Wednesday, May 27, 2020

HALMASHAURI ZA MKOA WA SIMIYU ZAAGIZWA KULIPA STAHILI ZA MADIWANI

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani hapa kuhakikisha wanawalipa Madiwani stahili zao zote wanazodai kabla ya kuvunjwa kwa mabaraza ya Halmashauri ambayo yanatarajiwa kuvunjwa kabla ya tarehe 10 Juni 2020. Mtaka ametoa agizo hilo Mei 26, 2020...

Tuesday, May 26, 2020

WASHIRIKI NANENANE KITAIFA MWAKA 2020 SIMIYU WAHIMIZWA KUANZA MAANDALIZI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ametoa wito kwa Taasisi, mashirika ya Umma na binafsi na wadau wote wa kilimo, mifugo na uvuvi wanaotarajia kushiriki maonesho ya Kitaifa ya Nanenane mwaka huu kuanza maandalizi ya maonesho hayo. Sagini ameyasema hayo jana mara baada ya kukagua...

Saturday, May 23, 2020

SIMIYU TUMEJIPANGA KIKAMILIFU KUWAPOKEA KIDATO CHA SITA KUANZA MASOMO JUNI MOSI: SAGINI

Na Stella Kalinga, Simiyu RS Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema mkoa huo umejipanga kikamilifu kuwapokea wanafunzi wa kidato cha sita kwa ajili ya kuanza masomo Juni Mosi, 2020 kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe  Magufuli. Akizungumza...

Thursday, May 14, 2020

SEKTA BINAFSI ILELEWE NA IPENDWE-RC MTAKA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa Serikali mkoani hapa kuilea na kuipenda sekta binafsi na kuona namna sahihi ya kutatua changamoto zinazoikabili badala ya kufikiria namna ya kukusanya mapato tu kutoka katika sekta hiyo. Mtaka ameyasema hayo katika kikao maalum...

Wednesday, May 13, 2020

TARURA SIMIYU KUFUNGUA BARABARA ZILIZOATHIRIWA NA MVUA KUZIFANYA ZIPITIKE WAKATI WOTE

Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Eng. Philemon Msomba amesema Serikali imedhamiria kufungua barabara zote zilizoharibiwa na mvua mkoani hapa na kuhakikisha zinapitika kwa mwaka mzima ili kuwarahisisha wananchi  mawasiliano na usafirishaji wa bidhaa...

Saturday, May 9, 2020

WORLD VISION YAKABIDHI VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA SIMIYU

Shirika lisilo la kiserikali la World Vision limekabidhi msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona pamoja na Jengo la zahanati kwa uongozi wa mkoa wa Simiyu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 95.7. Akikabidhi msaada huo jana Mei 08, 2020 kwa Katibu Tawala wa Mkoa...

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!