Na
Stella Kalinga
Mwenyekiti wa Baraza la
Uwezeshaji wananchi Kiuchumi ,Ndg. John
Jingu amesema Mkoa wa Simiyu umeonesha mfano wa namna viongozi wanavyoweza
kutumia nafasi zao katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Jingu ameyasema hayo
leo katika kikao maalum kilichofanyika kati ya Uongozi wa Baraza hilo na
Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika Ofisi za Baraza hilo jijini Dar es Salaam.
Jingu amempongeza Mkuu
wa mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka na viongozi wenzake kwa kutambua dhamira ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo na
kuitekeleza kwa vitendo.
“Tunaona namna mnavyofanya
kazi na mnatembea kwenye maneno yenu, mmefanikiwa kuanzisha viwanda sasa hivi
mnajipanga na kilimo cha umwagiliaji; mimi niseme tu kwamba tumepata mahali pa
kujifunza na tutawashauri watu wengine waje wajifunze Simiyu” alisema Jingu.
Akizungumza katika
kikao hicho Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo
imedhamiria kuzalisha mazao yote ambayo
malighafi yake inapatikana hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuyaongezea thamani
mazao yote yatokanayo na kilimo na mifugo.
Mtaka amesema wao kama mkoa
wameanzisha mfumo wa kuendesha miradi mbalimbali kwa Ubia kati ya Sekta Binafsi
na Serikali (PPP) ambapo katika miradi ya Kiwanda cha Chaki na Kiwanda cha
maziwa ambayo imeanza kutekelezwa mkoani humo, Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na Meatu
wamekuwa wakiendesha miradi hiyo kwa ubia na vikundi vya vijana.
“Tunataka ‘kutransform’
mkoa wetu ambao utakuwa ‘model’ katika kutekeleza dhamira ya Mhe.Rais, dhamira yangu
na wenzangu ni kufanya kitu cha tofauti na tutafanya kwa kuwa tumeamua” alisema
Mtaka.
Aidha , Mtaka ametoa
wito kwa viongozi wa Baraza la Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi kuwasaidia
wananchi katika kufikia azma ya kuwa na Tanzania yenye uchumi wa kati.
Kwa upande wake Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini ameomba Baraza la Uwezeshaji la Taifa
kushirikiana na Viongozi wa mkoa wa Simiyu kuwasaidia wananchi katika masuala
mbalimbali ya kiuchumi ili kuleta matokeo chanya.
Wakati huo huo Afisa
Kilimo wa Wilaya ya Busega Ndg.Juma Chacha ameomba Baraza la Uwezeshaji kupitia
programu yake ya mfuko wa pembejeo za kilimo, lishirikiane na Mkoa wa Simiyu kuwahakikishia
wananchi uhakika wa pembejeo za kilimo ili kuwasaidia kuongeza uzalishaji.
Naye Katibu Mtendaji wa
Baraza hilo, Bengi Issa amesema Baraza limekuwa likifanya kazi na makundi
mbalimbali ya watu katika jamii kwa kuwashirikisha kujenga na kuendeleza
uchumi,kuwepo kwa mazingira rafiki katika ufanyaji biashara,kupatikana kwa
mitaji ya gharama nafuu, kuhimiza uwepo wa bidhaa bora na masoko,kuimarisha
vyama vya ushirika na vikundi vya kiuchumi, kuhimiza matumizi bora ya ardhi na
kuwahamasisha kushiriki katika masuala ya ubinafishaji ikiwa ni pamoja na
ununuzi wa hisa za makampuni kupitia masoko ya hisa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akizungumza katika kikao kilichofanyika kati ya viongozi wa mkoa huo na Viongozi wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichofanyika jijini Dar es salaam |
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi akizungumza katika kikao kilichofanyika kati ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na Viongozi wa Baraza hilo kilichofanyika jijini Dar es salaam |
ReplyDeleteHello.
Mimi ni Mr Rahel binafsi wakopeshaji mkopo ambao hutoa maisha wakati nafasi ya mkopo kwa watu binafsi, makampuni ya biashara, bima, nk Je, katika shida yoyote ya kifedha au katika haja ya mkopo wa kuwekeza au unahitaji mkopo kulipa bili yako kutafuta hakuna zaidi kama sisi ni hapa kufanya matatizo yako yote ya kifedha kitu cha zamani. Sisi kutoa kila aina ya mkopo katika dhehebu lolote fedha kwa kiwango cha 2% bila fee.I upfront wanataka kutumia kati hii kubwa ya kukufahamisha kwamba tuko tayari kukusaidia kwa aina yoyote ya mkopo kutatua kwamba tatizo.Kama yako ya kifedha ndiyo basi kupata nyuma sasa kupitia barua pepe (rahelcohranloan@gmail.com) kwa maelezo zaidi, wewe ni sana makala.