Saturday, December 7, 2019

WANAFUNZI 18,306 WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 SIMIYU

Jumla ya wanafunzi 18,306 sawa na asilimia 73.5 kati ya 24,915 waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 wamechaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza katika awamu ya kwanza mwaka 2020 katika shule za Serikali za Bweni na Kutwa.

Akitangaza matokeo hayo Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema idadi ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2020 imeongezeka kwa wanafunzi 5900 sawa na asilimia 23.8 ikilinganishwa na wanafunzi 12,399 waliochaguliwa mwaka 2019.
Aidha, Sagini amezitaka Halmashauri mkoani Simiyu kukamilisha miundombinu inayohitajika ili wanafunzi 6609 watakaochaguliwa awamu ya pili waweze kuripoti shuleni kabla ya 15 Februari, 2020.

“Halmashauri kamilisheni miundombinu inayohitajika ili wanafunzi watakaochaguliwa awamu ya pili waweze kuripoti shule kabla ya tarehe 15 Februari 2020; nawasihi  wazazi na walezi wa wanafunzi 6609 waliokosa nafasi awamu ya kwanza kuwa wavumilivu wakati halmashauri zinaendelea kukamilisha miundombinu inayohitajika,” alisema Sagini.

Katika hatua nyingine Sagini amewapongeza wanafunzi wote waliopata nafasi ya kuchaguliwa kidato cha kwanza na kuwaasa wasifanye anasa watumie fursa hiyo kujifunza na hatimaye wakamilishe safari ya elimu, huku akiwashukuru wadau wote wa elimu wakiwemo wazazi na walimu kwa namna walivyochangia katika uendeshaji na utoaji wa elimu bora.

Ameongeza kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa kidato cha kwanza wanapaswa kuripoti shuleni tarehe 06 Januari, 2019 huku akiwasisitiza wazazi, walezi na jamii kwa kushirikiana na viongozi wa wilaya kuhakikisha wanfunzi woe waliochaguliwa wanaripoti shuleni na kubaki shuleni mpaka watakapohitimu elimu ya kidato cha nne.

Naye Afisa elimu wa Mkoa, Mwl. Ernest Hinju amesema matokeo ya mwaka 2019 kwa darasa la saba mkoa umepata zaidi ya asilimia 86 na kuufanya mkoa kushika nafasi ya nane Kitaifa ikilinganishwa na mwaka jana ambapo mkoa ulishika nafasi ya 22 Kitaifa, jambo ambalo limeufanya mkoa kuwa miongoni mwa mikoa iliyofanya vizuri na kuwa katika nafasi 10 bora kitaifa kwa mitihani yote mikubwa mtihani wa darasa la saba, kidato cha nne(nafasi ya 9) na kidato cha sita (nafasi ya 10).

Nao baadhi ya wajumbe walitoa maoni yao kuhusu namna ya kuboresha elimu na kuwasaidia wanafunzi ambao hawajapata nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari ambapo walishauri ujenzi wa vyuo vya ufundi na kuongea jitihada katika michezo.

“ “Ninashauri  kila Halmashauri iweke mkakati wa kuwa na vyuo ufundi ili waanfunzi wanaokosa nafasi kujiunga na elimu ya sekondari wapate fursa ya kujifunza ufundi na waweze kujiajiri na kujikwamua kimaisha,’ alisema Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Mwl. Juma Athuman.

“Moja ya sababu zinazochangia kushusha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi ni utoro, napendekeza kuwa ili kukabiliana na tatizo la utoro Halmashauri zione haja ya kuimarisha miundombinu ya michezo; wanafunzi wengi wanaopenda michezo wanajituma pia na darasani ushahidi ninao, wanamihezo wanaofanya vizuri kwenye riadha ndani ya mkoa wetu wanafanya vizuri kitaaluma,” alisema Yohana Misese.
MWISHO



 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza mwaka 2020 katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza mwaka 2020 katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Afisa elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya ufaulu kwa darasa la saba mwaka 2019 katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja katika katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza mkoani Simiyu, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza mwaka 2020 katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya akichangia hoja katika katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe  akichangia hoja katika katika kikao cha Kamati ya uchaguzi wa wanafunzi watakaoingia Kidato cha kwanza, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!