Mwekezaji Azhar
Malik kutoka Nchini Malaysia ameonesha nia ya kuwekeza kiasi cha Dola za
kimarekani bilioni 2.5 katika mradi mkubwa eneo la pori la akiba la Kijereshi
na Ziwa Victoria wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, sehemu ya uwekezaji huo ikiwa
ni katika ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji, utamaduni na maeneo
mengine yatakayoimarisha utalii na kutoa ajira kwa wananchi.
Mwekezaji ambaye
amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Ramadhan Dau amesema ikiwa kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa
ikiwemo mradi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwezi Januari 2020,
huku akisisitiza kuwa utatekelezwa bila kuathiri ikolojia na mazingira ya
uhifadhi.
“Nashukuru kwa ushirikiano
nilioupata kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu, pia namshukuru Balozi Dau kwa namna
alivyolisimamia jambo hili tangu likiwa wazo mpaka sasa tunapoelekea kwenye
utekelezaji niwaahidi tu kuwa pale pande zote zitakapofanya maamuzi mikataba
ikisainiwa kwa mujibu wa sheria, mwakani mwezi Januari tutaanza utekelezaji,”alisema
Malik
Kwa upande wake Balozi wa
Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Ramadhan Dau amepongeza uongozi wa Chama na
Serikali kwa utayari walioonesha, akisisitiza ushirikiano wa viongozi hao na
taasisi zote za Serikali zinazohusika, ili mambo yote muhimu yanayohitajika
kufanikisha uwekezaji huo yafanyike mapema kuanzia mwezi Januari kazi ianze.
“Kwa kasi na namna tulivyoanza lile
lengo tulilojiwekea kwamba ikifika Januari 2020 mambo yote yanayohusiana na
taratibu na kusaini mikataba, yanapaswa
yawe yamekamilika na wataalam waje site (eneo la mradi) waanze survey (utafiti)
watengeneze master plan(mpango kabambe), ili kabla ya mwezi Juni 2020 hili
jambo liwe limeanza,” alisema Balozi Dau.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony Mtaka amesema Uwekezaji huu utaupambanua Mkoa wa Simiyu, Kanda ya Ziwa
na kuupambanua utalii kwenye uso wa dunia, ambapo amebainisha kuwa mradi huu
utajibu mahitaji mengi kwenye ajira na kukua kwa maendeleo ya ukanda huo.
Kwa upande wao Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka
ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) wameahidi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha
mradi huu unafanikiwa.
Mradi huu wa uwekezaji katika
sekta ya utalii wilayani Busega utatekelezwa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza
inatarajiwa kugharimu takribani dola bilioni 500 na mpaka kukamilika kwake
utagharimu dola za Kimarekani bilioni 2.5.
MWISHO
Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar Malik(kulia) akiwasilisha taarifa yake ya
uwekezaji katika sekta ya Utalii kwenye Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu
na watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati wa Ziara yake jana
akiwa amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau aliyofanya
kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji
Balozi wa Tanzania
nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akizungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu
baada ya kuwasili mjini Bariadi akiwa na Malik(kulia) ambaye amekubali kuwekeza
katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi
wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na
maeneo mengine yenye kutoa ajira kwa wananchi wakati wa ziara yake jana mkoani
Simiyu,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia) akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Balozi
wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akiwa amefuatana na Mwekezaji
kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar Malik ambaye
amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la
Akiba la Kijereshi wilayani Busega
utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine
yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe. Tano Mwera (kulia) akitoa neon la shukrani mara baada ya
kumalizika kwa ziara ya Balozi wa
Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akifuatana na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw.
Azhar Malik ambaye amekubali kuwekeza
katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la
Kijereshi wilayani Busega utakaojumuisha
ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine yenye kutoa ajira
kwa wananchi mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua jambo katika kikao kati ya viongozi wa
mkoa, Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw.
Azhar Malik ambaye amekubali kuwekeza
katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli
ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani
Simiyu
Balozi wa Tanzania
nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau(wa tano kulia) akizungumza na viongozi wa
mkoa wa Simiyu baada ya kuwasili mjini Bariadi akiwa na Mwekezaji kutoka
Malaysia Azhar Malik(wa pili kushoto), ambaye amekubali kuwekeza katika mradi
mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega
utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine kwenye
Utalii yenye kutoa ajira kwa wananchi wakati wa ziara yake jana mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
akifungua kikao kati ya viongozi wa mkoa,
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw.
Azhar Malik ambaye amekubali kuwekeza
katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la Akiba la
Kijereshi wilayani Busega utakaojumuisha
ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine kwenye Utalii yenye
kutoa ajira kwa wananchi wilayani Busega
mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne
Sagini (kulia) akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan
Dau (katikati) na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar Malik(kushoto) mara baada ya kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa
Mwanza jana, kwa ajili ya kuanza ziara
ya kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani Simiyu.

Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akiteta jambo na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia,
Bw. Azhar Malik wakati wa ziara yake
katika Pori la Akiba la kijereshi wilayai Busega jana ambapo amekubai kuwekeza katika mradi
mkubwa utakaohusisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo
mengine ya kuinua utalii na ajira kwa wananchi.
Balozi wa Tanzania
nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (katikati) akifurahia jambo na baadhi ya
viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na
Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar
Malik(kushoto)mara baada ya ziara ya balozi na mwekezaji huyo katika
Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega
jana, iliyofanyika kwa lengo la
kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii.

Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wengine
wakifurahia jambo wakati wakiagana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt.
Ramadhan Dau (wa tatu kulia) Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar Malik,mara baada ya ziara ya balozi na
mwekezaji huyo katika Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega jana,
iliyofanyika kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta
ya utalii.
Mkurugenzi wa Utalii
kutoka wizara ya maliasili na utalii akieleza mchango wa wizara hiyo katika
kufanikisha mradi utakaotekelezwa na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw.
Azhar Malik, katika Pori la Akiba la Kijereshi
wilayani Busega jana ambapo amekubali
kuwekeza katika mradi mkubwa utakaohusisha ujenzi wa hoteli ya kitalii,
usafirishaji na maeneo mengine ya kuinua utalii na ajira kwa wananchi.
Kutoka kushoto Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Mwekezaji kutoka nchini Malaysia,
Bw. Azhar Malik na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakimsikiliza :- Balozi wa Tanzania nchini Malaysia,
Dkt. Ramadhan Dau, wakati wa ziara yake katika Pori la Akiba la kijereshi
wilayani Busega jana ambapo amekubali
kuwekeza katika mradi mkubwa utakaohusisha ujenzi wa hoteli ya kitalii,
usafirishaji na maeneo mengine ya kuinua utalii na ajira kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wengine wakifurahia
jambo wakati wakiagana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau
(wa tatu kulia) Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar Malik,mara baada ya ziara ya balozi na
mwekezaji huyo katika Pori la Akiba la kijereshi wilayani Busega jana,
iliyofanyika kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta
ya utalii.
Baadhi ya wataalam
wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw.
Azhar Malik(hayupo pichani), katika
sekta ya Utalii kwenye Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega aliyoiwasilisha kwa viongozi
wa Mkoa wa Simiyu na watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati wa
Ziara yake jana akiwa amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt.
Ramadhan Dau aliyofanya kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji.
Mwekezaji kutoka nchini
Malaysia, Bw. Azhar Malik(kulia)
akiwasilisha taarifa yake ya uwekezaji katika sekta ya Utalii kwenye Pori la
Akiba la Kijereshi wilayani Busega kwa
viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii,
wakati wa Ziara yake jana akiwa amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini
Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau aliyofanya kwa lengo la kuangalia mazingira ya
uwekezaji .
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia) akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Balozi
wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akiwa amefuatana na Mwekezaji
kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar Malik ambaye
amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la
Akiba la Kijereshi wilayani Busega
utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine
yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu.
Baadhi ya wataalam
wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw.
Azhar Malik(hayupo pichani) , katika
sekta ya Utalii kwenye Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega aliyoiwasilisha kwa viongozi
wa Mkoa wa Simiyu na watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati wa
Ziara yake jana akiwa amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt.
Ramadhan Dau aliyofanya kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji .
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua jambo (wa tatu kushoto) wakati wa
ziara ya Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akiwa amefuatana
na Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar
Malik ambaye amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya
utalii katika Pori la Akiba la Kijereshi
wilayani Busega utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji
na maeneo mengine yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka na viongozi wengine
wakifurahia jambo wakati wakiagana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt.
Ramadhan Dau (wa tatu kulia) Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar Malik,mara baada ya ziara ya balozi na
mwekezaji huyo katika Pori la Akiba la kijereshi wilayani Busega jana,
iliyofanyika kwa lengo la kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta
ya utalii.
Kutoka kushoto
Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar
Malik, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Balozi wa Tanzania
nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock
Yakobo wakiteta jambo wakati wa ziara ya Balozi na Mwekezaji huyo , ambaye
amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la
Akiba la Kijereshi wilayani Busega
utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine
yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu.
Kutoka kushoto Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Balozi wa Tanzania nchini
Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, wakifuatilia
uwasilishaji wa taarifa ya Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar Malik(hayupo pichani) , katika sekta ya
Utalii kwenye Pori la Akiba la Kijereshi
wilayani Busega aliyoiwasilisha kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na
watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakati wa Ziara yake jana akiwa
amefuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau.
Baadhi ya viongozi
wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya Mwekezaji kutoka nchini Malaysia, Bw.
Azhar Malik(hayupo pichani) ,amabye
amekubali kuwekeza katika sekta ya Utalii kwenye Pori la Akiba la
Kijereshi wilayani Busega
aliyoiwasilisha kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji kutoka Wizara ya
Maliasili na Utalii, wakati wa Ziara yake jana akiwa amefuatana na Balozi wa
Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau(kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kulia) akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Balozi
wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau akiwa amefuatana na Mwekezaji
kutoka nchini Malaysia, Bw. Azhar Malik ambaye
amekubali kuwekeza katika mradi mkubwa kwenye sekta ya utalii katika Pori la
Akiba la Kijereshi wilayani Busega
utakaojumuisha ujenzi wa hoteli ya kitalii, usafirishaji na maeneo mengine
yenye kutoa ajira kwa wananchi mkoani Simiyu.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini (kulia) akizungumza na akizungumza na Balozi wa Tanzania
nchini Malaysia, Dkt. Ramadhan Dau (wa pili kulia) na Mwekezaji kutoka nchini
Malaysia, Bw. Azhar Malik(kushoto) mara
baada ya kuwapokea katika Uwanja wa
Ndege wa Mwanza jana, kwa ajili ya
kuanza ziara ya kuangalia mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani
Simiyu, wengine ni wataalam walioambatana na mwekezaji huyo.