Jumla ya wafungwa 136 kutoka magereza za Mkoa wa
Simiyu wameachiwa huru kufuatia msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alioutoka Desemba, 2019 katika
sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika
jijini Mwanza.
Akitoa
taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari Desemba 10, 2019 Mkuu wa Jeshi la
Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP. Andulile Mwasampeta amesema anamshukuru Mhe. Rais Magufuli kitendo hicho cha kutoa msamaha ambacho kimesaidia
kupunguza msongamano kwenye magereza ya mkoa wa Simiyu.
“Ninamshukuru
sana Mhe. Rais Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kwa kutoa
msamaha huu ambao umepunguza msongamano katika magereza yetu hususani gereza la
Bariadi; nitumie nafasi kuwaasa wafungwa waliosamehewa kwenda kuwa raia wema na
wakafanye kazi halali na wasifanye makosa yatakayowaleta tena hapa gerezani,”
alisema ACP Mwasampeta.
ACP
Mwasampeta ameongeza kuwa wafungwa 136 waliopata msamaha wa Rais katika mkoa wa
Simiyu ni wale waliokuwa wamebakisha muda wa siku moja hadi miezi sita miezi 12 kumaliza
muda wa vifungo vyao, ambapo amebainisha kuwa wamezingatia maelekezo ya Mhe.
Rais katika vigezo vya watu walioachiwa huru.
Aidha,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa kufanikisha zoezi la kuwaleta
pamoja wafungwa wote waliopata msamaha wa
Rais kwa kutoa magari
yaliyowezesha jeshi la magereza kuwachukua katika magereza mbalimbali
mkoani Simiyu na kuwaleta katika gereza la Bariadi ambapo ndipo walipoanzia
safari ya kurejea majumbani kwao.
Kwa
upande wao wafungwa waliopata msamaha wa Rais na kuachiwa huru wamemshukuru
Mhe. Rais Magufuli kwa kutoa msamaha huo na kuahidi kuwa raia wema watakaofanya
kazi halali na kujiepusha na makosa yote yanayoweza kusababisha wakarudi tena
gerezani.
“Namshukuru
sana Mhe. Rais kwa msamaha huu alioutoa kwa wafungwa zaidi ya 5000 tuliokuwa
magereza mbalimbali niseme tu kwamba wale wote waliokuwa wafungwa kama mimi na
wakapata msamaha huu tukawe raia wema na tukachape kazi tujenge nchi yetu, “
alisema Buluba George miongoni mwa wafungwa 136 mkoani Simiyu.
“Mimi naahidi kwenda kujishughulisha na shughuli za
kuniwezesha kupata kipato, nitajitahidi kufanya kazi kwa bidii ili nisije
nikaletwa tena huku gerezani, namshukuru sana Rais Magufuli kwa kutupa msamaha
huu,” alisema Musa Lazaro miongoni mwa wafungwa 136 mkoani Simiyu
MWISHO
Sehemu ya Wafungwa 136
kutoka mkoa wa Simiyu waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli wakiwa tayari kuondoka katika Gereza la
Bariadi Desemba 10, 2019 mara baada ya
kuachiwa huru kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe za
miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.

Pombe Magufuli wakishuka kwenye magari yaliyowasafirisha
kutoka magereza mbalimbali mkoani Simiyu kuwaleta Gereza la Bariadi, Desemba
10, 2019 kwa ajili ya kuruhusiwa kurejea
majumbani kwao kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe za
miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
Mkuu wa Jeshi la
Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP Andulile Mwasampeta (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) Desemba 10, 2019 mara baada ya kuwaachia wafungwa 136 kufuatia msamaha wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru
wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
Bw. Buluba George
miongoni mwa wafungwa 136 mkoani Simiyu waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru
wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza akimshukuru Mhe. Rais kwa
msamaha huo mbele ya waandishi wa habari, Desemba 10, 2019.
Baadhi ya wafungwa
waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli wakiagana na Mkuu wa Jeshi la
Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP Andulile Mwasampeta (kushoto) Desemba 10, 2019 mara
baada ya kuachiwa huru kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika
sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
Bw. Musa Lazaro
miongoni mwa wafungwa 136 mkoani Simiyu waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru
wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza akimshukuru Mhe. Rais kwa
msamahahuo mbele ya waandishi wa habari, Desemba 10, 2019
Baadhi ya wafungwa
wakitoka katika gereza la Bariadi Desemba 10, 2019 mara baada ya kuachiwa huru
kufuatia msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli
alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba
09, 2019 Jijini Mwanza.
Mmoja wa Wafungwa 136 mkoani Simiyu waliopata msamaha wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli alioutoa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru
wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza akimshukuru Mhe. Rais kwa
msamahahuo mbele ya waandishi wa habari, Desemba 10, 2019
Baadhi ya wafungwa
waliopata msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli wakiagana na Mkuu wa Jeshi la
Magereza Mkoa wa Simiyu, ACP Andulile Mwasampeta (kulia) Desemba 10, 2019 mara
baada ya kuachiwa kufuatia msamaha huo uliotolewa na Mhe. Rais katika sherehe
za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 09, 2019 Jijini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment