Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa
wito kwa wazazi na walezi kuwapunguzia kazi wanafunzi wenye madarasa ya mitihani ya Taifa
ya darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne ambayo inatarajiwa
kufanyika mwezi Novemba ili waweze kujipatia muda mwingi wa kujisomea kujiandaa
na mitihani hiyo.
Mtaka ameyasema hayo jana wakati makabidhiano ya Chuo cha Ufundi Kasoli katika Kijiji cha Kasoli wilayani
Bariadi kilichojengwa na mwekezaji Alliance Ginnery Limited na kukabidhiwa kwa
Serikali na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt.
Maduhu Kazi kwa niaba ya kampuni hiyo na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka kwa niaba ya wananchi.
“Darasa la saba wameshafanya mtihani wao, watoto wa
darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne waendelee kufanya maandalizi,
wazazi na walezi wapunguzieni kazi watoto wote walio kwenye madarasa haya na
wakiwa nyumbani wafanye majadiliano ya pamoja,” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amewaonya wazazi na walezi wenye nia ya
kuwaozesha wanafunzi wa kike waliohitimu elimu ya msingi na kutoa wito kwa
jamii yote kuwa walinzi wa watoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao.
Mtaka ameishukuru Kampuni ya Allience Ginnery
kujenga chuo cha ufundi Kasoli na kutoa wito kwa wasichana na wanawake kijiji
cha Kasoli kujitokeza kupata mafunzo ya ushonaji bila malipo katika chuo hicho
katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba, kabla ya kuanza kwa mafunzo yatakayoanza
mwakani kwa mtaala wa Serikali na kuahidi kutoa vyerehani 25.
Meneja
Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola amesema Kampuni hiyo imekuwa
inajihusisha sana na maendeleo ya jamii katika sekta ya elimu, afya na maji kwa
kuwa wao ni sehemu ya jamii, ni wajibu wao kufanya hivyo na ni sehemu ya maelekezo ya TIC
wanayopewa wawekezaji wote.
“Tunashiriki
kwenye masuala ya jamii kwa sababu sisi ni sehemu ya jamii, sisi tunashughulika
na wakulima na wanaotulimia pamba na kutuuzia kutuwezesha kuendesha kiwanda
chetu, siku za nyuma tulijikita kwenye afya, maji na elimu ya msingi na
sekondari; tumeona haja ya kujenga chuo cha ufundi ili wanafunzi watakaoshindwa
kuendelea na masomo, wapate mafunzo ya
ufundi ili waweze kujitegemea,” alisema Ogola.
Aidha,
Ogola amesema pamoja na mafunzo ya ufundi mipango ya baadaye ya kampuni ya
Alliance Ginnery kuongeza darasa moja la wakulima kwa lengo la kutoa warsha na
mafunzo kwa wakulima ili waweze kulima kilimo chenye tija ili kampuni hiyo
iweze kupata malighafi bora kwa ajili ya kiwanda chake cha kuchambua pamba..
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),
Dkt. Maduhu Kazi ameipongeza na kuishukuru Kampuni ya Alliance Ginnery kujenga
chuo cha Ufundi na kutoa wito kwa wawekezaji wengine kuona umuhimu wa kuwafikia
wananchi walio katika maeneo yao huku akiahidi kuwa TIC itahakikisha kinakuwa
mstari wa mbele kutatua changamoto zinazowakabili wawekezaji.
“TIC
inashirikiana na Serikali hata ngazi ya mikoa na tumejielekeza zaidi kuongeza
ufanisi katika shughuli zetu za kuwasaidia wawekezaji masuala ya vibali kwa
kushirikiana na Taasisi zinazohusika; pia tumejipanga hata kuwafikia wawekezaji
wadogo Watanzania maana baada ya tathmini tumeona eneo hilo kuna mapungufu
maana wengi wanadhani sisi tunahusika na wawekezaji wa kigeni tu,” alisema Dkt.
Kazi.
Naye
Mkazi wa Kijiji cha Kasoli Shamsa Abdallah amesema anaishukuru Kampuni ya Alliance
Ginnery kwa kuwajengea chuo cha ufundi na anaamini kuwa kitawasadia kwenye
mafunzo ya ushonaji na mafunzo
yanayohusiana na kilimo yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.
Kampuni ya Alliance Ginnery Limited imejenga majengo
ya chuo cha ufundi kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 180, kuchimba
kisima cha maji chenye uwezo wa kutoa lita 5000 kwa saa pamoja na kuweka vifaa
kama vyerehani, majiko ya gesi na vifaa
mbalimbali vya kujifunzia upishi,vifaa vya kujifunzia uashi na useremala meza
na viti vya ofisi.
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (wa tatu kulia) akikata
utepe kufungua chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na Mwekezaji wa Kampuni ya Alliance
Ginnery na baadaye kukabidhiwa kwa Serikali jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi
mkoani Simiyu.
Sehemu ya majengo ya chuo
cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na Mwekezaji wa Kampuni ya Alliance
Ginnery na baadaye kukabidhiwa kwa Serikali iliyopo katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi
mkoani Simiyu. Meneja Mkuu wa Alliance
Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji
wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (mwenye
skafu) juu ya shule ya ufundi Kasoli iliyojengwa na kampuni hiyo kwa msaada na
kuikabidhi kwa serikali, baada ya kukifungua chuo hicho jana katika Kijiji cha
Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi akiyaangalia maji
yanayotoka katika kisima kilichochimbwa kwenye shule ya ufundi ya Kasoli iliyojengwa
kwa msaada na kampuni Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali, baada ya
kuifungua chuo hicho jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani
Simiyu.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi, Meneja Mkuu wa Alliance
Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
wakifurahia na wananchi katika kijiji cha Kasoli baada ya ufunguzi wa chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada
na kampuni Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali jana kijijini hapo. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto ) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi mara baada ya makabidhiano ya chuo
cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Alliance Ginnery na
kuikabidhi kwa serikali, katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani
Simiyu. Meneja Mkuu wa Alliance
Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akiwaongoza Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (mwenye skafu) na viongozi wengine kukagua chuo
cha ufundi ya Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni Alliance Ginnery na
kuikabidhi kwa serikali, baada ya kuifungua shule hiyo jana katika Kijiji cha
Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Meneja Mkuu wa Alliance
Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji
wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (mwenye
skafu) juu ya vifaa mbalimbali vilivyopo katika chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa na kampuni
hiyo kwa msaada na kuikabidhi kwa serikali, baada ya kuifungua chuo hicho jana katika
Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Kutoka kulia Meneja
Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo
cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakuteta jambo baada
ya makabidhiano ya chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni ya
Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali, katika Kijiji cha Kasoli wilayani
Bariadi mkoani Simiyu. Kutoka kulia Meneja
Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo
cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakiwa katika
picha ya pamoja jana baada ya makabidhiano ya chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa
kwa msaada na kampuni ya Alliance Ginnery na kuikabidhi kwa serikali, katika
Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Wasanii wa kundi la
FUTUHI kutoka jijini Mwanza wakitoa burudani katika hafla ya makabidhiano ya
shule ya ufundi ya Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Alliance Ginnery
na kukikabidhi kwa serikali, katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani
Simiyu.
Meneja Mkuu wa Alliance
Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akiwaongoza Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (mwenye skafu) na viongozi wengine kukagua chuo
cha ufundi ya Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni Alliance Ginnery na kukikabidhi
kwa serikali, baada ya kukifungua chuo hicho jana katika Kijiji cha Kasoli
wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Meneja Mkuu wa Alliance
Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji
wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (mwenye
skafu) juu ya chuo cha ufundi Kasoli
iliyojengwa na kampuni hiyo kwa msaada na kuikabidhi kwa serikali, baada ya
kuifungua chuo hicho jana katika Kijiji
cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto ) akiagana na na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi mara baada ya makabidhiano ya chuo
cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Alliance Ginnery na
kuikabidhi kwa serikali, katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani
Simiyu.
Meneja Mkuu wa Alliance
Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji
wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (mwenye
skafu) na viongozi wengine juu ya maeneo
mbalimbali ya shule ya ufundi Kasoli
iliyojengwa na kampuni hiyo kwa msaada na kukikabidhi kwa serikali, baada ya kukifungua
chuo hicho jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (mwenye skafu) akifurahia
burudani ya nyimbo kutoka kwa msaani Elizabeth Maliganya (mwenye kipaza sauti)
wakati wa ufunguzi wa chuo cha ufundi Kasoli
Sehemu ya majengo ya chuo
cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na Mwekezaji wa Kampuni ya Alliance
Ginnery na baadaye kukabidhiwa kwa Serikali iliyopo katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi
mkoani Simiyu.
Baadhi ya wananchi wa
kijiji cha Kasoli wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya shule ya ufundi Kasoli
iliyojengwa na mwekezaji kampuni ya Alliance Ginnery kwa msaada na kuikabidhi kwa serikali, baada
ya kukifungua chuo hicho jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani
Simiyu. Viongozi mbalimbali wa
mkoa wa Simiyu wakishangilia baada ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (wa tatu kulia)
kufungua chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na Mwekezaji wa Kampuni ya Alliance
Ginnery na baadaye kukabidhiwa kwa Serikali jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi
mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi (wa tatu kulia) akipanda
mti wa kumbukumbu mara baada ya kufungua
shule ya ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na Mwekezaji wa Kampuni ya Alliance
Ginnery na baadaye kukabidhiwa kwa Serikali jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi
mkoani Simiyu. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto ) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji
wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi mara baada ya makabidhiano ya chuo cha ufundi
Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni ya Alliance Ginnery na kukikabidhi kwa
serikali, katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania-TIC, Dkt. Maduhu Kazi, Meneja Mkuu wa Alliance Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakifurahia na wananchi katika kijiji cha Kasoli baada ya ufunguzi wa chuo cha ufundi Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni Alliance Ginnery na kukikabidhi kwa serikali jana kijijini hapo.Meneja Mkuu wa Alliance
Ginnery Limited, Bw. Boaz Ogola(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka katika hafla ya makabidhiano ya Chuo cha ufundi Kasoli
iliyojengwa kwa msaada na mwekezaji kampuni ya Alliance Ginnery na kukikabidhi kwa serikali, baada ya kukifungua
shule hiyo jana katika Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akiyaangalia maji yanayotoka katika kisima kilichochimbwa
kwenye shule ya ufundi ya Kasoli iliyojengwa kwa msaada na kampuni Alliance
Ginnery na kuikabidhi kwa serikali, baada ya kuifungua chuo hicho jana katika
Kijiji cha Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu
0 comments:
Post a Comment