Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa Serikali
mkoani hapa kuilea na kuipenda sekta binafsi na kuona namna sahihi ya kutatua
changamoto zinazoikabili badala ya kufikiria namna ya kukusanya mapato tu
kutoka katika sekta hiyo.
Mtaka ameyasema hayo katika kikao
maalum cha kujadili Hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 katika Halmashauri ya Mji wa
Bariadi, ambapo Halmashauri ya Mji Bariadi na nyingine za Mkoa wa Simiyu pamoja
na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa. Simiyu zimepata hati safi.
“Viongozi wa Serikali tujifunze
kuilea sekta binafsi, sekta binafsi ni lazima ilelewe na ipendwe pia, tuone
namna ya kutatua changamoto zinazoikabili na kuwafanya watu wapende kufanya
biashara badala ya kufikiria kukusanya mapato tu,” alisema Mtaka.
Mtaka ametoa wito huo kutokana na mapendekezo yaliyotolewa
katika ripoti ya CAG kuwa pamoja na Halmashauri ya Mji Bariadi kupata hati
safi, iko haja kwa Halmashauri hiyo kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na
Usimamizi wa Mapato yatokanayo na vyanzo vya ndani, huku akisistiza
kuweka utaratibu mzuri wa utoaji wa mikopo ya wanawake, vijana na wenye ulemavu
kutoka katika asilimia 10 ya mapato hayo ya ndani.
Aidha, Mtaka amewataka Wakurugenzi wa
Halmashauri zote mkoani Simiyu kuhakikisha wanawalipa madiwani stahili zao
kabla ya muda wao kuisha (kabla ya mabaraza ya amadiwani kuvunjwa,
“tusingehitaji tuvunje mabaraza madiwani wetu wakiwa wanadai stahili zao,
Wakurugenzi wote hili liwe kipaumbele chenu.”
Baadhi ya Madiwani na
wataalam wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi wakiwa katika Kikao maalum cha Baraza
la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa
lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa
fedha 2018/2019.
Diwani wa Kata ya
Nyangokolwa Mhe. Lukonge Nyakali akichangia katika Kikao maalum cha Baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo
la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha
2018/2019.
Mkuu wa wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za Wilaya katika Kikao maalum cha
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020
kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha
2018/2019.
Kamanda wa Polisi wa
Mkoa Wa Simiyu, ACP. Henry Mwaibambe akizungumza katika Kikao maalum cha Baraza
la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa
lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa
fedha 2018/2019.
Mkuu wa wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za Wilaya katika Kikao maalum cha
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020
kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa
fedha 2018/2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Madiwani na wataalam katika Kikao maalum cha
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020
kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa
fedha 2018/2019.
Baadhi ya viongozi
wakiwa katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Wajumbe wa Kamati ya
ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu wakifuatilia Kikao maalum cha Baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichofanyika Mei 12, 2020 kwa lengo
la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha
2018/2019.
0 comments:
Post a Comment