Na
Stella Kalinga
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli anatarajia kufanya ziara ya
siku mbili Mkoani Simiyu, kuanzia tarehe
11/01/2017 hadi tarehe 12/01/2017.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari ofisini kwake leo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka amesema, Tarehe
11/01/2017 Rais Magufuli ataweka jiwe la Msingi katika Hospitali ya Mkoa wa
Simiyu katika Mtaa wa Nyaumata Halmashauri ya Mji wa Bariadi na kufungua
barabara ya Lamadi-Bariadi.
Mtaka amesema baada ya
kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Mkoa na kufungua barabara ya Lamadi–Bariadi
Mhe. Rais atazungumza na wananchi wa
Bariadi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda, mahali lilipo jiwe la
ufunguzi wa barabara hiyo.
Aidha, Mtaka ameongeza
kuwa Siku ya tarehe 12/01/2017 Mhe.Rais atatembelea kiwanda cha kutengeneza
Chaki kilichopo Wilayani Maswa na baadaye ataweka jiwe la msingi katika
barabara ya Mwigumbi-Maswa ambapo pia atazungumza na wananchi wa Wilaya ya
Maswa.
“Kwa
niaba ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu,napenda kuwaalika wananchi wote wa mkoa
wetu kujitokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli katika maeneo yote atakayopita” amesema Mtaka.
0 comments:
Post a Comment