Monday, February 26, 2018

IGP SIRRO AWAONYA WANAOTAKA KUANDAMANA

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewaonya baadhi ya watu wanaohamasishana kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kufanya maandamano bila kufuata utaratibu uliopo na kwamba kitendo hicho ni kinyume cha sheria.


IGP Sirro amesema hayo leo Februari 26 Mjini  Bariadi Mkoani Simiyu mara baada ya kuzungumza na Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu wakati wa  ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani humo.

Amesema upo utaratibu wa kufuata maandamano unaoanisha maandamano halali na yasiyo halali akabainisha kuwa maandamano yasiyo halali yanaashiria uvunjifu wa amani na kutenda uhalifu, hivyo ikiwa maandamano yataashiria kutenda uhalifu na kwa kuwa jeshi la polisi lipo kuzuia uhalifu  litahakikisha maandamano hayo hayafanyiki.

“Maandamano ambayo si halali njia yake ni kuyadhibiti na uwezo wa kudhibiti tunao, wananchi wanataka maendeleo hawataki usumbufu wale wanaotaka usumbufu watapambana na Jeshi la polisi;  jambo la msingi nawaeleza wafuate utaratibu watoe taarifa sisi hatuna tatizo lakini wakitaka kufanya kwa vurugu wasije wakailaumu Serikali”  alisema IGP Sirro.

“Naona kwenye mitandao wanasema lakini niwaambie tu kwamba kuvunja sheria ni rahisi lakini madhara yake huwa ni mabaya sana, nawaomba wazazi waendelee kuwapa malezi bora na wawasaidie watoto wao  wasijiingize katika matukio ya kuvunja sheria” alisisitiza

Aidha,  IGP Sirro amewataka askari wa Jeshi la Polisi kote nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kufuata misingi ya sheria na taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanatenda haki kwa wananchi wanaowahudumia.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Jeshi la Polisi Mkoani humo limechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya uhalifu yaliyokuwepo katika miaka kadhaa iliyopita ambayo ni pamoja na mauaji ya watu wenye Ualbino, Vikongwe na ukataji wa mapanga.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati alipokuwa katika Ziara yake ya siku moja Mkoani Simiyu.


Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake ya siku moja Mkoani humo(kulia), Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro akifanya mazoezi ya utayari na  askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia  Mkoa wa Simiyu  wakati alipokuwa katika Ziara yake ya siku moja Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Simiyu, wakati wa Zaira yake mkoani humo, (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Wilya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga.
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, IGP Simon Sirro na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jmanne Sagini wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya IGP Sirro mkoani Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!