Na Stella Kalinga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
ameendelea kusisitiza kuwa Serikali yake ya awamu ya tano haitatoa chakula cha
msaada kwa wananchi.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipozungumza na wananchi wa Nyashimo,
Masanzakona, Lamadi, pamoja na Nyamikoma wilayani Busega na Somanda Bariadi
Mjini Mkoani Simiyu kwa nyakati tofauti, wakati wa ziara yake ya
siku mbili Mkoani humo.
Aidha, Rais Magufuli amesema kutokana na maeneo mengi nchini kutopata mvua
za kutosha, wananchi walime mazao yanayostahimili ukame na yale yanayokomaa
ndani ya muda mfupi kama vile mtama,uwele,ulezi
na viazi.
Ameongeza kuwa serikali haiwezi kutoa chakula cha msaada kwa
watanzania zaidi ya Milioni 50 nchi nzima, badala yake itaboresha miundombinu ikiwemo
barabara pamoja na huduma za jamii kama
vile elimu, afya,maji na umeme.
“Nasema sitaleta chakula, nataka Watanzania wafanye kazi, nimeona niwaeleze
ukweli ili mnielewe, maana msema kweli ni mpenzi wa Mungu, najua wapo wanasiasa
watawaambia kuwa watawaletea chakula, hakuna chakula fanyeni kazi” amesema Rais
Magufuli.
Aidha,Mhe.Rais amewataka wakazi wa wilaya ya Busega hususani wale walio
pembezoni mwa Ziwa Victoria kujipanga kutekeleza mpango wa kilimo cha
umwagiliaji ambao umeanzishwa na Viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Busega, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe.Anthony Mtaka na akaahidi kuwa Serikali itawasaidia katika miundombinu ya
umwagiliaji.
Akizungumzia gharama za ujenzi wa Hospitali ya mkoa wa Simiyu mara baada ya
kuweka jiwe la msingi la hospitali hiyo, Rais Magufuli ameugiza uongozi wa Mkoa
wa Simiyu, Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi, Wakala wa Majengo (TBA) kukaa
na kurejea upya gharama za ujenzi wa Hospitali hiyo ya shilingi bilioni 46 kwa
kuwa haiendani na hali halisi ya jengo litakalojengwa.
“Haiwezekani majengo ishirini yenye ghorofa nne kila moja ya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam kujengwa kwa shilingi bilioni 10 na jengo hili moja la ghorofa
moja kujengwa kwa shilingi bilioni 46” amesema Mhe.Dkt. Magufuli.
Pia Mhe.Rais ameahidi kutoa jumla ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya
ujenzi wa hospitali hiyo ambayo ameelekeza kuwa ikamilike kabla ya kumalizika
kwa kipindi chake cha uongozi ili wananchi wa Mkoa wa Simiyu wapate huduma za
afya zinazohitajika.
Wakati huo huo Rais Magufuli ameutaka uongozi wa Mkoa wa Simiyu kusimamia
na kuhakikisha ujenzi wa tenki la maji ya Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria(Katika
Mlima Ngasamo) ambao utatekelezwa na Serikali yake unaendelea ili wananchi wa Mkoa
huo kupata maji badala ya kukwama kutokana na Mwekezaji kutaka kuchimba madini
ya Nikeli katika mlima huo
Rais Magufuli amesema hayuko tayari
kuona wananchi zaidi ya milioni moja na
laki tano wa mkoa wa Simiyu wanakosa huduma muhimu ya maji kutokana na mwekezaji huyo kufanya shughuli
za uchimbaji wa madini hivyo amemtaka Waziri wa Nishati na madini kumfutia
leseni mwekezaji huyo.
Rais Magufuli yupo katika ziara ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo leo amepata
fursa ya kuzungumza na wananchi wa wilaya ya Busega na Bariadi pamoja na kuweka
Jiwe la Msingi katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu na kufungua barabara ya
Lamadi-Bariadi yenye urefu wa Kilomita 71.8.
|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkta John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa
Bariadi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda wakati wa ziara yake ya siku
mbili mkoani Simiyu.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akitoa salamu za Mkoa huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ambaye yuko mkoani humo kwa ziara ya siku
mbili.
Waziri
wa Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi,
Mhe.Prof.Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa Bariadi Mkoani Simiyu kabla
ya kumkaribisha Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kuzungumza na
wananchi hao wakati wa ziaa yake mkoani Simiyu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wananchi wa Masanzakona (hawapo pichani) Wilayani Busega mara baada ya kupokelewa
na Viongozi na wananchi wa mkoa wa Simiyu tayari kwa kuanza ziara ya siku mbili
mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wa mkoa wa
Simiyu akikagua jengo la Hospitali ya Mkoa huo mara baada ya kuweka jiwe la
msingi la hospitali hiyo wakati wa ziara
yake ya siku mbili mkoani Simiyu
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Shule ya
Msingi Somanda,kabla ya kuwahutubia wananchi na kufungua barabara ya
Lamadi-Bariadi wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Waimbaji wa kwaya ya
Kanisa la AICT Bariadi mjini wakiimba wimbo maalum mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli(hayupo pichani) wakati wa
ziara yake mkoani Simiyu.
Wanafunzi kutoka katika
baadhi ya shule za Msingi na Sekondari za Mjini Briadi wakiimba wimbo maalum wa
Mkoa wa Simiyu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John
Pombe Magufuli(hayupo pichani) wakati wa ziara yake mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wa mkoa wa
Simiyu akikagua jengo la Hospitali ya Mkoa huo mara baada ya kuweka jiwe la
msingi la hospitali hiyo wakati wa ziara
yake ya siku mbili mkoani humo, (kushoto) Mkuu wa Mkoa huo ,Mhe.Anthony Mtaka.
Baadhi
ya wananchi wa Bariadi wakimsilikilizaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli alipowahutubia wananchi wa Bariadi katika Uwanja
wa Shule ya Msingi Somanda wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa kata
ya Nyashimo (hawapo pichani) Wilayani Busega mara baada ya kupokelewa na Viongozi
na wananchi wa mkoa wa Simiyu tayari kwa kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo.
: Baadhi ya wananchi wa
kata ya Lamadi wilayani Busega wakimsilikilizaRais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani
Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wakizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe.Andrew Chenge mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu wakati waziara yake mkoani humo.
Baadhi ya viongozi wa
Halmashauri za Mkoa wa Simiyu na Wakala wa Barabara wakimsilikiliza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli alipowahutubia wananchi
wa Bariadi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda wakati wa ziara yake ya
siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akizungumza jambo
na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakiwa katika jukwaa kuu kabla ya kuwahutubia
wananchi wa Bariadi wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Viongozi wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili mkoani
Simiyu katika eneo la Masanzakona wilayani Busega wakati wa ziara yake Mkoani
humo.
Waimbaji wa kwaya ya Walimu
Bariadi mjini wakiimba wimbo maalum mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli(hayupo pichani) wakati wa ziara yake
mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Hospitali ya Mkoa
wa Simiyu mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli(hayupo pichani) wakati wa ziara yake mkoani humo.
Mbunge wa Jimbo la
Bariadi,Mhe.Andrew Chenge (kushoto) akiwasilisha matatizo na changamoto za
wananchi wa jimbo lake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.
John Pombe Magufuli(hayupo pichani) wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, (kulia)
Mkuu wa mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa
Bariadi mara baada ya kuwahutubia katika
Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani
humo.
|
0 comments:
Post a Comment