Na
Stella Kalinga
Mbunge wa viti Maalum
kupitia CCM Mkoa wa Simiyu,Mhe.Leah Komanya amekabidhi vyombo kwa ajili ya
kupikia chakula cha Mchana katika shule za Msingi na Sekondari za Kutwa za
Serikali Mkoani humo.
Makabidhiano hayo
yameanyika jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na kushuhudiwa na
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Mkoa, Maafisa Elimu, Waratibu wa Elimu Kata,Wakuu
wa Shule na Walimu wakuu pamoja na Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) mkoa wa
Simiyu.
Mhe.Komanya amekabidhi
vyombo hivyo ili kutimiza ahadi yake aliyoitoa katika kikao cha Kamati ya
Sherehe ya Mkoa mwishoni mwa mwezi Septemba, 2016 ya kuwasaidia wanafunzi kupata chakula shuleni
kusoma na muda waliokuwa wanakwenda kutafuta chakula wautumie kwa ajili ya
masomo.
Aidha,
Mhe.Komanya amewaomba wadau wengine wa maendeleo kumuunga mkono katika
kuchangia mahitaji mengine ya watoto yatakayowasaidia kupata chakula cha mchana.
Akizungumza
kwa niaba ya Serikali ya Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka amemshukuru
Mhe.Komanya kwa mchango wake huo ambao utakuwa msaada mkubwa katika maendeleo
ya wanafunzi kitaaluma.
Aidha,Mhe.Mtaka
amesema baada ya vikundi vya vijana kuanzisha miradi ya Usindikaji maziwa Meatu
na utengenezaji wa Chaki Maswa wakishirikiana na Serikali anatamani kuwaona
wanawake wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM-UWT Mkoa wa Simiyu kutambua fursa
zilizopo katika mkoa wao na kuanzisha miradi ya maendeleo.
Sambamba
na hilo Mhe.Mtaka ameitaka Jumuiya hiyo kuanzisha miradi itakayojibu kero na
matatizo ya jamii hususani wanawake ili wanawake na wasichana wenye matatizo
wakimbilie kupata suluhu katika jumuiya badala ya kukaa na kusubiri shughuli za
uchaguzi mkuu.
“Natamani
kuiona UWT yenye maono na kubuni miradi itakayojibu kero za watu wanaowazunguka;
natamani kuona mwanamke akipata tatizo aone msaada kutoka UWT na akimbilie UWT
badala ya kutegemea taasisi za kijamii pekee” amesema Mtaka.
Wakati
huo huo Mtaka amewataka wanawake wa jumuiya hiyo na wanawake wengine kuwahamasisha watoto
kwenda shue kwa kuwa watakapokula shuleni mchana watakuwa na uhakika wa kusoma
vizuri na kufanya vizuri kitaaluma.
Mbunge
Leah Komanya ametoa jumla ya sufuria 100 zenye ujazo wa lita 55 kwa kila moja ambazo
zote zina thamani ya shilingi 5,000,000/=
0 comments:
Post a Comment