Mwenyekiti wa Timu maalum ya mawaziri wanane ya kupitia maeneo yenye
migogoro kati ya wananchi na maeneo ya Hifadhi, Waziri wa
Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi amepokea ombi la
wananchi wa wilaya tatu za mkoa wa Simiyu wanaoishi katika vijiji
vinavyopakana na Pori la Akiba la Maswa la kupewa eneo lenye urefu wa
kilometa kumi, kwa ajili ya malisho na kuahidi kulifikisha kwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua zaidi.
Mhe. Lukuvi ameyasema hayo wakati
akizungumza na wananchi wa Vijiji vinavyopakana na pori la akiba la Maswa katika
mkutano wa hadhara uliofanyika Mji mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu.
Awali akijibu baadhi ya kero zilizowasilishwa
na Mwananchi wa Wilaya ya Meatu, Bw. Deusdedith Martin Waziri Lukuvi amesema timu hiyo imezisikia
kero hizo na akaahidi kuwasilisha taarifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kubainisha kuwa taarifa rasmi ya
majibu ya kero zao itatolewa.
Aidha, Waziri Lukuvi
amewahakikishia wananchi kuwa zoezi la kupima eneo la mita 500 kutoka
kwenye mpaka wa Pori la Akiba la Maswa kuelekea kwenye vijiji vinavyopakana na
Pori hilo (Buffer zone) katika Wilaya za
Meatu, Itilima na Maswa limesimamishwa mpaka litakapotolewa maelekezo.
“Hapa
kulikuwa na zoezi la kupima mita 500 kutoka kwenye mpaka wa Pori la Akiba la
Maswa kuingia kwa wananchi, maana yake ni kwamba kuna wananchi wengi na vijiji
vingi vingeathirika ili vipishe ‘buffer zone’, ingawa ni kwa mujibu wa sheria
lakini ‘buffer zone’ ile ingekula maeneo ya vijiji kwa hiyo zoezi hilo limesimamishwa”
“Zoezi
hili limesimamishwa kwa mujibu wa maelekezo ya Mhe Rais baada ya kuona watu
wengi maskini ambao walipaswa kupisha maeneo ya hifadhi;...... vile vile kuanzia
sasa zoezi lolote la kutambua mipaka litakalofanywa na watu wa Maliasili ni
lazima liwe shirikishi” alisema Waziri Lukuvi.
Awali
akiwasilisha taarifa kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Meatu, Bw. Deusdedit
Martin aliomba Timu ya Mawaziri wanane kuwasaidia katika kutatua changamoto ya
ubadilishaji wa mpaka kati ya Pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyopakana,
Uvamizi wa tembo katika mashamba na makazi ya watu na kukatazwa kwa wananchi
kulima katika eneo la mita 60 kutoka kwenye kingo za mito.
Kwa upande wake Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewahakikishia wananchi wa
Mkoa wa Simiyu upatikanaji wa uhakika wa maji kupitia mradi mkubwa
wa Ziwa Victoria, ambapo amesema kwa sasa mradi upo katika hatua ya kumtafuta mkandarasi.
Naye Naibu Waziri
wa Kilimo, Mhe.Omari Mgumba akieleza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inatoa
viatiifu kwa wakulima ambapo amesema hadi sasa zaidi ya chupa milioni saba
zimeshasambazwa kwa wakulima katika mikoa inayolima pamba hapa nchini.
Timu ya Mawaziri wanane inayoongozwa na Waziri Lukuvi pia
inajumuisha mawaziri kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Maliasili
na Utalii, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Maji na Manaibu Waziri
kutoka Wizara ya Kilimo na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
MWISHO
Mwenyekiti wa Timu ya
Mawaziri wanane wa kisekta, Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi katika
Mkutano wa hadhara Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya
mawaziri nane wa kisekta anayoiongoza kutembelea mpaka wa Pori la Akiba la
Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
Wananchi wa Wilaya ya
Meatu wakiwapungia mikono Timu ya Mawaziri nane wanaopitia maeneo yenye migogoro katika wananchi na hifadhi,
wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Meatu Mji mdogo Mwandoya mara baada ya timu hiyo kutembelea na
kujionea mpaka wa pori hilo, Februari 19, 2019
Mwenyekiti wa Timu ya Mawaziri wanane, Mhe. William Lukuvi akiteta jambo
na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa Mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Mjini Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, mara baada ya Timu
ya mawaziri wanane wanaopitia maeneo yenye migogoro kati ya wananchi na hifadhi, mara baada ya timu hiyo kutembelea na kujionea
mpaka wa pori la Akiba la Maswa, Februari 19, 2019
Bw. Deusdedit Martin
akiwasilisha taarifa ya mapendekezo ya wananchi kwa Mwenyekiti wa Timu ya
Mawaziri wanane, Mhe. William Lukuvi wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, mara baada ya timu hiyo kutembelea
mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019
Mwenyekiti wa Timu ya
Mawaziri wanane, Mhe. William Lukuvi(wa pili kushoto) akiteta jambo na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo (katikati) na Mjumbe wa
NEC, Mhe. Gungu Silanga(wa pili kulia), baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika
katika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, mara baada ya timu hiyo kutembelea
mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19,
2019.(kushoto) Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba na (kulia) Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi.
Meneja wa Pori la Akiba
la Maswa, Bw.Lusato Masinde akijibu baadhi ya hoja kutoka kwa Mwenyekiti wa
Timu ya Mawaziri wanane, Mhe. William Lukuvi katika Mkutano wa hadhara
uliofanyika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu hiyo kutembelea
mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019
Baadhi ya wajumbe wa
timu ya mawaziri wanane wa kisekta, Kutoka kulia Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Luhaga Mpina, Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI, Sulemani Jafo, Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira,Mussa Sima na Waziri wa Maji,
Pro. Makame Mbarawa wakiwa katika mkutano wa Hadhara Mji Mdogo wa Mwandoya
wilayani Meatu, baada ya timu hiyo kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa
na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi(kushoto) akifurahia jambo na Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika mkutano wa Hadhara Mji Mdogo wa
Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri nane wa kisekta ikiongozwa
na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kutembelea
mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
Wasanii kutoka wilayani Meatu wakitoa burudani katika
mkutano wa Hadhara Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya
mawaziri wanane wa kisekta ikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na
Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
Bw. Peter Ndekeja
mwananchi kutoka wilayani Meatu akitoa malalamiko yake kwa Mwenyekiti wa Timu
ya Mawaziri wanane wa kisekta, Mhe. William Lukuvi wakati wa Mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, mara baada ya timu
hiyo kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka,
Februari 19, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara Mji Mdogo
wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri wanane wa kisekta
ikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William
Lukuvi kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka,
Februari 19, 2019.
Mwenyekiti wa Timu ya
Mawaziri wanane, Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mjini Mdogo
wa Mwandoya wilayani Meatu, mara baada ya Timu ya mawaziri wanane wanaopitia
maeneo yenye migogoro wananchi na hifadhi, mara baada ya timu hiyo kutembelea
na kujionea mpaka wa pori la akiba la Maswa, Februari 19, 2019
Baadhi ya Viongozi wa
Mkoa wa Simiyu wakifuatilia Mkutano wa hadhara uliofanyika Mji Mdogo wa
Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri wanane wa kisekta ikiongozwa
na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi
kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari
19, 2019.
Baadhi ya wananchi wa
Wilaya ya Meatu wakifuatilia Mkutano wa hadhara uliofanyika Mji Mdogo wa
Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya mawaziri nane wa kisekta ikiongozwa
na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi
kutembelea mpaka wa pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari
19, 2019.
Kutoka kushoto Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock
Yakobo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira,
Mhe. Mussa Sima na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani, wakifurahia
jambo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani
Meatu, baada ya timu ya mawaziri wanane wa kisekta ikiongozwa na Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kutembelea mpaka wa
pori la Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
Mwenyekiti wa Timu ya
Mawaziri wanane wa kisekta, Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi(kushoto) katika Mkutano
wa hadhara uliofanyika Mji Mdogo wa Mwandoya wilayani Meatu, baada ya timu ya
mawaziri wanane wa kisekta ikiongozwa na Mhe.Lukuvi kutembelea mpaka wa pori la
Akiba la Maswa na Vijiji vinavyolizunguka, Februari 19, 2019.
0 comments:
Post a Comment