Mkuu
wa Jeshi la Polisi hapa nchini IGP Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi
halitawafumba macho wale wote watakaobainika kuhusika katika mauaji ya watoto
katika Kata ya Lamadi wilayani Busega na badala yake litawashughulikia kwa
mujibu wa sheria.
Inspekta
wa Polisi Sirro ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Lamadi
Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Uwanja wa Kisesa Kijiji cha Lamadi, kufuatia matukio ya mauaji yaliyoripotiwa
mwishoni mwa mwaka jana na hivi karibuni.
IGP
Sirro amewatoa hofu wananchi wa Lamadi na kuwasihi kuendelea kuliamini jeshi la
Polisi kuwa liko imara na kuwahakikishia kwamba Serikali yao ipo kazini
kuhakikisha mauaji hayo yanakomeshwa.
Amesema
mauaji hayo yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina na ramli chonganishi
hivyo akawataka waganga wa jadi wanaojihusisha na ramli chonganishi kuacha mara
moja maana ni kinyume na sheria, huku akiwataka waganga ambao bado
hawajasajiliwa kwa mujibu wa sheria wafanye hivyo haraka.
“Tutawashughulikia
wote wanaotaka kuwafanya wana Lamadi wasiishi kwa amani, kwa sababu tunaamini
waliofanya haya ni wanaopiga ramli chonganishi ambao ni wachache, nitumie
nafasi hii kuwataka waganga ambao hawajasajiliwa kwenda kujisajili haraka,
msipojisajili tutawachukulia hatua pia” alisema
Aidha, Sirro ametoa wito kwa
jamii kuachana na imani za kishirikiana, mila na desturi potofu ambazo amesema
zinarudisha nyuma maendeleo, badala yake akataka elimu iendelee kutolewa kwa
jamii ili iweze kubadilika.
Katika hatua nyingine IGP Sirro aliwataka wananchi na
viongozi Mkoa Simiyu kushirikiana na jeshi hilo, huku akisisitiza kuwa ushirikiano watakaotoa kwa polisi ndiyo
utasaidia wahusika wote kukamatwa.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kufuatia mauaji hayo Serikali imeshawafikisha
mahakamani watuhumiwa wa mauaji ya watoto.
Aidha,
Mtaka amebainisha kuwa kabla ya watuhumiwa kufikishwa mahakamani Serikali kupitia
vyombo vyake vya dola ilisimamia zoezi la upigaji kura za siri ambazo wananchi
waliomba wapige ili kuwabaini wauaji hao ambalo lilifanyika 13 Februari, 2019.
MWISHO.
Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini IGP Simon Sirro
0 comments:
Post a Comment