Wanafunzi wa shule za Serikali (kata) Wilayani Bariadi
Mkoani Simiyu, Ibrahim Buyungumya kutoka Shule ya Sekondari Nkololo ,
aliyeongoza kimkoa kwa kupata daraja la kwanza alama (points) saba na Kwandu
Maduhu wa Biashara Sekondari aliyepata daraja la kwanza alama kumi na
moja, wamekiri kuwa kambi za kitaaluma zimechangia kuongeza ufaulu wao katika Mtihani wa Kidato
cha Nne mwaka 2018.
Wanafunzi hao wameyasema hayo katika hafla ya kuwapongeza
walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Matokeo ya mtihani
wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 Kimkoa
na kuufanya mkoa kushika nafasi ya Tisa Kitaifa, iliyofanyika katika Shule ya
Sekondari Nkololo wilayani Bariadi, Februari 13, 2019.
Wanafunzi
hao wamesema pamoja na kumuomba Mungu, juhudi zao binafsi za kujisomea, jitihada
za walimu, malezi kutoka kwa wazazi wanakiri kambi za kitaaluma zilizofanyika
mkoani Simiyu kwa madarasa yote ya mitihani ziliwasaidia kuwaandaa na mtihani
huo wa Taifa, huku wakisisitiza kambi hizo ziwe endelevu na wakapendekeza kuwa kwa mwaka 2019 ziongezewe
muda na zianze mapema zaidi.
“ Namshukuru
Mungu kunifanikisha kupata daraja la kwanza alama saba, nawashukuru walimu
wangu, wazazi wangu kwa namna walivyokuwa msaada kwangu; pia kipekee namshukuru
Mkuu wetu wa Mkoa kwa kutuletea kambi,
zimetusaidia sana maana tulipata nafasi ya kukutana na wanafunzi wenzetu
na walimu mahiri kutoka shule mbalimbali na zilitusaidia kuelewa masomo kwa
mawanda mapana zaidi” alisema Ibrahimu Buyungumya.
“Namshukuru
Mungu kwa kuniwezesha kupata daraja la kwanza alama 11, nawashukuru wazazi,
walimu pia nashukuru uwepo wa kambi za kitaaluma ambazo zilitusaidia sana
kujiandaa vema na mtihani wetu, nashauri kambi hizi zianze mapema na muda uongezwe
ili ziwasaidie wadogo zetu wafaulu
vizuri zaidi yetu sisi” alisema Kwandu Maduhu.
Mkuu
wa Shule ya sekondari Biashara, Mwl. Mathias Joseph ambaye shule yake ilifanya
vzuri kwa kupata alama A 23 na alama B 79 amesema pamoja na kambi za kitaaluma siri
nyingine ya kufanya vizuri ni jitihada zilizofanywa na walimu pamoja na usimamizi
mzuri wa mikakati iliyowekwa na idara ya Elimu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi, ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi na mitihani ya mara kwa
mara.
Akizungumza
katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya
vizuri katika Matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 katika mkoa, Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewapongeza
viongozi, walimu, wanafunzi, wazazi na wadau wote wa elimu mkoani humo, kwa
jitihada walizofanya katika kuongeza ufaulu.
Aidha,
Mtaka ameelekeza kamati zote za shule zikutane na wazazi wa wanafunzi wa
madarasa ya mtihani ili wakubaliane juu ya wanafunzi hao kuanza kambi za kitaaluma
na wazazi hao wachangie chakula ambacho watoto wao wangekula wakiwa majumbani
kwao kitumike wakiwa kambini.
“Nilishatoa
maelekezo na nayarudia; kamati za shule zikae na wazazi wakubaliane madarasa yote
ya mtihani watoto waanze kambi za kitaaluma na wazazi wachangie chakula kile kile
ambacho watoto wangekula wakiwa nyumbani, ili watoto wapate nafasi nzuri ya
kusoma na kujiandaa na mtihani wa Taifa” alisema Mtaka.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo ametoa
wito kwa wazazi mkoani humo kuhimiza watoto kusoma ili waweze kufikia ndoto zao
akakemea tabia ya baadhi ya wazazi kuwaachisha masomo watoto wa kike na kuwaozesha.
Jumla
ya wanafunzi 7094 kati yao wavulana ni 4224 na wasichana 2875 walifanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha
Nne mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwezesha mkoa kushika nafasi ya tisa Kitaifa
kati ya mikoa 31, ambapo umepanda kwa nafasi mbili ikilinganishwa na mwaka 2017
ambapo ulishika nafasi ya 11 Kitaifa.
Katika
pongezi zilizotolewa kwa walimu na wanafunzi mwanafunzi wa kiume aliyeongoza
Kimkoa amezawadiwa shilingi milioni Moja, mwanafunzi bora wa kike shilingi
laki tano (wote wamefunguliwa akaunti) na kuahidiwa kupewa mahitaji yote muhimu
watakapochaguliwa kidato cha tano, huku walimu sitini kila mwalimu akipewa shilingi elfu ishirini kwa kila alama
A iliyopatikana kwenye somo lake.
MWISHO
Mwanafunzi kutoka Shule
ya Kata Nkololo aliyefanya vizuri kwa
kupata daraja la kwanza (pointi saba) na kushika nafasi ya kwanza kimkoa katika
mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 Ibrahimu Buyungumya(kushoto) na
Mwanafunzi wa Kike Kwandu Maduhu kutoka
Shule ya Sekondari Biashara aliyefanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza
(pointi 11) katika mtihani huo na kuongoza kimkoa (wasichana), wakionesha kadi
zao za akaunti ambazo wamekabidhiwa (katika hafla maalum ya kuwapongeza
iliyofanyika shule ya Sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari13, 2019 )
baada ya kufunguliwa akaunti na kuwekewa zawadi hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akizungumza jambo na Mwanafunzi kutoka Shule ya Kata Nkololo aliyeongoza
kimkoa katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 kwa kupata daraja la kwanza(pointi saba) ,Ibrahimu
Buyungumya(kushoto) na Mwanafunzi wa
Kike Kwandu Maduhu kutoka Shule ya Sekondari Biashara aliyeongoza kwa upande wa
wasichana kwa kupata daraja la kwanza
(pointi 11) katika mtihani huo, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu na
wanafunzi waliofanya vizuri kimkoa, iliyofanyika katika shule ya sekondari
Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(mwenye suti kulia) akishuhudia wanafunzi wa kidato cha nne
katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi wakifanya mazoezi kwa vitendo wakati wa hafla
ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika
Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa shuleni hapo, Februari
13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kushoto) akiwakabidhi zawadi ya ngao viongozi wa
Halmashauri ya mji wa Bariadi ambayo iliongoza kimkoa na kushika nafasi ya tisa
kati ya halmashauri zaidi ya 185 nchini katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha
nne mwaka 2018, (kushoto na wa pili kushoto) ni wanafunzi walifanya vizuri
Kimkoa kutoka shule za Serikali), wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu
waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika
kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (wa nne kushoto mbele) katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa mkoa na Halmashauri ya Mji wa Bariadi , walimu wa Halmashauri ya
Mji wa Bariadi, wanafunzi walawili walioongoza katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato
cha nne mwaka 2018 Kimkoa na wazazi wao, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu
waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika
kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na viongozi, walimu, wazazi na
wanafunzi katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi
waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika
kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Shule ya
Sekondari Biashara Mwalimu Mathias Joseph akionesha zawadi ya shilingi
460,000/= iliyotolewa kama motisha kwa walimu wa shule hiyo waliofanikisha
kutoa jumla ya alama A 23 katika Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha nne
mwaka 2018, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi
waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya
sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na viongozi, walimu, wazazi na
wanafunzi katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi
waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika
kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mwanafunzi kutoka Shule
ya Kata Nkololo aliyefanya vizuri kwa
kupata daraja la kwanza (pointi saba)na kushika nafasi ya kwanza kimkoa katika
Matokeoya mtihani wa Taifa wa Kidato cha
nne mwaka 2018 Ibrahimu Buyungumya, katika hafla ya kuwapongeza walimu
waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika
kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkololo wakishangilia jambo, katika hafla ya
kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Matokeo
ya Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika
kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (wa tano kushoto mbele) katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, walimu wa Halmashauri ya
Wilaya ya Meatu, wanafunzi wawili walioongoza katika mtihani wa Taifa wa kidato
cha nne mwaka 2018 Kimkoa na wazazi wao, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu
waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika
kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (wa tano kushoto mbele) katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, walimu wa Halmashauri ya
Wilaya ya Itilima, wanafunzi wawili walioongoza
katika matokeo ya mtihani wa
Taifa wa kidato cha nne mwaka 2018 kimkoa na wazazi wao, baada ya hafla ya
kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani
huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi
Februari 13, 2019.
Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Jackson Yuma akizungumza na viongozi, walimu,
wazazi na wanafunzi katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na
wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya
Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule
ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (mwenye skafu ) akiwa ameongoza na baadhi ya viongozi
waliompokea katika shule ya sekondari
Nkololo na kumuongoza kueleka eneo la
hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri
katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha
nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani
Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akizungumza na viongozi, walimu, wazazi na
wanafunzi katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi
waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika
kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akizungumza jambo na Mwanafunzi kutoka Shule ya Kata Nkololo aliyeongoza
kimkoa katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 kwa kupata (pointi saba) ,Ibrahimu Buyungumya(kushoto) na
Mwanafunzi wa Kike Kwandu Maduhu kutoka
Shule ya Sekondari Biashara aliyeongoza kwa upande wa wasichana kwa kupata daraja la kwanza (pointi 11) katika
mtihani huo, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya
vizuri kimkoa, iliyofanyika katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi
Februari 13, 2019.kuliani Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga.
0 comments:
Post a Comment