Wednesday, December 11, 2019

RC MTAKA AIPONGEZA AGPAHI KWA KUTEKELEZA MIRADI YENYE TIJA KWENYE SEKTA YA AFYA

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka Shirika lisilo la Kiserikali linaloshughulikia masuala ya UKIMWI la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa kutekeleza miradi yenye tija  katika sekta ya Afya ambayo inayoonekana na inayowagusa wananchi moja kwa moja.

Mhe. Mtaka ametoa pongezi hizo Desemba 6, 2019 kwenye kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa Afya  mkoani Simiyu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu mjini Bariadi

Mtaka alisema AGPAHI miongoni mwa wadau wa afya mkoani Simiyu shirika ambalo  limefanya kazi nzuri  ambayo inaonekana kutokana na kwamba imekuwa ikifanya vitu vinavyoonekana katik sekta ya afya mkoani humo kwa kusaidia wananchi.

“Nawapongeza sana AGPAHI kazi yenu inaonekana kazi yenu haihitaji tochi ili kuona mnachofanya, huwezi kuzungumzia mafanikio ya mkoa wa Simiyu kwenye sekta ya afya bila kuwataja AGPAHI”, alisema Mhe. Mtaka.

“Tunazo taasisi takribani 14 zinazojishughulisha na masuala ya afya mkoani Simiyu; hawa wadau 13 wangefanya walau robo tu ya kilichofanywa na AGPAHI,tungekuwa na maendeleo makubwa sana katika mkoa wetu na nchi kwa ujumla”,aliongeza Mtaka.

Aidha, Mtaka aliipongeza Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI inayoongozwa na Watanzania kwa kutekeleza miradi inayogusa maisha ya wananchi huku akitoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano wa AGPAHI na kuahidi kushirikiana na wote wa maendeleo mkoani humo ili katika kuwaletea maendeleo wananchi.

 .

“Wajumbe wa bodi ya AGPAHI mna ujasiri wa kutembelea miradi yenu kwenye mikoa kwa sababu miradi ipo.Nyinyi mna vitu,magari yenu pia yamekuwa yakitusaidia sana.Kuna baadhi ya taasisi hazina ujasiri wa kutembelea miradi kwa sababu hawana miradi,wengine kazi yao ni kugonga semina tu mwaka mzima.Hebu tufanye kazi zinazogusa wananchi tubadilishe mkoa huu”,alieleza Mtaka.


Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Dkt. Edith Ngirwamungu alisema AGPAHI inatekeleza miradi yake ya UKIMWI kwa kushirikiana na serikali lengo likiwa ni kuhakikisha fedha zinazotolewa na wafadhili zinawanufaisha watanzania.

“Tunaushukuru mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano mnaotupatia,tunajitahidi kufanya kazi kuwafikia wananchi,AGPAHI tunataka mtoto asizaliwe na maambukizi ya VVU,hivyo tutaendelea kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za VVU na UKIMWI kwa wananchi”,alisema Dkt. Ngirwamungu.

Alisema AGPAHI inaendelea kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma za matunzo na tiba za VVU kwa watoto wachanga,vijana na watu wazima katika mikoa ya Simiyu,Mwanza,Mara na Shinyanga.

Meneja Miradi AGPAHI mkoa wa Simiyu Dkt. Julius Sipemba alisema AGPAHI inatoa huduma za VVU na UKIMWI kwa mkoa mzima wa Simiyu ambapo alibainisha kuwa Simiyu una vituo 233 vya kutolea huduma za afya na 73 kati ya hivyo hupata usimamizi wa moja kwa moja kutoka AGPAHI. Alisema wagonjwa wanaopata huduma kwenye vituo 73 ni sawa na 95% ya wagonjwa wote walioko kwenye vituo 233.

"AGPAHI inaboresha miundombinu kwa kujenga na kukarabati majengo, huduma za maabara kwa kununua madawa na vifaa 'iliwezesha maabara za wilaya kutoka nyota moja mpaka tatu', imetoa magari mapya kwa halmashauri 4 kati ya 6, imetoa pikipiki, msaada wa kuchunguza kifua kikuu, Saratani ya mlango wa kizazi",alieleza Dkt. Sipemba.

Aliongeza kuwa AGPAHI pia inaajiri watoa huduma wa afya kwenye maeneo yenye uhitaji na inatoa mafunzo kwa watoa huduma kulingana na miongozo ya wizara ya afya.


Wakiwa mkoani Simiyu,Wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI wametembelea Kituo cha Tiba na Matunzo cha Hospitali ya Mji wa Bariadi,kukutana na Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu na Mkuu wa mkoa wa Simiyu pamoja na wadau wa VVU na UKIMWI mkoani Simiyu.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu Desemba 6,2019. Kushoto ni Mkurugenzi wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa,kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Dkt. Edith Ngirwamungu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Dkt. Edith Ngirwamungu akizungumza  katika kikao cha wadau wa afya na kueleza kuwa AGPAHI itaendelea kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za VVU na UKIMWI.
 Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt. Festo Dugange akichangia hoja wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.  




Katibu Tawala mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini akichangia hoja wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 


Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.


Kijana James Leonard akielezea jinsi alivyonufaika na Klabu za watoto na vijana zinazohudumiwa na AGPAHI wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 


Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI wakiwa kwenye kikao cha Bodi hiyo na  wadau wa afya mkoani, kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.


Picha ya pamoja uongozi wa mkoa wa Simiyu,AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu mara baada ya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI  na wadau wa Afya mkoani Simiyu kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.


Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji, Dkt. Gamitwe Mahaza akichangia hoja wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 
 Meneja Miradi AGPAHI mkoa wa Simiyu Dkt. Julius Sipemba akiwasilisha mada kuhusu shughuli zinazofanywa na Shirika lisilo la Kiserikali la AGPAHI mkoani Simiyu katika kikao kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi.  




Baadhi ya viongozi na wadau wa afya mkoani Simiyu wakiwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 


Picha ya pamoja uongozi wa mkoa wa Simiyu,AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu mara baada ya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI  na wadau wa Afya mkoani Simiyu kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.



Picha ya pamoja uongozi wa mkoa wa Simiyu,AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu mara baada ya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI  na wadau wa Afya mkoani Simiyu kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.


Baadhi ya viongozi na wadau wa afya mkoani Simiyu wakiwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa AGPAHI na wadau wa afya mkoani Simiyu, kilichofanyika Desemba 06, 2019 Mjini Bariadi. 


Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini akiagana na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI mara baada ya kikao cha Bodi hiyo na  wadau wa afya mkoani, kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  akiagana na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI mara baada ya kikao cha Bodi hiyo na  wadau wa afya mkoani, kilichofanyika Desemba 6, 2019 kilichofanyika Mjini Bariadi.



0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!