Na Stella Kalinga
Wakulima nchini wametakiwa
kufanya maamuzi magumu yatakayoleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kulima
kilimo HAI (kilimo kisichotumia kemikali za viwandani) kinachozingatia kanuni bora kwa kuwa
kimeonyesha tija katika kuongeza thamani ya mazao.
Wito huo umetolewa na Waziri wa
Biashara,Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi
Amina Salum Ali alipotembelea Kampuni ya Biore wilayani Meatu katika ziara yake
ya kutembelea viwanda vidogo na vya kati mkoani Simiyu.
Mhe. Balozi Amina Salum Ali amesema upo
umuhimu sasa kwa viongozi wa serikali kuhakikisha wanafanya maamuzi magumu
yatakayoboresha uchumi wa watanzania ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo sahihi
ya kuzingatia kilimo HAI (oganiki) kinachofuata
kanuni bora za kilimo pasipo kuchanganya
na masuala ya kisiasa.
“Biashara ya sasa hivi inaelekea zaidi
katika masuala mazima ya oganiki na ukiangalia kuna tofauti kubwa sana ya bei katika
vitu vya oganiki na ambavyo siyo oganiki, kwa mfano Karafuu ya tunayoiuza
ambayo siyo oganiki inauzwa shilingi 8100 na ambayo ni oganiki inauzwa 9900 kwa
hiyo chochote ambacho ni oganiki unapata bei nzuri; watu wengi wanakimbia
kulima kilimo hai kwa sababu ya hutumia nguvu zaidi katika usafi, ulimaji ,ukaushaji wake ambao unazingatia
viwango, lakini manufaa yake ni makubwa sana” amesema Balozi Amina Salum Ali.
Ameongeza Zanzibar imeingia katika hatua
nyingine ambapo imedhamiria kuanzisha viwanda vitakavyotumia malighafi ambayo
ni oganiki(hai) ambapo wanataka kulima maua, viungo na mazao mengine ambayo yatauzwa
ndani na nje ya nchi, hivyo wako tayari kuwekeza mkoani Simiyu hususani katika
ardhi ya kuzalisha mazao hayo.
Aidha Waziri huyo wa Zanzibar
akizungumzia umuhimu wa biashara ya ndani ya nchi amesema takwimu zinaonyesha kuwa
mataifa mengi ya Afrika yanafanya biashara ya ndani chini ya asilimia 27 na
akasisitiza uboreshaji wa mifumo ya uendeshaji wa biashara na mnyororo wa thamani ili Tanzania iweze kufikia
uchumi wa kati.
Kwa upande wake mmoja wa wawekezaji
anayetekeleza kilimo HAI (kisichotumia madawa na kemikali za
viwandani) kwa zao la pamba Mkurugenzi wa Kampuni ya Biore Tanzania Niranjan
Pattni amekiri kuwepo kwa tija kubwa
zaidi endapo wakulima wataingia katika mfumo wa kilimo HAI , ambapo
Kampuni yake imekuwa ikitoa elimu ya kilimo na utunzaji wa mazao, mikopo ya
gharama nafuu, pembejeo bora za kilimo na kuwahakikishia soko la uhakika na nyongeza
ya bei.
Naye Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony
Mtaka amesema ili kilimo kiweze kufikia kuwa eneo la kutegemewa kwenye
malighafi katika Tanzania ya Viwanda, ni
lazima wananchi waende kwenye kilimo cha kisasa ambacho kinahitaji gharama ya
mbegu bora, mbolea na pembejeo nyingine bora za kilimo.
“Sisi kama mkoa tunajipanga kuwa mkoa
utakaozalisha bidhaa za afya zitokanazo na pamba na bidhaa hizi zinahitaji
pamba iliyoandaliwa vizuri na mfano ni pamba ya Biore, kama ukitaka kupata eneo
ambalo unaweza kujifunza pamba tutakayoihitaji kuzalisha kama malighafi ya
bidhaa za kiwanda cha bidhaa za afya ni pamba ya Biore ambayo ni oganiki na ina
gharama kubwa hata kwenye soko la Dunia” amesema Mtaka.
Mheshimiwa Balozi Amina Salum Ally
amemaliza ziara yake wilayani Meatu na anatarajia kukamilisha ziara yake Mkoani
Simiyu na kufanya majumuisho wilayani Busega, ambapo akiwa Wilayani Meatu ametembelea
na kuona kiwanda cha kusindika maziwa, ng’ombe wa kisasa wa maziwa, mashamba ya
malisho ya mifugo na kukutana na mwekezaji wa kampuni ya Biore Tanzania
anayejishughulisha na kilimo cha pamba ya oganiki(pamba hai).
ReplyDeleteHello.
Mimi ni Mr Rahel binafsi wakopeshaji mkopo ambao hutoa maisha wakati nafasi ya mkopo kwa watu binafsi, makampuni ya biashara, bima, nk Je, katika shida yoyote ya kifedha au katika haja ya mkopo wa kuwekeza au unahitaji mkopo kulipa bili yako kutafuta hakuna zaidi kama sisi ni hapa kufanya matatizo yako yote ya kifedha kitu cha zamani. Sisi kutoa kila aina ya mkopo katika dhehebu lolote fedha kwa kiwango cha 2% bila fee.I upfront wanataka kutumia kati hii kubwa ya kukufahamisha kwamba tuko tayari kukusaidia kwa aina yoyote ya mkopo kutatua kwamba tatizo.Kama yako ya kifedha ndiyo basi kupata nyuma sasa kupitia barua pepe (rahelcohranloan@gmail.com) kwa maelezo zaidi, wewe ni sana makala.