wa heri kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka wakati alipowatembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujiridhisha na maandalizi
na kuwatakia heri wakati wakielekea katika Mtihani wa Taifa wanaotarajia kuufanya Oktoba
7-8, 2020. Mwanafunzi wa darasa la
saba katika Shule ya Msingi Sima B Mjini Bariadi, akizungumza namna
walivyojiandaa na mtihani wa Taifa unatarajiwa kufanyika Oktoba 07-08, 2020
wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka iliyolenga kujionea maandalizi yaliyofanyika na kutakia kila la
heri katika mtihani huo. Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Sima A na Sima B
wakati alipotembelea shule hiyo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi kwa
lengo la kijiridhisha na hali ya maandalizi ya mtihani wa Taifa na kuwatakia
kila la heri katika mtihani huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 07-08, 2020.Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda A na
Somanda B wakati alipotembelea shule hiyo akiwa ameambatana na baadhi ya
viongozi kwa lengo la kijiridhisha na hali ya maandalizi ya mtihani wa Taifa na
kuwatakia kila la heri katika mtihani huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 07-08,
2020. Mkuu wa mkoa wa Simiyu,

2020. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo na wanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Sima A na Sima B na Mwalimu
Mkuu wa Sima A baada ya kukamilisha ziara yake katika shule hizo ikiwa na lengo
la kujiridhisha na maandalizi ya Mtihani wa Darasa la Saba na kuwatakia heri
wanafunzi wa Darasa la Saba wanaotarajia kuafanya mtihani huo Oktoba 07-08, 2020. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akifurahia jambo na
Samson Robert mwanafunzi wa
Darasa la Saba katika Shule ya Msingi
Sima B, baada ya kukamilisha ziara yake katika shule hiyo ikiwa na lengo la
kujiridhisha na maandalizi ya Mtihani wa Darasa la Saba na kuwatakia heri
wanafunzi wa Darasa la Saba wanaotarajia kuafanya mtihani huo Oktoba 07-08, 2020. Mwanafunzi wa darasa la
saba katika Shule ya Msingi Somanda B Mjini
Bariadi, akizungumza namna walivyojiandaa na mtihani wa Taifa unatarajiwa
kufanyika Oktoba 07-08, 2020 wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wakiongozwa na
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka iliyolenga kujionea maandalizi
yaliyofanyika na kutakia kila la heri katika mtihani huo. Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Somanda A na
Somanda B wakati alipotembelea shule hiyo akiwa ameambatana na baadhi ya
viongozi kwa lengo la kijiridhisha na hali ya maandalizi ya mtihani wa Taifa na
kuwatakia kila la heri katika mtihani huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 07-08,
2020. Wanafunzi wa Darasa la
Saba katika Shule ya Msingi Somanda A na Somanda B Mjini Bariadi wakipokea
mkono wa heri kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati
alipowatembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujiridhisha na maandalizi na
kuwatakia heri wakati wakielekea katika Mtihani wa Taifa wanaotarajia kuufanya Oktoba
7-8, 2020. Mmoja wa Wanafunzi wa
Darasa la Saba katika Shule ya Sima A Mjini akiwaongoza wanafunzi wenzake kwa dua maalum
kwa ajili ya kuombe Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba unaotarajiwa kufanyika
tarehe 7-8 Oktoba, 2020; (kulia) waliosimama juu ya meza ni Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka akiungana nao katika dua wakati alipowatembelea
shuleni hapo Oktoba 05, 2020 kujionea maandalizi na kuwatakia heri katika
mtihani huo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Sima A na Sima B wakifurahia jambo
0 comments:
Post a Comment