Na
Stella Kalinga
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemuagiza Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Prof.Makame Mbarawa kuhakikisha zabuni ya ujenzi wa kipande cha
barabara ya Bariadi hadi Maswa yenye urefu kilomita 49.2 kutangazwa ndani ya
wiki moja kuanzia leo(11 Januari,2017).
Rais Magufuli ametoa
agizo hilo leo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Bariadi mkoani Simiyu
katika uwanja wa Shule ya Msingi Somanda, mara baada ya kufungua barabara ya kutoka
Lamadi hadi Bariadi yanye urefu wa kilomita 71.8 akiwa katika ziara ya siku
mbili mkoani Simiyu.
Mhe.Magufuli amesema Barabara
ya Lamadi-Bariadi imekamilika kwa kutumia fedha za Serikali na kwa upande wa
Barabara ya Maswa –Mwigumbi mkandarasi anaendela na kazi hivyo zabuni ya
kipande kilichobakia cha Braidi Maswa itangazwe ili barabara ya lami kutoa
Lamadi hadi Mwigumbi (Shinyanga) ikamilike kwa lengo la kurahisisha uchukuzi.
Aidha, Mhe.Rais Magufuli
amesema endapo kutakuwa na barabara ya lami kutoka Lamadi(Busega) hadi Mwigumbi(Shinyanga)
kutapunguza umbali wa kilomita zaidi ya 100 kwa watu watakakuwa wakisafiri
kutoka Nairobi kwa kupitia Lamadi-Bariadi-Maswa-Mwigumbi ambao kwa sasa
wanazunguka kupitia Mkoa wa Mwanza.
Mhe.Rais Magufuli
ameongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza wigo wa biashara kwa
mkoa wa Simiyu hivyo akawataka wananchi wa Simiyu kutunza
barabara hiyo iliyokamilika(kipande chaLamadi-Bariadi) kwa kuacha kung’oa alama
za barabarani.
Serikali imetimiza
wajibu wake kwa kuwajengea barabara kwa fedha zake ili ninyi watu wa Simiyu
mpata barabara, wajibu wenu ni kuitunza na muitunze kweli kweli”
Kwa upande wake Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ametoa wito kwa madereva kuacha kumwaga mafuta
barabarani ili kuifanya barabara hiyo idumu na kuwa na uhai mrefu.
Hta hivyo Rais Magufuli
ameupongeza uongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa kusimamia na
kuhakikisha barabara ya Lamadi-Bariadi inakamilika ambapo amesema TANROADS
imekuwa ikitekeleza majukumu yake vizuri hai iliyoifanya kushika nafasi ya tatu
katika Bara la Afrika ikiongozwa na Wakala wa Barabara wa Afika Kusini na Namibia
kwa kufanya kazi zenye ubora.
Wakati huo huo Rais
Magufuli amempongeza Mkuu wa mkoa wa Simiyu kwa kuanza kutekelza sera ya
Tanzania kwa vitendo kwa kuanziisha kiwanda cha kutengeneza chaki (Maswa), Kiwanda
cha kusindika maziwa ( Meatu) jambo ambalo linasaidia katika kutoa ajira kwa
watanzania; akawataka wakuu wa mikoa wengine kuiga mfano huo.
Rais Magufuli yupo katika ziara ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo leo amepata fursa ya kuzungumza na wananchi wa wilaya ya Busega na Bariadi pamoja na kuweka Jiwe la Msingi katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu na kufungua barabara ya Lamadi-Bariadi yenye urefu wa Kilomita 71.8.
Rais Magufuli yupo katika ziara ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo leo amepata fursa ya kuzungumza na wananchi wa wilaya ya Busega na Bariadi pamoja na kuweka Jiwe la Msingi katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu na kufungua barabara ya Lamadi-Bariadi yenye urefu wa Kilomita 71.8.
0 comments:
Post a Comment