Na
Stella Kalinga
Benki ya maendeleo ya
TIB imesema iko tayari kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha
kutengeneza bidhaa za hospitali zitokanazo
na zao la pamba mkoani Simiyu.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi Mkuu wa TIB Bw.Charles Singili katika kikao maalum kilichofanyika
jijini Dar es Salaam, kati ya uongozi wa Benki hiyo na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Simiyu ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka.
Singili amesema hakuna
haja kwa Bohari ya Dawa hapa nchini (MSD) kutumia fedha nyingi kuagiza bidhaa za
hospitali kama bandeji, mashuka, pamba za kusafishia na kufungia vidonda kutoka
nje ya nchi wakati Mkoa wa Simiyu unaongoza kwa uzalishaji wa pamba hapa nchini.
Aidha, Singili amesema
benki hiyo iko tayari kutoa mkopo kwa Halmashauri ya Wilaya Maswa kwa ajili ya
kujenga kiwanda kikubwa cha chaki ili kukiwezesha kiwanda kuongeza uzalishaji
utakaokidhi mahitaji.
“Benki iko tayari
kusaidia wasilisheni andiko la mradi tulipitie na kuona namna ya kuwawezesha kupata
mkopo wa kujenga kiwanda; mtakapojenga kiwanda kikubwa mtaisaidia serikali
kupunguza gharama za usafirishaji wa chaki kutoka nje” alisema Singili.
Sambamba na hilo
Singili amesema Benki ya TIB kwa kushirikiana na wadau wengine kama NHIF, NEMC,
TBS,TIRDO,TFDA pamoja na kusaidia ujenzi wa kwanda cha kutengeneza bidhaa za
Hospitali zitokanazo na Pamba, pia watasaidia ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza
maji ya kuwawekea wagonjwa( drip) mkoani Simiyu.
Kwa upande wao Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa huo wameushukuru
uongozi wa Benki ya TIB kwa kuunga mkono juhudi za Viongozi wa Mkoa huo hususani
katika utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda.
Mkurugenzi Mkuu wa TIB Ndg.Charles Singili akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Mkutano wa Benki hiyo jijini makao makuu Dar es Salaam. |
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Anthony Mtaka (wa pili kushoto) akizungumza na viongozi wa Mkoa huo na viongozi
wa Benki ya TIB katika kikao maalum kilichofanyika ukumbi wa Mkutano wa Benki
hiyo Makao makuu jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment