Thursday, December 5, 2019

VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUEPUKA MGONGANO WA KIMASLAHI KATIKA MAAMUZI WANAYOFANYA

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amewataka viongozi wa Umma kuangalia maslahi ya nchi katika maamuzi wanayofanya kwa kuwa kutanguliza maslahi binafsi kunasababisha mgongano wa kimaslahi unaopelekea kuiumiza nchi.


Jaji Nsekela ameyasema hayo  wakati akizungumza na viongozi wa Umma katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma mkoani Simiyu ambayo  yamefanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

"Viongozi wa Umma wanapaswa kuzingatia kanuni na taratibu katiia maamuzi wanayofanya , ambazo zitasaidia kusiwepo mgongano wa kimaslahi ili kutenganisha matakwa binafsi  na maslahi ya Umma katika kutekeleza majukumu, wakitanguliza maslahi binafsi wanaliumiza Taifa," alisema Jaji Nsekela.

Akizungumzia suala la ahadi ya uadilifu ambayo viongozi wa Umma hukiri mara baada ya kupewa nyadhifa mbalimbali na kuapishwa, Jaji Nsekeka amesema viongozi wa Umma wasikiri ahadi hiyo kama kasuku badala yake wawe waumini wazuri wa yale wanayoyakiri ikiwa ni pamoja na kufanya kazi zao kwa uadilifu.

Aidha, Jaji Nsekela amesema Viongozi wa Umma wanapaswa kuwa wakweli  na wajaze kwa uhalali Tamko la Mali na Madeni huku akiwasisitiza kuondokana na dhana kwamba matakwa ya kisheria ya kujaza tamko hilo yanalenga kuwafilisi Mali zao kwa kuwa hakuna sheria inayozuia kiongozi wa Umma kuwa na Mali isipokuwa sheria inamtaka amiliki Mali halali zilizopatikana kwa njia halali.

Katika hatua nyingine Jaji Nsekela amewatahadharisha viongozi wa Umma kuachana na tabia ya kupokea zawadi kutoka kwa wanaowahudumia kwa kuwa jambo hilo ni kichocheo kikubwa cha rushwa, maana wao wanalipwa mishahara kwa kazi wanazofanya.

Awali akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Umma mkoani Simiyu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mafunzo hayo yatawasaidia  na kuwakumbusha viongozi hao kutoka huduma kwa wananchi kwa uadilifu pasipo upendeleo kwa kigezo cha dini, ukabila, kujuana na kutekeleza majukumu yao kwa wakati.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Lamadi wilaya ya Busega, Mhe. Laurent Bija amesema ili viongozi wa Umma waendelee kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu ni vema taasisi na mifumo dhabiti ya usimamizi ikaimarishwa na iwe endelevu.

Naye Katibu wa Idara ya Ukuzaji Maadili  kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Waziri Kipacha amesema ikitokea kiongozi wa Umma amekiuka masharti yaliyopo kwenye Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, hatua ya kwanza ni Sekretarieti ya Maadili kufanya uchunguzi wa awali.
MWISHO



Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela akiwasilisha mada katika mafunzo ya  maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua mafunzo  ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani humo yaliyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(wa tatu kushoto), Desemba 04,2019.



Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya  maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.


Katibu wa Idara ya Ukuzaji Maadili  kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Waziri Kipacha akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyoulizwa na Viongozi katika mafunzo  ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani Simiyu yakiyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(kushoto), ambayo yamefanyika  Desemba 04,2019 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Wakala wa Ununuzi Serikalini (GPSA), Bw. Honest  Kahumba akichangia hoja katika mafunzo  ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani Simiyu yakiyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(hayupo pichani), ambayo yamefanyika  Desemba 04,2019 Mjini Bariadi.
Diwani wa Kata ya Lamadi wilayani Busega, Mhe. Laurent Bija akichangia hoja katika mafunzo  ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani Simiyu yakiyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(hayupo pichani), ambayo yamefanyika  Desemba 04,2019 Mjini Bariadi.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushoto) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya  maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.



Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua mafunzo  ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani humo yaliyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(wa pili kushoto),  ambayo yamefanyika Mjini Bariadi Desemba 04,2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifunga mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa viongozi wa Umma mkoani humo (kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka) yaliyoendeshwa na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela(kushoto),  ambayo yamefanyika Mjini Bariadi Desemba 04, 2019.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Idara wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Taasisi za Umma Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya  maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Seksheni na Vitengo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulizni na Usalama ya Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushotowalioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Madiwani kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (wa tatu kushoto walioketi) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Madiwani kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Simiyu mara baada ya mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa  Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, kwa ajili ya kutoa mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akiwasilisha mada katika mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (hayupo pichani) akizungumza na viongozi wa Umma, wakati alipowasili Mjini Bariadi  kutoa mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa   Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela (katikati)akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya  kuwasili Mjini Bariadi, kwa ajili ya kutoa mafunzo ya maadili na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi  kwa  kwa Viongozi wa Umma kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma mkoani Simiyu , yaliyofanyika Desemba 04, 2019 Mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!