Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, Mhe.Stella
Ikupa ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu,
kuwahamasisha wanachama wao kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF
)ulioboreshwa ili waweze kupata uhakika wa matibabu.
IKUPA ametoa wito huo wilayani Itilima
katika ziara yake wakati akizungumza na viongozi wa Wilaya, Viongozi wa Vyama
vya wenye ulemavu na baadhi ya wenye
ulemavu wenyewe wakati wa ziara yake wilayani humo Februari 25, 2019, ambayo ililenga
kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ikiwa ni pamoja na mradi wa Kitalu
nyumba na masuala mbalimbali yahusuyo wenye walemavu.
Amesema ni vema viongozi wa vyama na wenye ulemavu
wakapena taarifa na kuhamasishani kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF)
ulioboreshwa, ili wapewe vitambulisho waweze kutibiwa kirahisi.
“Mkijiunga na CHF iliyoboreshwa mkapata kadi mtakuwa na
uwezo wa kutibiwa muda wowote, kwa hiyo peaneni hizo taarifa mjiunge watu
mnaofahamiana muweze kupewa hivyo vitambulisho mpate kutibiwa kirahisi wakati
tukiwa tunasubiri ile bima ya afya kwa kila Mtanzania” alisema Mhe. Ikupa.
Katika hatua nyingine amewaagiza maafisa Ustawi wa
jamii na maendeleo ya jamii kutoa elimu vijijini kwa watu wenye
ulemavu kuhusiana na uundwaji wa vikundi na namna ya kutekeleza miradi
mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima,Mhe. Benson Kilangi akizungumzia utekelezaji
wa mradi wa kitalu nyumba amesema katika awamu ya kwanza jumla ya vijana 20
wamepata mafunzo ya utengenezaji wa vitalu nyumba na kufundishwa stadi
mbalimbali za kuendesha kilimo biashara na kuongeza mnyororo wa thamani.
Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Festo Kiswaga amesema miradi ya
vitalu katika Mkoa wa Simiyu itatekelezwa kwa viwango na kwa malengo
yaliyokusudiwa, huku akibainisha kuwa vitasaidia kuongeza kipato kwa wananchi katika
mkoa na kuwa sehemu ya wananchi kujifunza
kilimo bora.
Kwa upande wao viongozi pamoja na
watu wenye ulemavu walioshiriki katika ziara hiyo wamemwomba Mhe. Naibu Waziri
kushughulikia baadhi ya changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.
“Ninaomba Serikali itusaidie tuweze
kupata wakalimani wa lugha ya alama ili na sisi walemavu wa kusikia tuweze
kupata ujumbe unaokuwa unawasilishwa na viongozi wetu kwenye mikutano na ziara
kama hii ya leo hii itatusaidia sana” alisema Mhandi Ntobi Mwenyekiti wa Chama
cha Walemavu wasiosikia Mkoa wa Simiyu.
“NaombaWataalam waje watutembelee
kwenye vijiji vyetu na kwenye vyama vyetu watusaidie kutupa elimu ya namna ya
kuunda vikundi na namna ya kufanya shughuli zinazoweza kutuongezea kipato” Bw.
Seni Jitabo mlemavu wa viungo Mkazi wa Zagayu wilayani Itilima.
Naibu Waziri Ikupa, anaendelea na
ziara yake Mkoani Simiyu ambayo itahitimishwa 27 Februari 2019, akiwa wilayani Itilima
Naibu waziri ametembelea kitalu nyumba kilichopo Lagangabilili na kituo cha
maarifa ya jamii Kanadi, ambako amejionea shughuli mbalimbali za uzalishaji
zinazofanywa na vijana.
MWISHO
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia
walemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza jambo na Bw. Mhandi Ntobi ambaye ni
Mwenyekiti wa Chama cha Watu wasiosikia Mkoa wa Simiyu, wakati akiwa katika
ziara yake Wilayani Itilima Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019.
Mbunge wa Jimbo la
Bariadi, Mhe. Andrew Chenge akimweleza jambo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu,
Mhe. Stella Ikupa( wa pili kulia) alipotembea Ofisi za CCM Mkoa wa Simiyu
wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia
walemavu, Mhe. Stella Ikupa( katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watumishi wa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii Mkoani Simiyu(NSSF na PSSSF) mara baada ya kutembelea ofisi za
mifuko hiyo wakati wa ziara yake mkoani Simiyu , Februari 25, 2019.
Bw. Seni Jitabo ambaye
ni mlemavu wa Viungo akiwasilisha baadhi ya changamoto kwa Naibu Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia
walemavu, Mhe. Stella Ikupa(hayupo pichani) wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu,
Februari 25, 2019
Mwenyekiti wa Chama cha
Watu wenye ualbino , akiwasilisha baadhi ya changamoto za kundi hilo kwa Naibu Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia
walemavu, Mhe. Stella Ikupa(hayupo pichani) wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu,
Februari 25, 2019
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia
walemavu, Mhe. Stella Ikupa akipokea zawadi ya sabuni kutoka kwa Afisa Vijana
wa Wilaya ya Itilima ambaye alimkabidhi kwa niaba ya viongozi wa Wilaya hiyo wakati
wa ziara yake Mkoani Simiyu, Februari 25, 2019
Moja ya Kitalu
nyumba(green house) ikatika kata ya Lagangabilili wilayani Itilima,
kilichotembelewa na Naibu Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia
walemavu, Mhe. Stella Ikupa wakati wa ziara yake.
Baadhi
ya viongozi , watendaji na watu wenye ulemavu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya
Itilima, Mhe. Benson Kilangi akitoa taarifa ya Wilaya Februari 25, 2019 kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella
Ikupa,ambaye yupo ziarani mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia
walemavu, Mhe. Stella Ikupa(aliyeketi) akipewa maelezo ya namna sabuni za WIZA
zinavyotengenezwa, wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kata ya Kanadi wakati
waziara yake wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Februari 25, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia
walemavu, Mhe. Stella Ikupa(aliyeketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya Viongozi wa Wilaya ya Itilima, mara baada ya kukamilisha ziara yake wilayani
humo Februari 25, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia
walemavu, Mhe. Stella Ikupa(aliyeketi katikati )akiwa katika picha ya pamoja na
wana kikundi wanaojihusisha na utengenezaji wa sabuni za WIZA zinazotengenezwa katika
Kata ya Kanadi wakati wa ziara yake
Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Februari 25, 2019.
Sehemu ya Jengo la Kiwanda cha Sabuni Itilima kilichopo Kanadi
Viongozi wa Wilaya ya
Itilima wakimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa kwa
ajili ya kuanza ziara wilayani humo, Februari 25, 2019.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia
walemavu, Mhe. Stella Ikupa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya
sekondari Kanadi wilayani Itilima, wakati
wa ziara yake Wilaya ya Itilima mkoani
Simiyu Februari 25, 2019
0 comments:
Post a Comment