Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani hapa
kuhakikisha wanawalipa Madiwani stahili zao zote wanazodai kabla ya kuvunjwa
kwa mabaraza ya Halmashauri ambayo yanatarajiwa kuvunjwa kabla ya tarehe 10 Juni
2020.
Mtaka ametoa agizo hilo Mei
26, 2020 katika kikao cha baraza maalum la Madiwani wilayani Busega ambacho
kimefanyika kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
"Waheshimiwa madiwani
wamefanya kazi nzuri kwa miaka mitano haitakuwa busara wamalize muda wao wakiwa
wanadai; nisingependa kuona baada ya mabaraza kuvunjwa madiwani waanze kwenda
kwenye ofisi za wakurugenzi kufuatilia madai yao, malipo yao yawe ndiyo kipaumbele
cha Wakurugenzi wetu" alisema Mtaka.
Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njiginya ameahidi kutekeleza agizo la Mkuu wa
Mkoa na kuhakikisha madiwani wote wanalipwa madai yao kwa wakati.
Kwa upande wake Diwani wa
kata ya Imalamate, Mhe. Richard Magoti amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuliweka
suala la malipo ya stahili za madiwani katika mkoa wa Simiyu kuwa kipaumbele,
jambo ambalo limeonesha namna Serikali inavyothamini na kutambua mchango wa
viongozi hao.
Naye Mbunge wa Busega Dkt.
Raphael Chegeni amesema pamoaj na maendeleo yanayoendelea kufanywa na serikali
ya awamu ya tano katika wilaya ya Busega wilaya hiyo inakabiliana na changamoto
ya upungufu wa miundombinu ya elimu kutokana na ongezeko la wanafunzi, hivyo
akatoa wito kwa Serikali kushirikiana na jamii kuona namna ya kukabiliana na
changamoto hiyo.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani la
Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la
kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali(CAG).
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busega, mhe. Vumi Magoti akifungua kikao maalum cha Baraza
la Madiwani la Halmashauri hiyo lililofanyika
Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakifuatilia kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani la
Halmashauri ya Wilaya ya Busega lililofanyika Mei 26, 2020 kwa lengo la
kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali(CAG).
0 comments:
Post a Comment