Thursday, November 18, 2021

UZINDUZI WA UGAWAJI PIKIPIKI KITAIFA KWA MAAFISA UGANI KATIKA MIKOA INAYOZALISHA MAZAO KIMKAKATI, WAFANYIKA MKOANI SIMIYU.

Akizungumza,Mkurugenzi mkuu Bodi ya Pamba, Bw. Marco Mtunga alitoa shukrani kwa Waziri wa kilimo Mhe. Adolf Mkenda kwa kukubali kuhudhuria zoezi la ugawaji wa pikipiki. 

Pongezi kwa mkoa wa Simiyu kwa kuzalisha zaidi ya asilimia 61 ya pamba yote nchini msimu huu wa kilimo.Tatizo la msingi katika sekta ya kilimo ni kupungukiwa maarifa kwa sababu ya wataalamu kutowezeshwa ipasavyo.

Mkakati wa Wizara ni kuimarisha huduma za ughani. Maafisa ughani wote watakuwa na pikipiki kwa sababu ni vigumu kwa afisa ugani mmoja asiye na usafiri kutembelea kata nzima.Hivyo leo wataalam watapewa vitendea kazi ili waweze kuwafikia wakulima.Wakulima wafuate kanuni za kilimo.Lengo la zoezi la leo ni kuhakikisha mkulima anaboreshewa kielimu. Maafisa ughani wasitumie pikipiki kama biashara.Halmashauri zinapaswa kusimamia vizuri zoezi la kilimo cha pamba ili kuongeza mapato 


Dr. Sophia Kashenge Mkurugenzi Mkuu Wakala wa Mbegu za Kilimo,Tanzania, alitoa pongezi na shukrani kwa Wizara ya Kilimo kwa kutoa kipaumbele kikubwa kwa kazi ambazo zilikuwa hazipewi kipaumbele. Kazi ya Wakala wa mbegu za Kilimo ni kuhakikisha mbegu zinazogunduliwa na mtafiti zinamfikia mkulima na kuzizalisha kwa wingi ili zifike kwa mkulima kuendana na uhitaji.

Wakala wanafanya kazi kupitia mashamba kumi na nne ya mbegu ya serikali. Ombi letu kwa Serikali, ni kutuongeza mashamba kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu.

Mkoa wa Simiyu umepokea mbegu za alizeti tani 114 ambapo tani 60 zimepelekwa Halmashauri ya Wilaya ya itilima, tani 34 Meatu na tani 20 Maswa kwa ajili ya kilimo cha alizeti.Aidha, Wakala wa mbegu za kilimo wameanzisha duka la mbegu mkoa wa Si 

Akizungumza,Balozi wa Pamba Bw. Agrey Mwanri alitoa Shukrani kwa Wizara/Serikali kwa maamuzi ya kukubali mbegu zitolewe kwa mkopo. Hili ni jambo la busara kwani Wakulima watakatwa mikopo hiyo wakati wakiuza mazao yao.

Shukrani kwa Waziri Prof. Adolf Mkenda kwa kuja kutoa pikipiki. Tahadhari kwa Maafisa Ugani mnapaswa kutumia pikipiki kwa kazi iliyokusudiwa pekee. 

Nitumie fursa hii kuwashauri wakuu wa Wilaya/Mikoa kusimamia matumizi sahihi ya pikipiki hizo na kuhakikisha zinafanya kazi iliyo kusudiwa.

Kuleta vitendea kazi ambavyo watumishi wataenda kivitumia na kurahisisha kazi ya kilimo ni ukomavu wa kisiasa. 

Kila mkulima wa Pamba akimaliza kuvuna Pamba ahakikishe anatoa masalia yote ili kuhakikisha msimu mpya unapoanza yasiwepo mabaki na masalia yote ya pamba ili kukabiliana na wadudu waharibifu. 

Zoezi la kutoa masalia halijafanyika katika utimilifu kwani baadhi ya wakulima hawajatoa hivyo naomba Serikali kuwachukulia hatua. 

 M/kiti CCM Mkoa wa Simiyu Bi.Shemsa Mohamed alieleza lengo letu ni kuhakikisha Simiyu inakwenda kuwa kinara wa uzalishaji wa Pamba na kilimo cha biashara. Ombi la wakulima ni kupunguziwa makato ya (Amcos, Union, Bodi ya Pamba) pamoja na ongezeko la bei ya mbegu usiokuwa na utaratibu mzuri. 

Maafisa Ugani wanapaswa kutumia pikipiki kwa kazi ambayo Serikali imemtuma pamoja na kuhakikisha wakulima wanapata tija na kuongeza uzalishaji wa Pamba.

Amcos hazinufaishi wakulima. Pamba ni zao linalotegemewa na wakulima kuwainua ki uchumi hivyo  Amcos ziwe na utaratibu ambao mkulima atanufaika moja kwa moja.

Katibu mkuu wizara ya kilimo- Bw. Andrea Masawe,alisema ugawaji wa Pikipiki ni hatua ya utekelezaji wa kile Serikali ilichoahidi ikiwa ni kipaumbele cha tatu cha mkakati wa kuongeza tija ya kilimo nchini.

Nina imani kubwa kuwa uwekezaji uliofanyika una kwenda kuboresha huduma za ugani ili mkulima apate elimu ya uhakika ya kanuni bora za kilimo.

Maafisa ugani 258 kutoka mikoa 3 na 1018 kutoka mikoa 18, wamepata mafunzo. Mkoa wa Simiyu una maafisa ugani 134 ambao wamepata mafunzo hayo.

Tunategemea kutakuwa na mashamba darasa mawili kwa kila afisa ugani na shamba darasa moja la mfano. Uzinduzi huu ni sehemu kidogo ya zoezi kubwa la kugawa vitendea kazi kwa wakulima.Wizara imeimarisha taasisi kutoa ushirikiano kwa taasisi zake katika utendaji wa kazi.Mkoa wa simiyu umepokea pikipiki 86. 

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila alieleza, Mkoa wa Simiyu ni mkoa wa kilimo. Asilimia 92 ya mkoa ni vijiji na wakazi wake ni Wakulima. 

Niwahakikishie kuwa Afisa Ugani yeyote atakayetumia Pikipiki kufanya bodaboda hatakuwa mtumishi wa Serikali katika mkoa wa Simiyu. 

Mkoa umetengeneza vikosi katika ngazi zote hivyo pikipiki hizi zitakwenda kusaidia hasa ngazi ya kijiji na kata ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa Pamba.

Utekelezaji wa azimio la Meatu la uzalishaji wa Pamba, Wizara ikiunga mkono mkakati huu itaongeza uzalishaji wa Pamba nchini. Mkoa utahakikisha watumishi ambao sio waadiilifu katika vyama vya Ushirika, Ushirika unawaondoa.Lengo la kuchukua hatua kali ni sababu ya kilio cha muda mrefu cha wakulima kudhurumiwa haki zao kwa sababu utaratibu unakiukwa huku sheria ikimbana mkulima auze katika ushirika. 

Mkoa una Amcos zaidi ya 300 hivyo mkoa unaomba kupatiwa mafunzo kwa watumishi wa Amcosi ili kuondoa mapungufu yaliyopo ambapo watumishi wanaonekana sio waadilifu kwa sababu ya kukosa maarifa.Wizara iendelee kuwezesha mikakati ya kuinua kilimo cha Pamba ambapo kwa sasa halmashauri zinabeba mzigo wa kuwezesha mikakati hiyo. 

Mkoa wa Simiyu umeteuliwa kuwa mkoa ambao unazalisha mafuta kwa kiwango kikubwa .Hivyo naoimba Wizara kuwezesha mikakati ya kuhakikisha mkoa unafikia malengo ya kuongeza uzalishaji. Mkoa utatumia shule kama mashamba darasa katika kuzalisha alizeti na kila shule itakuwa na mshamba darasa ya Alizeti pamoja na Pamba. Mkoa unahamasisha vilimo mbalimbali vya biashara kwenye kila wilaya.

Matumaini yetu ni kuwa mkoa wa Simiyu utaendelea kuwa karibu na Wizara kwa sababu m 92% ni wakulima na ni mkoa wa mfano katika kilimo. 

Akizungumza, Waziri wa kilimo Mhe.Prof. Adolf Mkenda, alisema kugawa pikipiki ni zoezi la kurudisha hadhi ya maafisa ugani. Nimpongeze mkuu wa Mkoa kwa jitihada za kuhakikisha anaongeza tija kwenye kilimo katika Mkoa wa Simiyu.Kama hatutawathamini Madaico na Maafisa ugani hatutafikia kile kilichoagizwa na ilani ya chama cha mapinduzi 

Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila mkulima anapata kilo zaidi ya 1000 kwa ekari kwenye zao la Pamba.Tija ikiwa ndogo wanapata shida kwenye uzallishaji wa malighafi katika viwanda. Lengo kubwa la kilimo ni kupunguza bei ya mazao katika nchi yetu na kuongeza kipato cha wakulima. Hivyo ni wajibu wa Serikali kuhakikisha inamuwezesha mkulima kuzalisha mazao mengi zaidi ili hata kama bei ya mazao itakuwa ndogo mkulima bado atapata faida. Tunataka hata Bei ya mazao ikishuka lakini kipato cha mkulima kiongezeke.Hii inawekana kwa kuongeza tija ya kilimo. 

Changamoto kubwa kwenye kilimo ni tija. Baada ya utafiti wa kilimo bora na kupata mbegu bora za pamba kwa sasa tunaendelea na kuboresha kazi za ugani. Afisa ugani anajukumu la kupeleka matokeo ya utafiti kwa wakulima na kufundisha matumizi ya mbegu bora. Maafisa ugani wanajukumu la kuwafundisha wakulima mabadiliko ya hali ya hewa ili waweze kulima mazao yanayokabiliana na ukame. 

 Hatuwezi kupuuza huduma za ugani tukabaki salama Hakuna maafisa ugani wa kutosha, nchi ina maafisa ugani 6704 sawa na asilimia 32.6 uhitaji ukiwa ni maafisa ugani 20538. Hakuna Vitendea kazi vya kutosha kwa wasimamizi wa shughuli za ugani na ushirika (Daico) hawana vitendea kazi kama magari na hakuna bajeti ya kuwawezeaha kuendesha shughuli za ugani katika ngazi zilizo chini yao. Kuwapatia mafunzo maafisa ugani ili kurejesha kilimo cha kisasa . 

 Makusanyo ya mapato ya Halmashauri nyingi yanategemea kilimo, licha ya kuwa wasimamizi wa kilimo hawapewi kipaumbele cha mahitaji yao katika kuwawezesha kufanya kazi yao. Halmashauri hutenga fedha kwa ajili ya maafisa ugani, Wizara itatoa mafuta kwa msimu huu wa kilimo pamoja na vipuli baada ya msimu huu wa kilimo Halmashauri zitaendelea na zoezi hilo. 

 Niahidi; Maafisa ugani kufufua mashamba darasa pamoja kupatiwa mafuzo rejea. Maafisa ugani kwa mikoa mitatu kununuliwa simu janja kwa ajili ya kujaza taarifa za wakulima wanapo watembelea wakulima kutatua changamoto za wakulima Bodi zote za mazao zitanunua pikipiki kwa ajili ya kuboresha huduma za ugani. Maafisa ugani wanapaswa kutunza pikipiki vizuri. Wakulima wazingatie kung'oa mabaki ili kumaliza magonjwa ya pamba. Ambaye hajang'oa masalia atachukuliwa hatua za kisheria. 

Mwisho.

Waziri wa Kilimo Mhe.Prof. Adolf Mkenda akifanya uzinduzi wa Kitaifa wa Ugawaji Pikipiki kwa Maafisa ugani katika mikoa inayozalisha Mazao ya Kimkakati,

Picha za baadhi ya pikipiki zilizogawiwa kwa maafisa Ugani, jumla ya pikipiki 86 ziligaiwa kwa maafisa Ugani.


Picha za Viongozi baada ya uzinduzi wa ugawaji Pikipiki

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca  Kayombo akijaribu Pikipiki zilizogawiwa kwa maafisa ugani







Wakuu wa Wilaya za Dodoma wakipokea mbegu na mafuta ya alizeti kutoka kwenye duka la Wakala la mbegu, duka ambalo limefunguliwa Mkoani Simiyu.Mbegu hizo zilitolewa na Waziri wa kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda.

WAZIRI MKUU MSTAAFU NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM ATEMBELEA OFISI YA MKUU WA MKOA SIMIYU

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Mizengo K.Pinda , jumatatu tarehe 15/11/2021,alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kusaini Kitabu cha Wageni ambapo Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.Mhe David Z.Kafulila aliwasilisha kwake taarifa fupi katika Sekta mbalimbali za Miradi ya Maendeleo.


Mhe.Pinda alisisitiza miradi ya utekelezaji kwa fedha za covid 19 usimamiwe kikamilifu na Mkoa na kusiwepo na ubadhirifu wowote. Aidha alisisitiza viongozi wa CCM wasihusike kwa vyovyote vile katika utekelezaji wa miradi hiyo kuepusha mgongano  wa maslahi.  

Mhe.Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa alisisitiza suala la Udumavu(Malnutrition), lisimamiwe kikamilifu ili takwimu za Mkoa kwenye udumavu lishuke au liishe kabisa.

Mwisho.*

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Mizengo K.Pinda atembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala, Mkuu wa Wilaya Bariadi

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Mizengo K.Pinda akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Simiyu

Wednesday, November 17, 2021

SIMIYU YASHIKA NAFASI YA 4 KUTOKA NAFASI YA 20 (2019) MIRADI YA MWENGE KITAIFA !

Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe.David Kafulila, leo amewapongeza wakurugenzi wa wakuu wa wilaya 5 za Mkoa wa Simiyu kwa kuendelea kuboresha usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusisitiza kuwa ni juhudi hizo zilizofanikisha mkoa wa simiyu kushika nafasi ya 4 mwaka huu 2021 kutoka nafasi ya 20 mwaka 2019.

 " Mimi naona fahari kuwa na timu hii ya wakuu wa wilaya na wakurugenzi. Mbali ya kupaisha mkoa huu kutoka nafasi ya 2 kutoka mwisho mwaka 2020 mpaka nafasi ya 2 juu katika makusanyo ya halmashauri kimkoa, leo nimepata taarifa kuwa mkoa wetu umeshika nafasi ya 4 kitaifa katika miradi ya mwenge iliyokaguliwa kulinganisha na nafasi ya 20 mwaka 2019.

 Naamini mwakani tutashika nafasi ya 1." Angalia hapa Busega, taarifa ya makusanyo ya robo ya mwaka wa fedha 2020 ilikuwa asilimia 15% ya lengo, kulinganisha na asilimia 29% kwenye robo ya kwanza mwaka 2021. Hivyo inawezekana. Tuendelee kupambana kujenga mkoa wetu " alisisitiza Kafulila wakati wa kikao cha mabaraza la Madiwani Wilayani Busega.

 Mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu  Mhe.David Kafulika akipokea mwenge wa Uhuru June 28,2021 kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Ally  Hapi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulia akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria.



Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu wakikabidhiana Mwenge wa Uhuru



MKUU WA MKOA WA SIMIYU ATAKA KASI ZAIDI UJENZI WA MADARASA YA UVIKO/IMF

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amefanya ukaguzi wa ujenzi madarasa 6 katika shule tatu za Sekondari ( Mwakaleka, Nyalikungu na Binza) zilizopo wilayani Maswa na kubainisha kuwa taratibu za ujenzi zinaonekana kwenda vema na kuzitaka Kamati za shule zinazosimamia ujenzi kuhakikisha mambo matatu; ubora, kasi na thamani kwa maana ya bei. Amezipongeza Kamati za shule zinazosimamia ujenzi na kuelekeza Halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Maswa kuhakikisha Kamati hizo zinamiliki miradi hiyo kwa kufanya kila kitu ili kupunguza urasimu katika maeneo ambayo shule zimejipanga vizuri. Mkoa wa Simiyu umepokea zaidi ya TZS.11.6/-Bln, kwa ajili ya miradi na mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano ya Uviko-19, ambapo Wilaya zilipokea fedha zifuatazo: Maswa Tsh. 2.1 bln, Meatu Tsh.2.0 bln, Busega Tsh.bln na Bariadi vijijini Tsh. 2.05 bln. 

Mwisho.




Mkuu wa Mkoa Mhe David Kafulila akitembelea  miradi ya ujenzi wa shule za Uviko-19/IMF







Mhe. Kafulila akiwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Simiyu Bi. Shamsa Mohamed  na baadhi ya Viongozi wa Mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wakitembelea miradi ya Ujenzi ya Shule 6 za Sekondari





MKOA WA SIMIYU KUWA KATI YA MIKOA MITANO ITAKAYONUFAIKA NA MRADI WANNE WA TASAF (TPRP IV) .

Akizungumza wakati wa kikao kazi cha kuzindua Utekelezaji wa awamu ya Nne ya Mradi wa Kupunguza Umaskini Tanzania (TPRP IV), na Viongozi na watedaji wa Mkoa wa Simiyu, Mkurugenzi Mtendaji wa TASA,  Bw.Ladislaus Mwamanga,alisema kuwa lengo la kikao kazi hicho ni kuzungumza na Viongozi na watendaji wa Mkoa wa Simiyu juu wa utekelezaji wa awamu ya nne ya mradi wa kupunguza Umaskini Tanzania ambapo pamoja na hayo mada mbalimbali kuhusu utaratibu wa kutuma fedha, majukumu  ya wadau wa ngazi zote yatawasilishwa.

 Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa mitano nchini Tanzania itakayonufaika na mradi wa (TPRP IV) ambao kwa ujumla wake utagharimu kiasi cha Dola za Marekani 50 Milioni. Mkoa Wa Simiyu unategemea kunufaika kwa takribani Tsh. 24.3Bln.

 Meneja miradi TASAF Bw. Paul Kijazi akiwasilisha mada alieleza kuwa TASAF imekuwa ikifanya miradi mbalimbali ya kupunguza umaskini nchini Tanzania ulifanyika. Mradi wa nne wa TASAF utahusisha mikoa 5 na wilaya 33.Mradi huo utakuwa na thamani ya USd. 50 mln. Aidha Bw.Kijazi alieleza kuwa miradi ya aina tatu ndio itakayotekelezwa ikiwa ni pamoja na;Miradi ya Jamii, miradi ya kuongeza kipato na miradi ya kutoa ajira ya muda kwa kaya za walengwa.Tathimini za miradi hiyo zitakuwa zikifanyika kila baada ya miezi sita ya kwanza baada ya mradi kuanza. 

 Aidha Bi.Sekela Mwakatumbula aliwasilisha mada kuhusu utaratibu wa kutuma Fedha iliwasilishwa ambapo TASAF waliwaeleza viongozi na wadau kuwa TASAF hutuma fedha kwa wakati na kuhakikisha kuwa mradi unatekelezwa kwa kipindi kilichopangwa.Fedha inayotolewa kwa mradi inatakiwa itumike kwa mradi husika na si vingenevyo, ni vyema wanakijiji wakahusishwa katika miradi kwani wafadhili hupenda kuzungumza na wanakijiji wenyewe. Asilimia 88 ya fedha hutolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi,asilimia 1 ya fedha huenda kwa Katibu Tawala, ambazo hutumika kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji, aidha viongozi walishauriwa kutembelea miradi wakiwa na wataalam. Asilimia 8.5% ya fedha hizo hupelekwa Halmashauri, 3.5% hutolewa mapema kwa ajili ya kuibua na kutathimini miradi,na 5% huwasilishwa baadae. Asilimia 1.5 hutumwa katika kata kwa ajili ya usimamizi wa utekelezaji wa miradi.Baada ya kupokea fedha hizo ni muhimu barua na stakabadhi zikatumwa kwa wakati. 

 Bw. Abdulmariki Shaaban aliwaeleza Viongozi na Wataalamu walielezewa majukumu yao mbalimbali ikiwa ni pamoja na majukumu ya TASAF Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Bw. Donatus Weggina aliwafahamisha Viongozi wa TASAF na wataalam kutoka Simiyu kuwa kama Mkoa tutazingatia taratibu zote, tutahakikisha taarifa za kila robo mwaka zinatolewa kwa wakati na kwa usahihi .Aliwaasa viongozi wanapokwenda kwenye utekelezaji wawe na ushirikiano na umoja.

 Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Kayombo aliushukuru uongozi wa TASAF na hasa Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia mkoa wa Simiyu kuwa miongoni mwa mikoa mitano itakayonifaika na (TPRP IV) na kupokea kiasi cha takribani Tsh. 24.3bln zitakazotumika kwa kipindi cha mika mitano. Bi.Kayombo aliipongeza TASAF kwa kuongeza posho ya watenda kazi kuanzia Tsh. 2500/= hadi Tsh.3000/= kwa siku.Aidha Katibu Tawala huyo aliwapongeza watoa mada kwa kuwasilisha mada nzuri.Aliwaahidi TASAF kuwa, akiwa mtemndaji mkuu atahakikisha kuwa fedha na miradi inatakelezwa , inasimamiwa na kukamilishwa ipasavyo.#

Mwisho.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF -Bw.Ladislaus Mwamanga akizungungunza wakati wa kikao  kikao kazi cha kuzindua Utekelezaji wa awamu ya Nne ya Mradi wa Kupunguza Umaskini Tanzania (TPRPIV)


Picha ya pamoja ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na TASAF



Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo, akizungumza na Viongozi na wadau mbalimbali waliohudhuria  kikao kazi cha kuzindua Utekelezaji wa awamu ya Nne ya Mradi wa Kupunguza Umaskini Tanzania (TPRP IV),katika ukumbi wa Bariadi Conference- Bariadi Simiyu.




Baadhi ya Wadau walioshiriki  kikao kazi cha kuzindua Utekelezaji wa awamu ya Nne ya Mradi wa Kupunguza Umaskini Tanzania (TPRP IV)

Wednesday, July 14, 2021

MKUU WA MKOA AELEKEZA WATENDAJI KUPIMWA KWA MIKATABA AIDHA CHMT ITAKAYOSHINDWA KUSIMAMIA AFYA KUVUNJWA

Ku


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na Wadau wa Sekta ya afya 


 

Katibu Tawala Bi. Prisca Kayombo akiwatambulisha Viongozi Mbalimbali waliofuatana na mkuu wa mkoa 

                                        


                                        Wadau wa sekta ya afya wakijiandaa na kikao kazi








Wadau wakisikiliza mada wakati wa Kikao kazi

Kufuatia taarifa ya tathimini kuonesha usimamizi duni sekta ya Afya, RC Kafulila amelekeza kuandaliwa mikataba ya usimamizi kati ya RMO na DMOs,  RAS na DEDs na yeye mwenyewe RCs a DCs ili kuhakikisha wilaya na halmashauri zinasimamia sekta ya afya kikamilifu.  

Maelekezo hayo ameyatoa kufuatia tathimini ya usimamizi wa sekta ya afya kuonyesha kuwa kwa muda mrefu usimamizi wa Kamati za Afya Wilaya ( CHMT) ni dhaifu,  wakurugenzi na wakuu wa wilaya hawajawa na msukumo wa kutosha kuhakikisha usimamizi.

Aidha Mhe. Kafulila ameagiza KUVUNJWA kwa Kamati za usimamizi wa huduma ya Afya (CHMT)  itakayoshindwa kusimamia sekta ya afya katika halmashauri husika.  Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo kufuatia taarifa ya tathimini ya robo mwaka kuonyesha kuwa CHMT zote mkoani Simiyu kwa kipindi kirefu  zimekuwa na usimamizi dhaifu hata kusababisha vifo kizembe. 

Katika tathimini hiyo  Bariadi DC ilipata alama C, Busega D, Bariadi mji C, Meatu E , Maswa F huku Itilima ikipata F. Mhe.Kafulila ameelekeza kuwa katika taarifa ya oOktoba, halmashauri itakayopata chini ya alama B, basi CHMT husika itavunjwa na  wengine kuchukuliwa hatua za kiutumishi.

Mwisho

TANZANIA INAJENGA SGR KWA GHARAMA NAFUU- KAFULILA.

 


 Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo wakati wa kikao na Waandishi wa habari.


 
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Simyu wakiwa katia mkutano na waandishi wa Habari.

Kuanzia kulia Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Kayombo, Mkuu wa Mkoa Mhe. David Kafulila na Meneja Mradi  Ujenzi wa reli ya kisasa Mwanza- Isaka Eng. Machibya Masanja wakiwa katika kikao na waandishi wa habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.


Hayo ameleza jana RC KAFULILA wakati akifungua kampeni ya kuhamasisha uelewa wa wananchi kuhusu mradi wa SGR kipande cha Mwanza - Isaka( 341km), kitakachojengwa kwa gharama ya Tsh.3trn sawa na $1.3bn. 


Mhe.Kafulila amempongeza Rais kwa kuendeleza ujenzi huo kwa kasi zaidi na kusema kuwa gharama hii ni nafuu kulinganisha na Kenya na hata Ethiopia na hivyo inathibitisha usimamizi madhubuti wa fedha za Serikali.

 " Hii inazidi kuthibitisha ripoti ya jukwaa la kimataifa kuhusu uchumi- World Economic Forum 2019 kuonesha kwamba Tanzania ni nchi ya 29 katika nchi 186 duniani katika usimamizi thabiti wa matumizi ya fedha za umma".

 Mhe.Kafulila amesisitiza wananchi kujitokeza kwenye kampeni hiyo iliyoanza jana na itakamalizika  alhamisi ili kupata uelewa zaidi wa mradi. Amewahakikishia fidia kulipwa kwa mujibu wa sheria na zaidi kuwaomba wachangamkie fursa za biashara wakati wa ujenzi hususan eneo la Malampaka ambapo kambi kubwa ya ujenzi zinajengwa. Amesisitiza Shirika la reli kutoa upendeleo kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Simiyu kwa kazi ambazo zipo ndani ya uwezo.

Mwisho
Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!