Na
Stella Kalinga
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
amesema Serikali itaandaa mpango na utaratibu wa kuwawezesha wafanyabiashara wa
kata ya Lamadi kufanya biashara zao kwa saa ishirini na nne.
Mtaka ameyasema hayo
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Lamadi wilayani Busega kwa lengo
la kuhamasisha mpango wa Kilimo cha Umwagiliaji pamoja na kisikiliza kero za
Wananchi na kuwapatia ufumbuzi wakati wa ziara yake wilayani humo.
Mtaka amesema Lamadi ni
Kituo(centre) kikubwa cha biashara mkoani Simiyu ambacho watu kutoka mikoa na
nchi mbalimbali wamekuwa wakipita hapo, hivyo ipo haja ya kukifanya kituo
kikubwa zaidi kwa kukiwezesha kufanya kazi muda wote ili kuongeza kasi ya
ukusanyaji wa kodi na ushuru na kuinua uchumi wa wananchi,Halmashauri ya Busega
na Mkoa kwa ujumla.
“Watu wanatoka Kenya na
mikoa mingine hapa nchini wakipita hapa saa tatu usiku baa, maduka na biashara
nyingine zote zimefungwa; tunataka mapato ni lazima watu wafanye biashara ili
tuyapate, naona ipo haja ya kuibadilisha Lamadi, tutakaa na wenzetu wa Ulinzi na Usalama tuone
namna nzuri itakayofaa kuwafanya wafanyabiashara wa makundi yote kufanya kazi
muda wote wakiwa na uhakika wa usalama wao na biashara zao.” Alisema Mtaka.
Hata hivyo Mkuu huyo wa
Mkoa amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega kuweka viongozi
sahihi na waadilifu katika Vijiji vya Kata ya Lamadi kwa kuwa ndiyo kata
inayochangia kwa kiasi kikubwa mapato ya Halmashauri yake.
Sanjali na hilo
Mhe.Mkuu wa Mkoa amewataka viongozi wa vijiji na Kata wa wilaya zote mkoani
kwake kuhakikisha wanasoma taarifa ya
mapato na matumizi kwa wananchi kwa mujibu wa sheria na taratibu.
Wakati huo huo Mtaka
amewahamasisha mpango wa kilimo cha umwagiliaji wilayani Busega ambao
ameutambulisha kama kipaumbele cha mwaka 2017 kwa kuwashauri wajiorodheshe kwa
viongozi wao wa vijiji na kujiunga katika vikundi ili watambuliwe na kuwezeshwa
kwa pembejeo na miundombinu ya umwagiliaji.
Mtaka amesema Serikali
iko tayari kuwasaidia wananchi hivyo watekeleze wajibu wao wa kulima na
Serikali iko tayari kupeleka maji ili kuwaondoa wananchi wa Busega kwenye aibu
ya kufa njaa wakati wana maji ya kudumu ya Ziwa Victoria.
Naye Chele Nkulima
makaziwa Lamadi amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kuanzisha mpango huo wa kilimo cha
umwagiliaji ambapo alimuomba Mkuu huyo wa Mkoa kuwasaidia wananchi wa Busega
ili mradi huo uwafikie watu wote.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
yuko katika ziara ya siku 6 wilayani Busega ambapo anazungumza na wananchi
kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu mpango wa kilimo cha umwagiliaji na
kujibu kero mbalimbali za wananchiwa wilaya hiyo.
0 comments:
Post a Comment