Wednesday, October 21, 2020

SERIKALI YATOA BILIONI 1.2 KULIPA WAKULIMA WA PAMBA SIMIYU

Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya kukamilisha malipo ya madeni ya wakulima wa pamba kwa msimu wa mwaka 2019 mkoani Simiyu, ambapo kufikia tarehe 21 Oktoba 2020 wakulima wote waliokuwa wanadai fedha watakuwa wameshalipwa fedha zao. 

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka jana tarehe 19 Oktoba 2020 katika kikao cha wadau wa pamba kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa mpango mkakati wa mageuzi ya kilimo cha zao la pamba kwa mwaka 2019/2020 na mpango wa uzalishaji kwa mwaka 2020/2021. 

" Tulishafanya uhakiki wa wakulima wetu wote, kufikia Jumatano wakulima wote waliokuwa wanadai malipo ya pamba kwa mwaka 2019 watakuwa wamelipwa fedha zao; vyama vya ushirika hakikisheni kila mkulima anapata fedha yake, ole wenu wakulima walalamike kuwa hawajapaya fedha zao au fedha zao zimekatwa mtakuwa hamjipendi," alisema Mtaka. 

Aidha, Mtaka amewakata Maafisa Ushirika wa Halmashauri waandae taarifa ya malipo ya pamba kwa wakulima kwa malipo ya awamu ya kwanza yaliyofanyika Septemba na malipo yanayofanyika sasa ili kupata takwimu za wakulima waliolipwa, kilo zilizolipwa na fedha zilizolipwa kwa kila mkulima ifikapo Oktoba 22, 2020. 

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesisitiza umuhimu wa Vyama vya msingi vya Ushirika (AMCOS) vipatavyo 70 vya mfano kuingia mkataba na makampuni ya ununuzi wa pamba ili Bodi ya pamba itakapotoa leseni za ununuzi wa pamba isitoe leseni kwa wanunuzi wengine kununua katika AMCOS hizo. 

“Ninataka hizi AMCOS 70 kwa kupitia Bodi ya pamba, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika mtambue kampuni ambayo itaingia mikataba na hizi AMCOS moja kwa moja ili Bodi ya pamba itakapotoa leseni isitoe leseni kwa mnunuzi mwingine kwenda kwenye hizo AMCOS,” alisema Bashe.

Katika hatua nyingine Bashe amesema ni vema wakulima wenye mashamba ya pamba yaliyosajiliwa wapewe hati za kimila wapewe hati za kimila ili waweze kukopesheka, huku akitoa wito kwa taasisi za fedha kutoka kwenye mifumo za kizamani ya biashara (utoaji mikopo) ili mifumo ya mikopo iwe na uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya kilimo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga amesema ipo haja kwa wadau wa pamba kuona namna ya kuwasaidia wakulima kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba kwa kuwa kumekuwa na dhana kwamba bei ya pamba ndiyo tatizo, ambapo amebainisha kuwa changamoto kubwa katika uzalishaji wa pamba ni tija ndogo. 

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Gatsby Tanzania ambalo limeshiriki kuandaa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mkoani Simiyu, Bw. Samwel Kilua amesema kama wadau muhimu wamejipanga kufanikisha mkoa wa Simiyu kuwa mfano wa maeneo mengine yanayozalisha pamba.

Akiwasilisha taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa mpango mkakati wa mageuzi ya kilimo cha zao la pamba kwa mwaka 2019/2020 na mpango wa uzalishaji kwa mwaka 2020/2021, Afisa Kilimo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Kija Kayenze amesema katika msimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2020/2021 unaoendelea hadi kufikia tarehe 04 Oktoba 2020 kilo 111,610,227 zimeshanunuliwa. 

Aidha, Kayenze amesema Mkoa wa Simiyu unaongoza kwa kilo 62,822,941 za pamba mbegu ambazo kati yake kilo 4,479,117 ni pamba kilimo hai.

MWISHO  

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba wakifuatilia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe akizungumza na viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Miriam Mmbaga akielezea jambo katika kikao cha viongozi na na wadau mbalimbali wa zao la pamba katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.

Baadhi ya viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) wakifuatilia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi kikiwahusisha viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba .

Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba wakifuatilia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mkuu wa Gatsby Africa Bw. Samwel Kilua akiwasilisha mada katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadiambapo Gatsby ilishirikiana na Ofisi ya mkuu wa Mkoa kuandaa mkakati huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Bw. Marco Mtunga akitoa ufafanuzi wa jambo katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Afisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Kija Kayenze akiwasilisha taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akichangia hoja katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Aswege Kaminyoge  akichangia hoja katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Mageuzi ya uzalishaji wa zao la Pamba mwaka 2020/2021 Mkoani  Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi

Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba wakifuatilia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.


Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wa zao la pamba wakifuatilia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa mageuzi ya uzalishaji wa zao la pamba mwaka 2020/2021 Mkoani Simiyu, kilichofanyika tarehe 19 Oktoba 2020 Mjini Bariadi.




0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!