Wito umetolewa kwa jamii kuondokana na mila potofu ya kuwazuia watoto wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 10 mpaka 19 kutumia virutubishi vya madini chuma na foliki asidi vinavyotolewa kwa rika hilo kwa ajili ya kuwakinga na upungufu wa damu kwa madai kuwa virutubisho hivyo vibaharibu uzazi jambo ambalo halina ukweli.
Wito huo umetolewa na Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige katika kikao cha Kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF Health Africa kwa kushirikiana na Serikali kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
"Baadhi ya wazazi wamekuwa wakizuia watoto wao kupata virutubisho vinavyotolewa shuleni kutokana na imani potofu kwa madai kuwa vinaharibu uzazi; tunaendelea kutoka elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa virutubisho hivi na tunapendekeza masuala ya lishe yajumuishwe katika mitaala ya elimu na itakapobidi kufanyike mabadiliko ya mitaala ili kuongeza uelewa wa masuala haya kwa jamii," alisema Chacha.
Awali akitoa taarifa ya hali ya lishe ya Mkoa, Dkt. Magige amesema utoaji wa huduma kwa watoto wenye utapiamlo umeongezeka kutoka asilimia 14 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 88.4 Septemba 2019; huku uwekezaji katika utoaji wa elimu ya unasihi wa masuala ya lishe ngazi ya jamii pia ukiongezeka kutoka asilimia 50 mwaka 2017 hadi asilimia 72.2 Septemba 2019.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Ngulyati wilayani Bariadi, Nyabuho Paschal ambaye pia ni muelimishaji rika, amesisitiza watoto wa kike kuona umuhimu wa kutumia Virutubishi vya Madini Chuma na foliki asidi kwa kuwa vina mchango mkubwa katika rika balehe kwa wasichana na kutosikiliza maneno ya upotoshaji yanayotolewa na baadhi ya wazazi na walezi kuhusu virutubishi hivyo.
Naye Mratibu wa lishe ya Mama, watoto na vijana balehe kutoka Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Bibi. Tufingene Malambugi amesema katika ziara iliyofanywa na Kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start katika vituo vya kutolea huduma za afya wilayani Bariadi, ilibainika kuwa shughuli mbalimbali za afya na lishe zinatolewa ikiwemo matibabu ya utapiamlo na utoaji wa elimu ya lishe.
Meneja Mradi wa Right Start Initiatives mikoa ya Simiyu na Mwanza, Dkt. Rita Mutayoba amesema pamoja na shughuli za afya na lishe mradi huu pia unatoa elimu ya lishe ngazi ya jamii kupitia vipeperushi na mabango, kufanya uhamasishaji kupitia wahudumu wa afya ngazi ya jamii, mikutano ya uhamasishaji ya mara kwa mara ambao unafanywa kwa kutumia ngoma za asili ili kufikisha ujumbe katika maeneo husika.
Sanjali na hilo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF Health Africa, Dkt. Florence Temu amewashukuru wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika utekelezaji wa mradi wa Right Start unaotarajiwa kufikia ukomo wake mwezi Machi 2020, huku akibainisha kuwa mradi huo umesaidia kuboresha masuala mbalimbali ya afya na lishe.
Wakati huo huo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah Bw. Donatus Weginah amesema Mkoa wa Simiyu utaendelea kuweka mipango madhubuti ya kuendeleza shughuli mbalimbali za masuala ya afya na lishe zinazofanywa na Mradi wa Right Start na kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya wananchi kuwa na lishe bora yanafikiwa.
MWISHO
Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Mipango na Uratibu, katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akifungua kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, Dkt. Florence Temu akizungumza na wajumbe wa kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.
Meneja Mradi wa Right Start, Dkt. Rita Mutayoba akiwasilisha taarifa ya mradi huo kwa wajumbe wa kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya mradi huo unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange akizungumza na wajumbe wa kikao cha kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, wakiwa katika kikao kilichofanyika Desemba 20, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa Lishe wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Chacha Magige (kulia) akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa kamati tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa, wakati walipotembelea kituao cha Afya cha Ngulyati wilayani Bariadi Desemba 19, 2019 kujionea hali ya utekelezaji wa masuala ya lishe .
Baadhi ya wakina mama na wakina baba wakipata elimu ya masuala ya lishe katika kituo cha afya cha Ngulyati .
Kaimu Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akizungumza na Baadhi ya wajumbe wa kamati
tendaji ya Kitaifa ya Mradi wa Right Start unaotekelezwa kwa ushirikiano kati
ya Serikali na Shirika lisilo la kiserikali la AMREF Health Africa,
walipomtembelea ofisini kwake Desemba
19, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment