Na
Stella Kalinga
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli ameagiza kiwanda cha
kutengeneza Chaki kilichopo wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu kuongeza uzalishaji ili kiweze kukidhi
mahitaji ya chaki ya nchi nzima.
Rais Magufuli
ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa mara baada ya kutembelea kiwanda hicho siku ya pili ya Ziara yake Mkoani Simiyu ambapo baadaye ameweka jiwe
la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa kilomita 50.3
ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.
Rais
Magufuli amewapongeza Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Maswa kwa kutekeleza kwa vitendo sera ya Tanzania ya Viwanda na jitihada
walizozifanya katika kuanzisha kiwanda hicho kwa kuwa kimekuwa msaada hasa
katika kuwapatia ajira vijana.
“Kuanzisha
kiwanda hiki mmetengeza ajira na chaki nimezijaribu mimi mwenyewe kuandikia nimeona
ni nzuri kwa sababu hata mimi nilikuwa mwalimu, hongereni sana Maswa kwa kuwa
na kiwanda hiki, hii ndiyo dhamira yetu ya kuwa na viwanda, kiwanda siyo lazima
kiwe na ghorofa ishirini, hata ukiwa na chumba kimoja kinaweza kuwa kiwanda”
alisema Magufuli.
Rais
Magufuli amesema kikijengwa kiwanda kikubwa na
kikaongeza uwezo wa kuzalisha chaki za kutosheleza mahitaji ya nchi
nzima, chaki hizo zitanunuliwa na kutumika nchi nzima kwa kuwa kwa sasa
kinaweza kutosheleza mahitaji ya mikoa 10.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema uwepo wa kiwanda cha chaki
Maswa uwe ni kichocheo cha vijana na wanawake wa wilaya na mkoa wake kwa ujumla, kujiunga katika vikundi kubuni miradi ya maendeleo, ili Serikali iwawezeshe
kupata mikopo kwa ajili ya mitaji kwa kuwa hata kiwanda hicho kilianzishwa na kikundi
cha vijana ambao wanashirikiana na Halmashauri ya Wilaya kwa sasa.
Wakati
huo huo Rais Magufuli amewataka wananchi wa Wilaya ya Maswa na mkoa wa Simiyu
kwa ujumla kuitimia vizuri barabara ya Maswa-Mwigumbi ambayo ameiwekea jiwe la
msingi leo pindi itakapokamilika, kwa lengo la kujiletea maendeleo ikiwa ni
pamoja na kufanya biashara mbalimbali, kwa kuwa itarahisisha usafirishaji wa
watu na bidhaa pia.
Kwa
upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Prof.Makame
Mbarawa amewataka wakandarasi na
wahandisi washauri wanaojenga barabara hiyo kuhakikisha wanaijenga kwa viwango kulingana
na thamani ya fedha zilizotolewa na kuimaliza kwa muda uliopangwa.
Aidha,
Waziri Mbarawa amewataka wasimamizi wa barabara hiyo kwa viwango vilivyopo katika mkataba vinginevyo hawatapewa
kazi tena hapa nchini.
Sambamba
na hilo Mhe.Rais aliahidi kutatua kero za wananchi wa Wilaya ya Maswa zilizowasilishwa
na Wabunge wote (Maswa Mashariki na Maswa Magharibi) moja baada ya nyingine
kulingana hali itakavyoruhusu ikiwepo tatizo la maji, ambapo aliwahaakikishia kuwa mwaka fedha zimetengwa
jumla ya shilingi bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa chujio la maji
katika Bwawa la Sola(Zanzui)
Vile vile Mhe.Rais amewataka viongozi wa serikali kutowapangia bei ya mazao wakulima na badala yake wawaache wajipangie wenyewe, ambapo amewataka kuuza mazao yao katika bei itakayowanufaisha huku wakitunza akiba wa ajili chakula chao.
Vile vile Mhe.Rais amewataka viongozi wa serikali kutowapangia bei ya mazao wakulima na badala yake wawaache wajipangie wenyewe, ambapo amewataka kuuza mazao yao katika bei itakayowanufaisha huku wakitunza akiba wa ajili chakula chao.
Mhe.Rais
Magufuli amekamilisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo ameweka
jiwe la msingi katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu, kufungua barabara ya Lamadi-Bariadi
na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa
kilomita 50.3.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe ikiwa ni
ishara ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi wilayani
Maswa, yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami
wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akiwasalimia mamia ya
wananchi wilayani Maswa katika Viwanja vya Benki ya CRDB Maswa kabla ya kuweka
jiwe la msingi barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha
lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu,( kulia)Mkuu wa
wilaya hiyo,Mhe.Dkt.Seif Shekalghe.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akwahutubia mamia ya
wananchi wilayani Maswa katika Viwanja vya Benki ya CRDB Maswa kabla ya kuweka
jiwe la msingi barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha
lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akizungumza
na mamia ya wananchi wilayani Maswa mara baada ya kutembelea kiwanda cha chaki
na duka la maziwa ya Meatu kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara yenye
urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati
akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akionesha maziwa ya
Meatu kwa mamia ya wananchi wa Maswa mara
baada ya kutembelea kiwanda cha chaki na duka la maziwa ya Meatu kabla ya
kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo
itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili
mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa
Simiyu akitoa Salamu za Mkoa huo na kutambulisha wageni ngazi ya Kimkoa na
Kitaifa wakati wa ziara ya Mhe.Rais wilayani Maswa , ambaye aliweka jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye
urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati
akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Wilaya ya Maswa Dkt.Seif Shekalaghe akitambulisha
wageni ngazi ya wilaya wakati wa ziara
ya Mhe.Rais wilayani humo , ambaye aliweka jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye
urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati
akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu
Waziri
wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Prof.Makame Mbarawa akizungumza na
wananchi wa Maswa katika uwanja wa Benki ya CRDB kabla ya kumkaribisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, ambaye aliweka jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye
urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati
akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
:Mbunge
wa Maswa Mashariki,Mhe.Stanslaus Nyongo akiwasilisha kro na matataizo ya
Wananchi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph
Magufuli, ambaye aliweka jiwe la msingi la
barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa
kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Waziri wa TAMISEMI wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe.Omary Haji akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa
wakati wa ziara ya kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John
Pombe Joseph Magufuli mkoani Simiyu ambaye aliweka jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye
urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.
Waimbaji wa Kwaya ya Walimu wilaya ya Maswa wakiimba wimbo maalum mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, ambaye aliweka jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu leo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe.Zainab Taleck akipanda mtipamoja na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu kama ishara ya ujirani mwema mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, kuweka jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu leo.
Waimbaji wa Kwaya ya Walimu wilaya ya Maswa wakiimba wimbo maalum mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, ambaye aliweka jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu leo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe.Zainab Taleck akipanda mtipamoja na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu kama ishara ya ujirani mwema mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, kuweka jiwe la msingi la barabara ya Maswa-Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka na baadhi ya wabunge wa mkoa huo wakipanda Mti wa
kumbukumbu katika eneo la jiwe la ufunguzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi mara
baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph
Magufuli kuweka jiwe la msingi la barabara
hiyo yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati
akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka na baadhi ya wabunge wa mkoa huo wakimwagilia Mti wa
kumbukumbu walioupanda katika eneo la jiwe la ufunguzi wa barabara ya
Maswa-Mwigumbi, mara baada Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, kuweka jiwe la msingi la barabara hiyo yenye urefu wa
Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara
yake ya siku mbili mkoani humo leo.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akiwasalimia mamia ya
wananchi wilayani Maswa katika Viwanja vya Benki ya CRDB Maswa, kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara
ya Maswa- Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango
cha lami wakati akihitimisha ziara yakeya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu,Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi
na Mawasiliano na Wakala wa barabara (TANROADS) Simiyu, baada ya kuweka jiwe la
msingi ujenzi wa barabara ya Maswa- Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3
ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku
mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu,Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano na Wakala wa barabara (TANROADS) wa Simiyu na mikoa jirani, baada
ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Maswa- Mwigumbi yenye urefu wa
Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara
yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi
wa barabara ya Maswa- Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa
kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja
na Waziri wa Ujenzi, baadhi ya viongozi
wa Mkoa wa Simiyu na wakandarasi wanaojenga barabra ya Maswa-Mwigumbi baada ya
kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara hiyo, yenye urefu wa Kilomita 50.3
ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami , wakati akihitimisha ziara yake ya siku
mbili mkoani Simiyu.
Baadhi
ya Watumishi wa Wilaya ya Maswa na Madiwani wa Mkoa wa Simiyu wakimsilkiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Maswa
kabla ya kuweka jiwe la msingi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa
kwa kiwango cha lami wakati akihitimisha ziara yakeya siku mbili mkoani Simiyu.
Kikundi cha Ngoma cha
Simba Mchawi cha Wilayani Maswa wakitoa burudani kwa wananchi wa wilaya hiyo kabla
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuweka jiwe
la msingi yenye urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami
wakati akihitimisha ziara yakeya siku mbili mkoani Simiyu.
Baadhi ya Wananchi wa
Wilaya ya Maswa wakimsilkiliza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa
akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Maswa kabla ya kuweka jiwe la msingi yenye
urefu wa Kilomita 50.3 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami wakati
akihitimisha ziara yakeya siku mbili mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment