Tuesday, December 3, 2019

SERIKALI YAWAFICHUA WATOTO 16,000 WENYE ULEMAVU WALIOFICHWA NA KUWAANDIKISHA SHULE


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa amesema Serikali imewafichua na kuwatambua jumla ya watoto 16,000 wenye ulemavu wa aina mbalimbali waliokuwa na umri wa kwenda shule katika mikoa yote hapa nchini waliokuwa wamefichwa na kuwaandikisha shule kulingana na mahitaji yao ya msingi.

Naibu waziri Ikupa ameyasema hayo Desemba 03, 2019 katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

“Watoto wenye mahitaji maalum waliokuwa wamefichwa Serikali imewatambua na kuwaandikisha shule kulingana na mahitaji yao ya msingi, watoto 16,000 wametambuliwa kutoka mikoa na halmashauri zote nchini isipokuwa Halmashauri tisa tu ambazo hazijafikiwa kwa kuwa zoezi hili ni endelevu kadri bajeti itakavyoruhusu nazo zitafikiwa,”alisema Ikupa.

Aidha akijibu baadhi ya changamoto zilizowasilishwa na  Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) kuhusiana na kutengewa bajeti  ndogo amesema kuwa tayari serikali imetenga milioni 30 kwa ajili ya kuliwezesha baraza la watu wenye ulemavu  kufanya kazi kwa ufanisi, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kuongeza nguvu katika kuwasaida watu wenye ulemavu hususani walio katika maeneo ya pembezoni.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri  Ikupa ametoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutenga nafasi maalum za uwakilishi bungeni kwa watu wenye ulemavu kama kilivyofanya Chama Cha Mapinduzi( CCM), huku akiwasisitiza wenye ulemavu na wao kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi badala ya kusubiri nafasi maalum pekee.

Awali akiwasilisha taarifa ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi amesema Simiyu inawathamini na kuwajali watu wenye ulemavu huku akibainisha kuwa Halmashauri zimetenga zaidi ya shilingi milioni 231 katika mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa watu wenye ulemavu na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo ili wajikwamue kiuchumi.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Bibi. Tungi Mwanjala ameiomba Serikali   kuviwezesha viwanda vya ndani kutengeneza vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ili kupunguza gharama zitokanazo na kodi ya kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.

Naye mmoja wa Watu wenye ulemavu Bi Nuru Awadh amesema katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano watu wenye ulemavu wameaminiwa  katika nafasi mbalimbali na sheria nyingi zinazowahusu watu wenye ulemavu zitakelezwa kwa vitendo.

Maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu inayosema: “HAMASISHA USHIRIKI WA WATU WENYE UELMAVU NA UONGOZI WAO: TEKELEZA AGENDA ENDELEVU 2030” 
**Mwisho**


Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kushoto) akizungumza na  watu wenye ulemavu  wakati alipotembelea mabanda yao kuona shughuli wanazofanya, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa tatu kushoto) akizungumza na wananchi na watu wenye ulemavu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kushoto) akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu nchini(SHIVYAWATA), Bi. Tungi Mwanjala katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Baadhi ya watu wenye ulemavu wakimsikiliza Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(hayupo pichani) katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa alemavu wasioona  kwenye banda lao , katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa pili kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi fedha  zilizotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili kuwaunga mkono watu wenye ulemavu  katika shughuli zao za uzalishaji(kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka), katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa nnekushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Mkoa wa Simiyu, Viongozi wa SHIVYAWATA na Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akitoa salamu za Mkoa kwa Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa pili kushoto) mara tu baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu nchini(SHIVYAWATA), Bi. Tungi Mwanjala akiwasilisha taarifa ya SHIVYAWATA katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu sehemu ya  fedha  zilizotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili kuwaunga mkono katika shughuli zao za uzalishaji, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaye shughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi ya sabuni ya maji kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa pili kulia) akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa kabla ya kueleka katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa nnekushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mkoa wa Simiyu na  Viongozi wa SHIVYAWATA, mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Msanii Elizabeth Maliganya akiimba wimbo wenye ujumbe maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akifurahia jambo na Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa mara baada ya kiwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kuhoto) akikaribisha katika banda la watu wenye ualbino wakayti alipotembelea mabanda ya watu wenye ulemavu kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na walemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa nnekushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mkoa wa Simiyu, Viongozi wa SHIVYAWATA na Maafisa Usatawi wa Jamii Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa nnekushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mkoa wa Simiyu na  Viongozi wa SHIVYAWATA, mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaye shughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(katikati akizungumza na wananchi na watu wenye ulemavu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu sehemu ya  fedha  zilizotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili kuwaunga mkono katika shughuli zao za uzalishaji, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(wa tano kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Mkoa wa Simiyu, Viongozi wa SHIVYAWATA na wadau wa watu wenye ulemavu, mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Baadhi ya viongozi na watendaji kutoka mkoa wa Simiyu na kutoka SHIVYAWATA wakifuatila mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendela wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaye shughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaye shughulikia watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa watu wenye ulemavu, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Gamitwe Mahaza akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi, katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Desemba 03, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!