Na
Stella Kalinga
Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa
huo,Mhe.Anthony Mtaka imetembelea SUMA
JKT jijini Dar es Salaam kuona pampu za
umwagiliaji.
Lengo
la ziara hiyo ni kujionea aina mbalimbali za pampu za umwagililiaji kwa kuwa
Mkoa huo una mpango wa kuanza kutekeleza kilimo cha umwagiliaji wilayani Busega
kama kipaumbele kwa mwaka 2017.
Pamoja
na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa,viongozi wa wilaya ya Busega
na Maswa pia walishiriki ziara hiyo.
|
Mkuu
wa Mafunzo na Ufundi wa SUMA JKT (kulia) akitoa maelezo juu ya pampu ya umwagiliaji
yenye uwezo kusukuma mapipa 13 ya maji kwa dakika kwa Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa
wakati wa ziara yao jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mafunzo na
Ufundi wa SUMA JKT (kulia) akitoa maelezo juu ya pampu ya umwagiliaji yenye
uwezo kusukuma mapipa 13 ya maji kwa dakika kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka (kulia) na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wakati wa ziara
yao jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa, Viongozi na baadhi ya Watalaam wa Wilaya ya Busega na Maswa na Wataalam
wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu katika
picha ya pamoja walipotembelea SUMA JKT jijini Dar es Salaam.
|
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDelete