Sunday, January 29, 2017

WAZIRI WA VIWANDA ,BIASHARA NA MASOKO WA ZANZIBAR AANZA ZIARA YA SIKU TATU MKOANI SIMIYU

Na Stella Kalinga

Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Simiyu.

Mhe.Waziri akiwa mkoani Simiyu atatembelea maeneo mbalimbali yanayogusa wizara yake ikiwa ni pamoja kutembelea viwanda vidogo na vya kati vinavyochakata na kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo malighafi yake inapatikana hapa nchini.

Akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Balozi Amina Salum Ali amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kufanya biashara na wananchi/wafanyabiashara wa Mkoa huo kwa lengo la kuboresha biashara ya ndani ya nchi ikiwa ni njia mojawapo  ya kudumisha Muungano kati ya pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe.Waziri amesema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inataka kufanya biashara ya viungo(spices), mazao ya jamii ya mikunde na mchele, ambapo amewaeleza viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuwa endapo Serikali ya Mkoa huo itaihakikishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar upatikanaji wa bidhaa hizo hakutakuwa na haja ya kuagiza kutoka nje ya nchi.

Ameongeza kuwa biashara ya wenyewe kwa wenyewe itawahakikishia wananchi kupata soko la uhakika hali itakayowawezesha kuinua uchumi wao.

“Biashara hii itafanikiwa ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake na ni lazima kuwe na mkakati wa pamoja utakaoenda sambamba na utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda na itawezekana kufikia Uchumi wa Kati” alisema Mhe. Waziri Amina Salum Ali.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema Mkoa huo uko tayari kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika masuala ya biashara hususani kwenye mazao ya mikunde na viungo ambapo amesema watawahamasisha wananchi kulima mazao hayo kwa kilimo chenye tija(kilimo biashara).

Kuhusu uhakika wa upatikanaji wa mchele Mtaka amesema Mkoa wake ka kushirikiana na wadau wengine ikiwepo Benki ya NMB utaanza kutekeleza mradi wa kilimo cha umwagiliaji wilayani Busega ambao ni kipaumbele cha mkoa kwa mwaka 2017, ambapo wananchi watakuwa na uwezo wa kulima mpunga kwa kutumia maji ya uhakika ya Ziwa Victoria, hivyo kupitia mradi huo wananchi wataweza kuuza mchele Zanzibar.

“ Mhe..Waziri tumeamua kama mkoa kulima kilimo cha umwagiliaji Busega kwa kuwa tuna uhakika wa maji ili wananchi wa wetu walime mpunga, hatuwezi tukawa tunaletewa mchele kutoka nje na nchi ambazo zinatumia maji ya Ziwa victoria na sisi tulionalo hapa tunaliangalia tu, .......Nikuahidi kuwa hatutakuangusha” alisema Mtaka

Mhe.Balozi Amina Salum Ali amefanya ziara hii kutekeleza agizo la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein  aliyoitoa wakati wa Maadhimisho Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere Oktoba  2016,  yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu; ambapo alielekza kuwa
baadhi ya mawaziri wake watakuja kwa ajili ya kujadili namna ya Kujenga urafiki na ushirika kati ya Zanzibar na Mkoa wa Simiyu katika masuala ya sekta mbalimbali ikiwemo elimu, kilimo na viwanda.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali(wa tatu kushoto) akiangalia chaki zilizotengenezwa na vijana wa Maswa Family mara baada ya kutembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.

Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali(mwenye ushungi ) akiangalia namna chaki zinavyotengenezwa na vijana wa Maswa Family mara baada ya kutembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali(mwenye ushungi) akipewa maelezo mafupi juu ya utengenezaji wa chaki na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko (wa pili kushoto) mara baada ya kutembelea kiwanda cha Chaki wilayani Maswa wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali(mwenye ushungi rangi ya maziwa (kushoto)) akiangalia mchele ulikobolewa na kupangwa katika madaraja tofauti mara baada ya kutembelea kiwanda cha kukoboa mpunga na kupanga mchele katika madaraja cha N.G.S Company Liimited kilichopo Majahida Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa N.G.S Company Limited, Njalu Silanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu(kulia) akimkabidhi Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali (kushoto) zawadi ya mchele baada ya kutembelea kiwanda chake kilichopo Majahida Mjini Bariadi wakati wa ziara yake mkoani Simiyu
Mkurugenzi wa N.G.S Company Limited, Njalu Silanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu(kulia) akimuonesha Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali (wa pili kushoto) baadhi ya maghala ya kuhifadhia nafaka mara baada ya  kutembelea kiwanda kukoboa mpunga na kupanga mchele katika madaraja (ambacho ni mali ya N.G.S Company Limited ) kilichopo Majahida Mjini Bariadi wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa mtalaam wa kusindika mafuta ya alizeti katika moja ya kiwanda cha kusindika mafuta hayo wilayani Maswa wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa N.G.S Company Limited, Njalu Silanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu(kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali (wa pili kushoto) kabla ya waziri huyo   kutembelea kiwanda kukoboa mpunga na kupanga mchele katika madaraja (ambacho ni mali ya N.G.S Company Limited ) wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.
Mkulima wa Kijiji cha Senani , Bw. Lupande Nila wilayani Maswa akimwelezea Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali juu ya zana za kisasa za kilimo alizotengeneza kwa kushirikiana na wenzake mara baada ya Waziri huyo kutembelea shamba  lake na kuona zana anazozitumia wakati akiwa katika ziara yake Mkoani Simiyu
Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali akisaini kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kuwasili Mjini Baridi kwa lengo la kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la  Zanzibar, Dkt. Said Seif Mzee akichangia jambo mara baada ya kupata taarifa ya Mkoa wakati wa ziara ya :- Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe.Balozi Amina Salum Ali mkoani Simiyu.






1 comment:


  1. Hello.
    Mimi ni Mr Rahel binafsi wakopeshaji mkopo ambao hutoa maisha wakati nafasi ya mkopo kwa watu binafsi, makampuni ya biashara, bima, nk Je, katika shida yoyote ya kifedha au katika haja ya mkopo wa kuwekeza au unahitaji mkopo kulipa bili yako kutafuta hakuna zaidi kama sisi ni hapa kufanya matatizo yako yote ya kifedha kitu cha zamani. Sisi kutoa kila aina ya mkopo katika dhehebu lolote fedha kwa kiwango cha 2% bila fee.I upfront wanataka kutumia kati hii kubwa ya kukufahamisha kwamba tuko tayari kukusaidia kwa aina yoyote ya mkopo kutatua kwamba tatizo.Kama yako ya kifedha ndiyo basi kupata nyuma sasa kupitia barua pepe (rahelcohranloan@gmail.com) kwa maelezo zaidi, wewe ni sana makala.

    ReplyDelete

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!