Saturday, February 17, 2018

WAZIRI MBARAWA AITAKA TBA KUKAMILISHA MIRADI KWA WAKATI


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amemtaka Wakala wa Majengo  hapa nchini (TBA), kuhakikisha anakamilisha kwa wakati  ujenzi wa miradi mbalimbali anayotekeleza

Waziri Mbarawa ameyasema hayo wakati akikagua Ujenzi wa Hospitali  ya Mkoa, Nyumba za Viongozi wa Mkoa zinazojengwa na Wakala huyo eneo la Nyaumata mjini Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani  Simiyu.

Amesema kuwa TBA ni Taasisi ya Serikali  ambayo imeaminiwa na Serikali kwa kuwa  inafanya kazi vizuri lakini imekuwa ikichelewa kukamilisha miradi inayopewa  tofauti na muda uliowekwa kulingana na mikataba.

“TBA ni Taasisi ya Serikali na katika Serikali hii ya awamu ya tano tumeipa miradi mingi tukiamini kuwa watafanya kazi nzuri zenye ubora na kukamilika kwa wakati, ubora upo lakini tatizo kubwa ni kutomaliza kazi kwa wakati” alisema Waziri Mbarawa.

“TBA mjipange mhakikishe mnamaliza miradi kwa wakati vinginevyo hatutawapa kazi kwa sababu hatuwezi kuwapa fedha za Serikali jengo la mwaka mmoja mnajenga miaka mitano, naamini mkijipanga vizuri uwezo mnao na Serikali inawaamini” alisema Mbarawa.

Naye  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka pia ametoa wito kwa Wakala wa majengo TBA kukamilisha ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Mkoa huo ili viongozi waweze kupata makazi .

Wakati huo huo Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amesema kuwa ameshalipa fedha kwa TBA ili waweze kukamilisha ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Mkoa na wameahidi  kukabidhi nyumba hizo mwezi Mei mwaka huu.

Awali akitoa maelezo ya Miradi inayotekelezwa na TBA mkoani Simiyu, Meneja wa TBA mkoani humo Mhandisi.Likimaitare Naunga  amesema wanashindwa kukamilisha baadhi ya miradi kwa wakati kutokana na kucheleweshewa fedha. 
 Meneja wa Wakala wa Majengo nchini(TBA) Mkoa wa Simiyu.Mhandisi.Likimaitare Naunga(katikati) akitoa maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Mkoa huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alipotembelea mradi huo wakati wa ziara yake Mkoani humo. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa TBA Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Likimaitare Naunga(kulia) wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa Mkoa huo unaotekelezwa na TBA wakati wa ziara yake Mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akitoa maelezo juu ya miradi yake inayotekelezwa na TBA kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame Mbarawa alifanya ziara mkoani humo. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof.Makame Mbarawa(mwenye kofia) na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakielekea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Katibu Tawala Mkoa ili aweze kukagua mradi huo wakati wa ziara yake Mkoani humo.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!