Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amezipongeza Wakala wa Barabara nchini
(TANROADS) na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoa wa Simiyu kwa
kazi nzuri zinazofanya na kuzisisitiza kutenga bajeti ya kuboresha ujenzi wa
Barabara zote zinazounganisha Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine ili zipitike
wakati wote.
Kiswaga
ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Simiyu,
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Desemba 30, 2019 mjini
Bariadi ambapo amebainisha kuwa barabara zikiboreshwa zitarahisisha usafiri kwa
wananchi na usafirishaji wa malighafi mbalimbali za viwanda na bidhaa
zitakazozalishwa na viwanda, vinavyotarajiwa kujengwa Mwaka 2020.
“Kazi
inayofanywa na TANROADS na TARURA ni kazi ambayo inatia moyo na itakuwa na mchango mkubwa kwa viwanda vya
nguo, glasi na vifaa tiba vitakavyoanzishwa mwakani; kwa maana ya material(malighafi)
itakayoingia na bidhaa zitakazotengenezwa zitasafirishwa kwa urahisi,” alisema
Kiswaga.
Akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa miradi Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. John Mkumbo amesema katika robo ya pili ya mwaka wa fedha
2019/20 kazi za matengenezo ya barabara ambazo zipo kwenye
utekelezaji ni kilometa 108.12 na madaraja 14.3 sawa na 54.3% huku
iliyokamilika kwa barabara kuu ni kilometa 246.52 na madaraja 19.71 sawa na
40.8%.
Kwa upande
wake Mratibu wa TARURA mkoa wa Simiyu Mhandisi Dkt. Philemon Msomba
amesema kuwa wametekeleza jumla ya miradi 30 ambayo tayari imekamilika
yenye thamani ya shilingi 3,694,627,194 bila VAT .
Katika
hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya Meatu, Dkt Joseph Chilongani amesema ni
vyema wakala wa barabara nchini (TANROADS) na Wakala wa Barabara Mijini na
Vijijini (TARURA) kuboresha madaraja
yaliyopo wilaya ya Meatu kwa kujenga madaraja ya juu badala ya yale yaliyopo
sasa ambayo ni ya chini ili barabara hizo zipitike wakati wote.
Naye
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Enock Yakobo aliwataka
wakala hao kuweka taa kwenye maeneo ya katika ya miji ili wananchi waweze kufanya
biashara zao nyakati zote ( saa 24).
Mbunge wa Busega,
Mhe. Dkt. Raphael Chegeni ameshauri kuwa ni vema Serikali ikafanya marekebisho katika mgao wa fedha za bajeti ya barabara kati
ya wakala Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Mijini
na Vijijini (TARURA) kutoka kwenye uwiano wa sasa, ambapo TANROADS inapata asilimia 70 na
TARURA asilimia 30, iwe asilimia 40 kwa
TARURA na asilimia 60 kwa TANROADS ili kuongeza ufanisi kwa TARURA.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.
Festo Kiswaga akifungua kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka, kikao kilichofanyika Desemba 30,
2019 mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi
ya Barabara Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa
katika kikao hicho, Desemba 30, 2019.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara
Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. John Mkumbo akiwasilisha taarifa
katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Desemba
30, 2019 mjini Bariadi.
Mratibu wa Wakala wa Barabara za
Mijini na Vijijini Tanzania (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Dkt.Philemon
Msomba akiwasilisha taarifa katika
kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Desemba 30, 2019
mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.
Jumanne Sagini , akifafanua jambo katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa
Simiyu, kilichofanyika Desemba 30, 2019 mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Enock Yakobo akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa
wa Simiyu, kilichofanyika Desemba 30, 2019 mjini Bariadi.
Mbunge wa Jimbo la Itilima Mhe.
Njalu Silanga akichangia hoja katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa
Simiyu, kilichofanyika Desemba 30, 2019 mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi
ya Barabara Mkoa wa Simiyu, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa
katika kikao hicho, kilichofanyika Desemba 30, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment